PICHA ZA WANA USCF-SJUT KATIKA TUKIO LA UZINDUZI WA ALBAMU YA CHOIR YA NEW JERUSALEMU TAREHE 5/7/2015

MGENI RASMI AKIBARIKI DVD ZA ALBAMU YA" MUNGU KWETU SISI NI KIMBILIO"(kulia)TUKIO LA UZINDUZI WA ALBAMU YA CHOIR YA NEW JERUSALEMU TAREHE 5/7/2015

SHEREHE YA KUWAAGA WAHITIMU WANAKWAYA 24 JULY, 2015.

Uongozi wa the New Jerusalem choir ya USCF-CCT St. John's University of Tanzania Tunapenda kuwashukuru wote mliojumuika pamoja nasi kuwaaga wanakwaya wahitimu walionza masomo yao mwaka 2011 na 2012,

KUTIMIA KWA UNABII WA NYAKATI ZA MWISHO

Dalili ya Mvua ni mawingu, hivyo kwa mtu mwenye busara, aliyeanika nguo zake nje anapoona tu mawingu yametanda kila mahali, anajua kwamba mvua wakati wowote inaweza kunyesha, na hakika atafanya haraka kwenda kuzianua nguo hizo.

Tunatoa Huduma ya Kutengeneza na kuendeleza Website na Blogs for free

Blog hii ya USCF-SJUT imetengenezwa na inaendelezwa na Joel Elphas kwa kushirikiana na USCF-SJUT. kwa mawasiliano kuhusiana na kuendeleza Blog hii wasiliana nae kwa namba 0757 755 228 au 0655 755 228 au elphasjoel@yahoo.com Pia tunatoa huduma za kutengeneza Website kwa bei nafuu pamoja na Blog

MAOMBI YENYE UWEZO WA KUPASUA ANGA

Moja kati ya silaha kuu, ambayo inamwezesha mtoto wa Mungu kushinda vita dhidi ya majeshi ya giza, ni maombi. Hofu kubwa kwa shetani na majeshi yake, ni pale anapokuwapo mtu mwenye nguvu ya kuzalisha maombi yaletayo moto, na hatimaye kuleta athari kubwa sana katika ufalme wa giza.

Saturday, January 23, 2016

JIFUNZE BIBLIA INASEMAJE KUHUSU ADHARI NA MATOKEO YA KUFANYA DHAMBI YA UZINZI/UASHERATI KWA MTU ALIYEOKOKA.


ADHARI NA MATOKEO YA DHAMBI YA  UZINZI/UASHERATI KWA MTU ALIYEOKOKA.

Katika Mithali 6:32 Biblia inasema “Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake” na pia katika  Mithali 6:26 inasema “Maana kwa Malaya mtu hutiwa katika hali ya kuhitaji kipande cha mkate; na kahaba humwinda mtu anase nafsi yake iliyo ya thamani”



UZIZI/UASHERATI: Ni tendo la ndoa linalofanywa na mtu mume na mtu mke kinyume na mapenzi ya Mungu/ kabla ya wakati sahihi wa Mungu (Ndoa takatifu).



Ni watu wengi sana ambao wamerudi nyuma na kuanguka katika dhambi hii. Hadi sasa bado kuna kundi kubwa la watu waliokoka ambao bado dhambi hii ina nguvu juu yao na bado wanafanya jambo hili kinyume na mapenzi ya Mungu katika maisha yao.



Si kana kwamba Mungu anafuga dhambi kwa kutokuwadhihirisha hao watu na uovu wao, isipokuwa hataki jina lake litukanwe, kwa kuwa ikijulikana huyo mtu au hao watu wameanguka huenda  kutokana na nafasi zao kiuongozi, kihuduma kiushuhuda nk jina la Mungu litatukanwa sana na mataifa lakini pia hata na wale waliokwisha kuokoka. Kwa lugha rahisi hao watu au huyo mtu atakuwa ametoa nafasi ya jina la Mungu kutukanwa.



