Wednesday, August 5, 2015

MATUKIO YA KIBIBLIA YA NYAKATI ZA MWISHO NA: DR. GODWIN GUNEWE

MATUKIO YA KIBIBLIA YA NYAKATI ZA MWISHO

NA: DR. GODWIN GUNEWE

KUTIMIA KWA UNABII WA NYAKATI ZA MWISHO

   Dalili ya Mvua ni mawingu, hivyo kwa mtu mwenye busara, aliyeanika nguo zake nje anapoona tu mawingu yametanda kila mahali, anajua kwamba mvua wakati wowote inaweza kunyesha, na hakika atafanya haraka kwenda kuzianua nguo hizo. Vivyo hivyo, Yesu Kristo anatuonya katika maandiko juu ya kuzitambua ishara za zama hizi yaani ishara za nyakati hizi za mwisho, na kujua yale yanayokuja hivi karibuni ili tujiandae vema kuyakabili. Biblia inasema katika Mathayo 16:2-3 “Akajibu, akawaambia kukiwa jionimwasema, kutakuwa na kianga; kwa maana mbingu ni nyekundu na asubuhi, mwasema, Leo kutakuwa na dhoruba; kwa maana mbingu ni nyekundu, tena kumetanda. Enyi wanafiki, mwajua kuutambua uso wa mbingu: lakini Je? Ishara za zama hizi hamwezi kuzitambua?”

DALILI ZA MWISHO WA DUNIA.
  Kila kilicho na mwanzo hakikosi kuwa na mwisho, na mwisho wa dunia umekaribia sana. Dalili mbalimbali za mwisho wa dunia, zinatajwa katika sehemu mbalimbali katika Biblia.kwa mfano katika Mathayo 24:3-14 Biblia inasema, “Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakasemaTuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia? Yesu kajibu, akawaambia, Angalieni mtu asiwadanganye Kwa sababu wengi watakuja Kwa jina langu, wakisema, Mimi ni kristo; nao watadanganya wengiNanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita; angalieni, msitishwe; maana hayo hayana budi kutukia; lakini ule mwisho bado. Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na njaa, matetemeko ya ardhi mahali mahali. Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu. Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao wawaua; nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu. Ndipo wengi watakapojikwaa nao watasalitiana, na kuchukiana. Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi. Na kwa sababu ya kuongezaka maasi mengi upendo wa wengi utapoa. Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka. Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.” Pia tukiangalia katika kitabu cha 1 Timotheo 4: 1-5 Biblia inasema “Basi roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na Imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe; wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.” Kadhalika tukiangalia katika kitabu cha2 Timotheo 3: 1-5 Biblia inasema, “Lakini ufahamu neno hili yakuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi,wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio taka kufanya suluhu, wasio na shukrani,wasio safi, wasio wapenda wa kwao, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda mungu, wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake, hao nao ujiepusha nao.” Dalili zote hizi zimekwishatimia, na zinazidi kuwa dhahiri mbele ya uso wa dunia kila iitwapo leo. Ni vizuri pia kufahamu kwamba moja ya utendakazi wa nabii wa uongo, ni ishara na ajabu za uongo, kimsingi dalili hii iko wazi zaidi, kwani ulimwengu wote sasa, umetekwa na Ishara na miujiza ya uongo kutoka kwa watenda kazi wa shetani, ingawa ipo miujiza ya kweli inayotoka kwa Mungu.

MAKRISTO WA UONGO.
   Katika kitabu cha Marko 13:22-23 Biblia inasema, “Kwa maana wataondoka Makristo wa uongo, watatoa Ishara na maajabu, wapate kuwadanganya, kama yamkini hata hao wateule.Bali ninyi jihadhalini; nimekwisha kuwaonya yote mbele.” Makristo wengi sana wa uongo wametokea hapa duniani tangu unabii huu ulipotolewa.Na kila mmoja amekuja kwa sura na mtazamo tofauti kabisa na jinsi maandiko yanavyozungumza juu ya Kristo wa kweli.Na hii ilimthibitishia kila mtu kuwa hao ni makristo wa uongo, kwa mfano nchi kama Zambia, Kongo, Kenya, Tanzania na nchi mbalimbali za jirani, walikwishawahi kutokea watu waliojiita hao ndiye kristo lakini baadaye waliishia kuaibika. Kwa ujumla nchi nyingi sana duniani wameibuka makristo wengi sana wa uongo na wamedanganya wengi. Asilimia kubwa ya wateule katika kanisa la leo, wapo kwenye hatari kubwa sana ya kuachwa wakati wa unyakuo wa watakatifu, na hii ni kutokana na wakristo hao kupenda kufuata makanisa yanayohubiri miujiza zaidi kuliko kufundisha neno la Mungu na hivyo kuwafanya wawe mwilini sana. Pia mafundisho ya Mashetani yamekuwa kivutio kikubwa sana kwa wateule wengi katika kanisa la leo, hivyo kupelekea maasi kuongezeka sana yamkini hata nyumbani mwa Mungu, kwa kuwa neno halisi la Mungu limekuwa adimu sana kwenye makanisa hayo.