Kwa bahati mbaya sehemu kubwa ya watumishi wa Mungu katika makanisa yao hawaoni athari ya hili jambo katika upana wake kama Biblia inavyosema.   Inafika mahali baadhi yao wanawafariji wale walioanguka kwa kusema jipe moyo, tubu na Mungu ni wa rehema atakusamehe. Na wengine utasikia wanasema haukuanza wewe, Daudi naye yalimshinda sembuse wewe!!.



Wengine wanatumia maandiko kabisa wanasema ‘mwenye haki huanguka mara saba’ we mara moja tu wala isikusumbue sana tengeneza tu Mungu atakusamehe, na wengine wanasema mimi mwenyewe nilishindwa kwahiyo, hata wewe isikusumbue saana kazana tu uoe wa kwako au omba upate mume/mke. Ni kama vile watu wanatumia rehema/neema ya Mungu kuendelea kutenda dhambi tena kwa ujasiri.



Sikiliza, si kana kwamba napingana na neno au na mawzo ya hao watumishi wenzangu La hasha!. Nakubali kwamba Mungu husamehe dhambi na maovu  ikiwa ni pamoja na dhambi hii ya uasherati/uzinzi (Matendo ya Mitume 3:19 ‘Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana’).



LAKINI TAMBUA Mungu husamehe kwa sababu 2 kubwa sana:-

Ø  Moja hafurahii kifo cha mwenye dhambi ‘Ina thamani machoni pa Bwana mauti ya wacha Mungu wake’ Zaburi 116:15.

Ø  Na pili ni ili kukurejesha kwenye nafasi yako ili uweze kulitumikia kusudi lake.

Lakini je, unajua madhara/matokeo ya dhambi hii kwa mtu aliyeokoka anapoifanya? Hata kama Mungu akikusamehe/amekusamehe, unajua nini kimetokea/kilitokea kwako pale ulipofanya dhambi hii? Au je unaijua gharama ya kurejea kwenye nafasi yako aliyoikusudia Mungu?





Biblia inasema aziniye na mwanamke afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake? Huenda huwa unausoma tu huo msitari bila kujua uzito wa hayo maneno. Ni vizuri kwanza ukajua kwamba ndani ya nafsi ya mtu ndiko kwenye hisia, nia (utashi), akili, na maamuzi. KUBWA Zaidi kwa Mungu nafsi ndiyo ‘operating system’ kama kwenye computer, kwa maana ndiyo kiwanda kinachotoa tafsiri ya kila kitu ambacho Mungu anazungumza/sema na mwanadamu



MAMBO 3 YANAYOTOKEA MTU ALIYEOKOKA ANPOFANYA DHAMBI HII YA UASHERATI/ZINAA:-



1.   Kuharibika kwa mfumo wa mahusiano na mawasiliano kati yake na Mungu.



Katika  mfumo wa ufalme wa Ki – Mungu ni kawaida kwa mtu aliyeokoka na mwenye mahusiano mazuri na Mungu, kuona Mungu akiwasiliana/akisema naye kwa njia mbalimbali ili kumshirikisha mawazo na mipango yake ikiwa ni namna ya kumuongoza mtu huyo katika kusudi lake chini ya jua.  Hii ina maana suala la mawasiliano kati ya mtu na Mungu ni la kawaida kwa mtu mwenye mahusiano mazuri na Mungu wake.



Sasa mtu anapofanya dhambi hii, athari yake ni hii, dhambi inaharibu mfumo huu wa mahusiano kati ya mtu na Mungu. Na mahusiano kati ya mtu na Mungu yakiharibika mawasilano kati ya Mungu na mtu yanakatika/kuharibika pia. Ninaposema yanakatika ina maana si rahisi kwa Mungu kusema tena na huyo mtu au huyo mtu kusema tena na Mungu wake kwa sababu asili/mazingira hayaruhusu na hili linapelekea mafunuo/sauti ya Bwana kuwa hadimu kwako, kwa kanisa, kwa jamii, kwa kampuni na hata nchi tegemeana na nafasi yako katika ufalme wa Mungu.

2.   Kuharibika kwa mfumo wa kufanya maamuzi/kufikiri ndani yako.

Dhambi hii inaharibu mfumo wa kufanya maamuzi, shetani anapomuongoza mtu kufanya dhambi hii, lengo/interest yake ipo kwenye nafsi ya mtu huyo. Shetani akikamata nafsi ya mtu maana yake amekamata akili/nia ya mtu huyo, akikamata akili ya mtu huyo maana yake amekamata maamuzi yake pia. Na akikamata maamuzi yako amekamata matokeo ya maisha yako ya sasa na ya baadae.



Hivyo mtu huyu hataweza tena kufikiri mambo ya rohoni kama Paulo anavyoagiza kwa Warumi ile sura ya 8:5Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili, bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho”. Hivyo kufanya dhambi hii ni kuathiri mfumo wako wa kufanya maamuzi, na hii ina maana hata Mungu akileta wazo lake kwako huwezi kulipokea maana mfumo wa kuamua umeukabidhi kwa Shetani kwa njia ya zinaa/uasherati.



3.   Kuharibika kwa mfumo wa utiifu ndani yako.



Warumi 2:13 ‘Kwa sababu sio wale wasikiao sheria walio  wenye kuhesabiwa haki, bali ni wale waitendao sheria watakaohesabiwa haki”. Baada ya matokeo hayo 2 hapo juu hiki ndicho kinachozaliwa mwishoni. Ubaya wa dhambi hii inaharibu mifumo hii ambaayo ndiyo misingi ya mwenye haki. Fuatili maisha ya watu wengi sana walioanguka kwenye dhambi hii angalia utiifu wao mbele za Mungu ukoje. Nakuhakikishia utagundua ni ngumu sana kwao kutii maagizo ya Mungu kwao. Mtu wa aina hii hata Mungu akimpa maagizo ya kutekeleza hataweza kwa kuwa tayari mahusiano yamevunjika, mamuzi yametekwa .



JE MUNGU ANATAKA TUJIFUNZE NINI KUPITIA HILI? 



Unapokuwa na mahusiano mazuri na Mungu  hii mifumo yote mitatu/Mambo yote 3 yatafanya kazi vizuri na ndiyo kusudi la Mungu. Dhambi hii inapoingia inasababisha kuharibka kwa mifumo hii mitatu (MAHUSIANO,KUFIKIRI NA UTII). Kitu kibaya au kinacho muumiza Mungu ni kwamba hata kama akikusamehe pale utakapotubu, LAKINI itakugharimu sana kuirejesha mahali pake mifumo hii 3. Na ndio maana neno linasema afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake, kwahiyo utakua unakazi ya kurejesha NAFSI yako katika upya wake na ni garama sana sana tu. Kwasababu kila kilichomo ndani ya nafsi (HISIA, NIA, AKILI, MAAMUZI) kimeangamizwa. Ili kuirejesha mifumo hii maombi ya muda mrefu ya rehema na kutengeza mahali palipobomoka ni ya lazima.  



PENGINE unaweza kusema la muhimu Mungu amenisamehe, hayo mengine sijali sana. Unaweza kusema hayo maneno kama hujui/ huelewi muda unathamani kiasi gani kwa Mungu, na pia mahusiano kati ya muda na Mungu.



NGOJA NIKUAMBIE SIRI YA MUNGU NA MUDA JAPO KIDOGO; Muda na Mungu ni marafiki, na tena wote wana mahusiano mzuri sana.  Muda anaongoza maamuzi ya Mungu na Mungu anaongoza matumizi ya muda kwa kuiweka mipango ndani ya mtu na kumwagiza atekeleze ndani ya muda. Hivyo kwa Mungu muda ni muhimu sana.



Kitu gani namaanisha hapa; Mungu hakutenga/kuweka muda wa mtu kurejesha mifumo hii kwa sababu umeanguka katika dhambi. Katika kipindi ambacho wewe unatubu na kutengeneza kwa Mungu wako ili kurejesha mifumo hii, basi uwe na uhakika upande wa pili umesha athiri kusudi la Mungu duniani kupitia wewe ambalo limefungwa katika muda. Sasa kama utatumia siku tano, mwezi mmoja, miezi sita, mwaka mzima nk, kurejesha hii mifumo basi kwa kipindi hicho chote utakuwa umekwamisha kusudi la Mungu kupitia wewe. Na ndio maana Biblia inasema Shetani anawinda nafsi yako iliyo ya thamani, maana anajua akikamata nafsi yako amekamata akili, nia, hisia na maamuzi yako na hivyo amefanikiwa kuharibu hiyo mifumo na kusababisha mipango ya Mungu isifanyike kwa muda aliokusudia kupitia wewe.



Kwa Mfano; Fikiria umepangiwa na Mungu kusafiri umbali wa kilomita 500 ndani ya masaa saba (7).  Mungu amekupa gari ambalo ni kusudi lake  kwako. Hivyo litazame gari ulilopewa kama kusudi la Mungu kwako na wewe ni dereva. Sasa wewe ukaamua kuliendesha  gari bila kuweka maji kwenye injini. Baada ya kusafiri umbali wa kilomita 300 injini ya gari ikafa kwa kukosa maji na mbele yako zimebaki kilomita 200. Je unajua utakuwa umeathiri kwa kiwango gani kusudi la Mungu? Kutokana na mfano huu, unapotenda dhambi hii  je unajua ni kwa kiwango gani utakuwa umeathiri mipango ya Mungu kupitia wewe duniani kwa kipindi chote ambacho utakuwa unairejesha mifumo iliyopo ndani ya nafsi yako mahali pake?.



Kinacho muumiza/huzunisha Mungu kimsingi si kwa sababu umeanguka dhambini, lakini ni kwa sababu kuanguka kwako dhambini kunamzuia yeye kukutumia wewe mpaka hiyo mifumo yote irejee mahali pake. Hii ina maana interest ya Mungu ipo kwenye muda. Maana anajua itakugharimu wewe muda wa kutengeneza na itamgharimu yeye muda wa kukusubiri wewe utenegeze mifumo hii.



Mpendwa kumbuka hili usije sahau, Mungu hategemei wewe uanguke katika dhambi hii, maana kadri unavyoanguka ndivyo unavyokwamisha na kuchelewesha kazi ya Mungu duniani kupittia wewe. Je unajua hasara na matokeo ya kukwamisha na kuchelewesha kazi ya Mungu?



Je katika nafasi ambayo Mungu amekupa Kazini, huduma, au kanisa unachunga kwa kiasi gani nafsi yako isiharibiwe na dhambi hii? Neno linasema Matendo ya Mitume 20:28Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe”.

Naamini ujumbe huu utakusaidia kuhakiksha unafanya maamuzi ya kutofanya tena dhambi hii si kwa sababu imeandikwa tu usizini bali ni kwa sababu unampenda Mungu na unataka kuhakikisha kusudi la Mungu linafanikiwa bila kukwamishwa kwa dhambi hii.



                                                   Mwisho.

                            ******** MUNGU ATUSAIDIE. *********


Share:

Friday, January 22, 2016

FAHAMU KUHUSU SAUTI YA MUNGU KWAKO.


FAHAMU NAMNA YA KUSIKIA NA KUIELEWA SAUTI YA MUNGU ILI IKUSAIDE KATIKA KUFANYA MAAMUZI.



Lengo kuu la somo hili ni kumsaidia Mwanadamu yeyote yule aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu kujua namna anavyoweza kusikia Sauti ya Mungu na Kuielewa Sauti ya Mungu. Kwanini? Kwasababu ni wachache sana wanao sikia na kuilewa sauti ya Mungu pamoja na kuwa Mungu huzungumza nao mara kwa mara. Wengine hujiuliza swali hili; Je ni kweli Mungu anazungumza na mwanadamu hata sasa? Hili ni moja ya swali ambalo watu wengi wamekuwa wakijiuliza na kukosa majibu muafaka kwani baadhi yao hawaamini kwamba ni kawaida ya Mungu kuzungumza na wanadamu. Kama ilivyokuwa katika agano la kale, agano jipya, naam hata sasa, Mungu ni yeye yule jana na leo na hata milele.

Maandiko yanadhibitisha wazi kuwa ni kweli Mungu anazungumza na mwanadamu hata hivi leo na si Mitume na Manabii tu tunaowasoma katika Biblia, lakini hata mimi na wewe katika ukawaida wetu Mungu husema nasi.



Mungu anasema “Enyi watu, nawaita ninyi; Na sauti yangu ni kwa wanadamu” (Mithali 8:4). Hivyo ni kusudio la somo hili kuongeza ufahamu wako ili uweze kujua ni kwa namna gani Mungu huzungumza na mwanadamu na kisha nini ufanye ili kumuelewa Mungu anapozungumza na wewe. Ni muhimu kwanza tujiulize swali hili muhimu tunapotafakari somo hili, Kwa nini Mungu azungumze/aseme na mwanadamu? Jibu la swali hili, linalenga kutaka kujua sababu za Mungu kuzungumza na mwanadamu au mwanadamu anahitaji kuisikia sauti ya Mungu ili:-

       I.            Aishi sawasawa na kusudi au mapenzi ya Mungu awapo hapa duniani. Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama. (Zaburi 32:8)

   II.            kujenga na kudumisha mahusiano/mawasiliano mazuri kati yake na Mungu. Kutoka 33:11 Naye Bwana akasema na Musa uso kwa uso, kama vile mtu asemavyo na rafiki yake. Kisha akageuka akarejea hata maragoni; bali mtumishi wake Yoshua, mwana wa Nuni, naye ni kijana, hakutoka mle hemani

III.            kuona kama Mungu aonavyo na hivyo kutafsiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni. Yeremia 1:11-12 “Tena neno la Bwana likanijia, kusema, Yeremia, waona nini? Nikasema, Naona ufito wa mlozi. Ndipo Bwana akaniambia, Umeona vema, kwa maana ninaliangalia neno langu, ili nilitimize.



MAMBO MHUMU YA KUJUA KUHUSU SAUTI YA MUNGU

Yafuatayo ni baadhi ya mambo muhimu ya kukusaidia kuijua, kuisikia na kuielewa sauti ya Mungu, nawe hunabudi kuyafahamu na kuyatenda:-

1.     Jenga na kudumisha mahusiano mazuri na Roho Mtakatifu – Ni vizuri ukafahamu kwamba Roho Mtakatifu yupo duniani sasa akiliongoza kanisa katika kuyatenda mapenzi ya Mungu. Hivyo uwepo wa mahusiano mazuri kati yako na Roho Mtakatifu ndio ufunguo wa mawasilaino mazuri kati yako na Mungu. Biblia inasema wazi kabisa katika 1Wakorinto 2:10

Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu… vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu”. Andiko hili linatuonyesha umuhimu na nafasi ya Roho Mtakatifu katika kutusaidia kuisikia sauti ya Mungu. Hivyo jenga na kudumisha uhusiano wako na yeye, itakusaidia sana katika kiujua na kuisikia sauti ya Mungu.



2.     Ongeza ufahamu wa viashiria (signal) vya mawasiliano kati yako na Mungu Ufahamu wa viashiria (signal) za mawasiliano kati yako na Mungu ni wa lazima ili kusikia na kuielewa sauti ya Mungu. Zipo alama mbalimbali kwa kila mwamini ambazo Mungu hutumia katika kusema naye. Biblia katika 1Samweli 3:9 inasema “… Enenda, kalale, itakauwa AKIKUITA, utasema, Nena, BWANA; kwa kuwa mtumishi wako anasikia…” Kwahiyo kiashiria kimojawapo ambacho Mungu anakitumia kusema na Mwanadamu ni KUITA, naam anaweza kukuita kwa sauti itokayo kinywani pake au KWA NJIA KUKULETEA ALAMA/VIASHIRIA VYENYE KUKUFANYA UJUE MUNGU ANANIITA.



Kama ilivyo kwa jinsi ya kibinadamu anayekuita si lazima aongee, anaweza kutumia alama za mikono au hata maandishi nk, kukuita. Katika kukuita kwa njia ya viashiria/alama Mungu anaweza kuleta nguvu/msisimuko/ubaridi/maumivu fulani kwenye sehemu ya mwili wako au huzuni moyoni mwako kama ishara/kiashiria cha uwepo wake juu yako na hivyo KUTAFUTA/KUTAKA USIKIVU WAKO ILI ASEME NAWE. Hivyo ni lazima uwe na ufahamu na utafute kujua kuhusu alama/namna ya kwako ambayo Mungu hutumia kutafuta usikivu wako.



N: B Tambua kuwa Ipo namna ya kwako ambayo Mungu hupenda kusema na wewe ambayo inaweza kabisa ikawa tofauti na anavyosema na rafiki yako, Mke, Mume au ndugu yako. Ni jukumu lako kujua viashiria hivyo kwa upande wako kwa kumuuliza Roho Mtakatifu pekee ambae hutufunulia siri za Mungu. Usijefanya vitu kwa Mkumbo au kuiga kutoka kwa rafiki yako na ikakugharimu.



3.     Ni lazima ujue kutofautisha sauti ya Mungu na sauti nyingine. Hapa ndipo penye mtihani mkubwa sana kwa watu wengi mno, kama ilivyokua kwangu kabla sijajifunza kuhusu jambo hili. Ni muhimu sana kwako kulielewa ili usije ukaipuuza sauti ya Mungu kwa kudhani ni mawazo yako au ni ya Shetani au usije ukatekeleza jambo ukiamini kwamba Mungu amesema nawe kumbe Shetani ndiye alisema nawe. Shida ya namna hii aliipata Samweli wakati huo akiwa mtoto na Mungu alikusudia kumuita kwaajili ya Taifa la Israeli. Mungu alimuita kwa sauti yake lakini hakuitambua, badala yake alifananisha na sauti ya Babu yake Mzee Eli. Maandiko yanasema “Ikawa wakati huo, Eli alipokuwa amelala mahali pake (tena macho yake yalikuwa yameanza kupofuka, hata asiweze kuona), na taa ya Mungu ilikuwa haijazimika bado, na Samweli alikuwa amelala katika hekalu la Bwana, palipokuwa na sanduku la Mungu; basi, wakati huo Bwana akamwita Samweli; naye akasema, Mimi hapa. Akamwendea Eli kwa haraka, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Akasema, Sikukuita; kalale tena. Naye akaenda, akalala tena. Bwana akaita mara ya pili, Samweli! Samweli! Akaondoka akamwendea Eli, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Akajibu, Sikukuita, mwanangu; kalale tena. Basi Samweli alikuwa hamjui Bwana bado, na neno la Bwana lilikuwa bado halijafunuliwa kwake. Bwana akamwita Samweli mara ya tatu. Naye akaondoka akamwendea Eli, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Ndipo Eli akatambua ya kuwa Bwana ndiye aliyemwita yule mtoto. Kwa hivyo Eli akamwambia Samweli, Enenda, kalale; itakuwa, akikuita, utasema, Nena, Bwana; kwa kuwa mtumishi wako anasikia. Basi Samweli akaenda akalala mahali pake. Bwana akaja, akasimama, akaita vile vile kama kwanza, Samweli! Samweli! Ndipo Samweli akasema, Nena, Bwana; kwa kuwa mtumishi wako anasikia (1Samweli 3:2-10). Ni muhimu ukaelewa kwamba Mungu anaweza kusema na wewe hata kama uko katikati ya mkutano wa watu wenye kelele nyingi sana. Hii ni kwa sababu Mungu hatumii mdomo kusema nasi bali anatumia moyo wako kuzungumza. Moyo ndio kiungo muhimu cha mawasiliano kati ya mtu na Mungu.



Ukisoma katika Matendo ya Mitume 12:22 Biblia inasema “Watu wakapiga kelele, wakasema, Ni sauti ya Mungu, si sauti ya Mwanadamu. Mara malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu; akaliwa na chango, akatokwa na roho”. Kauli hii ya watu ilikuja baada ya Mfalme Herode kuhutubia watu na kutoa maneno makuu. Watu waliamini kwamba ile ilikuwa sauti ya Mungu, kumbe sivyo na matokeo yake Herode alipigwa na Mungu akafa.



Katika hili nataka nikupe Tahadhari ndugu mpendwa, kuna wakati mtu/watu au watumishi wanaweza kunena mambo makubwa na watu wakadhani Mungu wa kweli anasema ndani yao, kumbe ni mungu wa dunia hii. Na ndio maana ni muhimu sana wewe binafsi uongeze ufahamu wako katika kuijua, kuisikia na kuielewa sauti ya Mungu, ili hata mwanadamu akinena unajua kwamba hili limetoka kwa Mungu wa kweli au vinginevyo.



Naam! mpendwa zipo sauti mbalimbali ambazo zote zinalenga kupambana/kuharibu kusudi la Mungu ndani ya mtu, zipo sauti za wanadamu (wazazi, walezi, mwenza wa ndoa, viongozi wa kiroho), ipo sauti ya Shetani kupitia majeshi ya pepo wabaya nk. Ni lazima mwanadamu amjue sana Mungu kiasi cha kutosha ili kuweza kutofautisha sauti hizi. Njia au namna pekee ya kutofautisha sauti hizi na ile ya Mungu ni kuwa na uelewa au ufahamu mkubwa wa Neno la Mungu pekee, kwasababu Mungu hawezi hata siku moja kukuagiza jambo lililo kinyume na Neno lake.



FAHAMU VIKWAZO VINAVYOWEZA KUPELEKEA KUTOKUSIKIA SAUTI YA MUNGU.

Biblia imeainisha vikwazo kadhaa vyenye kupelekea mtu kutokuisika sauti ya Mungu. Nitakuonyesha vikwazo 2 vikubwa na nikupe changamoto ya kuingia ndani Kiimandiko ili kujua vikwazo vyengine:-

       I.            Dhambi au kuishi maisha ya dhambi. Mungu hapendezwi na Mtu anayeishi katika mazingira au maisha ya dhambi, (1Yohana 3:4) “Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi”. Maana yake ni kuwa atendaye dhambi anakua amemuasi Mungu, kwahiyo amekwenda kinyume na sheria iliyowekwa na Mungu. Matokeo yake mtu huyo na Mungu wanakua mbali kila mmoja akiacha kujishughulisha na mwenzie. Isaya 59: 1-2 Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia”. Angalia lilee neno ‘HATA HATAKI KUSIKIA’.



    II.            Kukosa uaminifu. (Hesabu 12:7-8,). Mungu hupendezwa sana na Mtu aliye mwaminifu kwake siku zote za maisha yake. Kwa mtu huyo Mungu hujenga mahusiano ya karibu kwa haraka mno na hata kusemezana nae Zaidi. Maandiko yanalidhibitisha hili pale Mungu aliposema mwenyewe akiwaambia Haruni na Miriamu Bwana akashuka katika nguzo ya wingu akasimama pale mlangoni pa Hema, akawaita Haruni na Miriamu, nao wakatoka nje wote wawili. Kisha akawaambia,Sikizeni basi maneno yangu;Akiwapo nabii kati yenu,Mimi,Bwana,nitajifunua kwake katika maono,Nitasema naye katika ndoto. Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote; Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la Bwana yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa? (Hesabu 12:5- 8). Uhusiano wa karibu sana aliokua nao Musa na Mungu ulitokana na UAMINIFU aliokua nao Musa mbele za Mungu. Mungu alimpenda na kuamua kuingilia kati kwa yeyote yule aliyejaribu kufuatilia au kugusa maisha ya Musa, hakika ni kama alikua akigusa maisha ya Mungu kwasababu haukunyamaza hata kidogo. Cheki kilichomtokea Miriamu baada ya kumsemasema Musa kwa habari ya Mke wake “Hasira za Bwana zikawaka juu yao; naye akaenda zake. Kisha hilo wingu likaondoka kutoka pale juu ya hema; na tazama, Miriamu akawa mwenye ukoma, mweupe kama theluji; Haruni akamwangalia Miriamu, na tazama, yu mwenye ukoma. Kisha Haruni akamwambia Musa, Ee bwana wangu nakusihi sana usituwekee dhambi juu yetu, kwa kuwa tumefanya ya upumbavu, na kufanya dhambi. (Hesabu 12:9-10). Kwa muda wako unaweza soma habari za Samweli katika ile 1Samweli 2:26-35 utajifunza kitu kuhusu uaminifu kupitia wito wa Samweli.

Ipo mifano ya wanamapinduzi wengi amabo walifanya mambo makubwa wakiongozwa na sauti ya Mungu katika kila jambo; akina Daniel, Paulo, Samweli, Yoshua na wengine wengi. Maisha ya uaminifu mbele za Mungu ndiyo ilikua silaha kubwa ya mafanikio na ushindi wao dhidi ya wengine.



MAMBO YATAKAYOWEZA KUKUSAIDIA KUJUA NA KUISIKIA SAUTI YA MUNGU KATIKA MAISHA YAKO.



       I.            Unahitaji kufahamu umuhimu wa Mungu kuzungumza/kusema nawe. Zipo sababu nyingi za Mungu kuzungumza na wanadamu laikini kubwa yenye kuzibeba zote ni ile iliyoandikwa katika Zaburi 32:8 kwamba Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama”. Kwanini? Kwasababu mwanadamu haishi duniani kwa muda ambao Mungu amemuweka kwa kusudi lake mwenyewe, bali ni kwa kusudi la Mungu pekee.

Ndivyo maandiko yanavyotueleza ukisoma kitabu cha (Warumi 8:28)Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. Kwahiyo ili uweze kulitumikia vizuri kusudi la Mungu katika maisha yako sharti ni kwamba; lazima uongozwe nay eye katika njia sahihi. Na njia mojawapo ni ya Mungu kusema na wewe. Lengo lake katika kusema na wewe ni kukuongoza katika njia sahihi kwa kukuondoa kwenye makusudi ambayo yapo nje na mapenzi yake kwenye maisha yako maana imeandikwa “Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani; Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao,Ili amwondoe mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi; Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni, Na uhai wake usiangamie kwa upanga” (Ayubu 33:14-18)



    II.       Ongeza ufahamu wako kuhusu ulimwengu wa roho. Mambo yote yanayotokea katika ulimwengu wa mwili yameanzia katika uilimwengu wa roho, naam maamuzi ya kile ambacho hutokea katika ulimwengu wa mwili hufanyika katika ulimwengu wa roho. Zaidi hata mapambano (vita vya kiroho) yote aliyoanayo mwanadamu katika kulitumikia kusudi la Mungu hufanyika katika ulimwengu wa roho.

Hivyo kuwa na ufahamu wa ulimwengu wa roho hususani namna ya kuishi na kuwasiliana katika ulimwengu huo ni muhimu sana kwa mwamini mwenye kutafuta kujua na kuisikia sauti/mawazo ya Mungu katika maisha yake. Kwa kuwa Mungu ni roho kama alivyo na Shetani pia. Hebu tusome habari ya Elisha na Mtumishi wake, 2 Wafalme 6:8-17. Maandiko yanatueleza kwamba Shetani nae ni roho ukisoma Waefeso 6:10-12.



Ndugu mpendwa usiruhusu yale unayoyapitia au yale ambayo watu /mazingira yanasema juu yako yabadilishe au kuongoza maisha yako, bali tafuta kuijua na kuielewa sauti ya Mungu kwenye maisha yako. Na ndiyo maana somo hili limekuja ili kukusaidia kufika mahala ambapo utaweza kuyatenda mapenzi kamili ya Mungu kwenye maisha yako.






Share:

Tuesday, January 12, 2016

wahi ibada

Mpendwa zingatia muda wa ibada zetu na Mungu atakubariki sana.
Share:

Friday, January 8, 2016

KARIBU NA SHIRIKI IBADA YA USCF-CCT KILA JUMAPILI..

Tunazidi kukumbusha na kukujulisha kwamba, ibada zetu za kila jumapili zinaendelea kama kawaida. Kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 3:00 asubuhi. Karibuni sana.
Share:

MY LUNCH IS YOUR HAPPINESS!!


Share:

USCF-SJUT NEWS

Designed by Joel Elphas @ 2015. Powered by Blogger.

Recent Posts