WACHAFU WATAZIDI KUWA WACHAFU NA MAASI KUONGEZEKA.
(Ufunuo 22:11, Mathayo 24:12).
  Yapo matukio mengi sana ya aibu na ya kutisha, yanayotokea kila siku katika dunia yetu, na matukio haya yanadhihirisha wazi kutimia kwa unabii unaosema“Wachafu watazidi kuwa wachafu”. Uchafu unaotajwa hapa ni ulawiti.Katika nchi yetu, pamoja na sheria kali ya kujamiiana, ambayo inawafanya watu wanao najisi watoto wadogo au wabakaji na walawiti, kupewa adhabu ya kifungo cha maisha; bado vitendo hivi vinaongezeka kwa kasi sana kama vile watu hawajali! Karibu kila siku tunasikia habari hizi katika vyombo vya habari. Wengine wanaripotiwa kulawiti watoto wadogo waliowazaa wenyewe! Wengine wanalawiti vikongwe! Wengine wanalawiti wanyama.Wengine wanawabaka mama zao! Mtu mmoja anaripotiwa kulawiti watoto wadogo watano wa shule ya msingi zamu kwa zamu! Pia kiongozi mmoja wa dhehebu la kikristo anaripotiwa kumlawiti mtoto wa kiume wakiwa ndani ya gari maeneo ya chuo kikuu cha Dar -es- salaam! Waziri mkuu mmoja wa nchi moja ya Ulaya anataka ushoga uwe halali kupitia bunge la nchi yake. Maaskofu wa dhehebu moja kubwa la kikristo, hivi karibuni wamepiga kampeni ya kutaka ushoga uhalalishwe! Hakika wachafu watazidi kuwa wachafu! Katika nchi ya Tanzania kumeripotiwa matukio mengi sana ya mauaji ya vikongwe na maalbino. Wanaume wengi hapa duniani wamelipotiwa kuwaacha wake zao, kwa sababu ya ulawiti!. Huko Marekani na ulaya ndoa za wanaume kwa wanaume (mashoga) na ndoa za wanawake kwa wanawake (wasagaji) zinazidi kuongezeka kila siku. Mchungaji mmoja wa dhehebu la kikristo hapa nchini Tanzania anaripotiwa kushiriki biashara haramu ya viungo vya wanadamu (Albino). Miezi michache iliyopita viongozi wa dhehebu kubwa la kikristo huko nchini Marekani wameripotiwa kuwalawiti watoto wadogo! Hata hivyo makanisa mengi, katika nyakati za leo, yanahusianishwa na nguvu za kishetani na hata kupelekea kupoteza wateule wengi. Katika kitabu chake Iyke Nathan Uzorma Kiitwacho Mkuu wa wachawi sasa ampokea Kristo Ukurasa wa 38 na 39 anataja kwa uwazi kabisa kuwa makanisa yafuatayo kuwa ni makanisa ya shetani:- Kanisa la shetani San Francisco nchini Marekani lililoanzishwa mwaka 1996 na kuhani mkuu wa shetani, aliyeitwa Anton Laveyambaye pia ndiye mwandishi wa biblia ya shetani, kadhalika kanisa la Wicca la California Marekani lililoanzishwa na Askofu Mkuu aitwaye Frost ambaye pia ni mwandishi wa kitabu kiitwacho “Sanaa ya Wachawi”. Yapo makundi mengi sana ya Imani potofu (Cults) hapa ulimwenguni ambayo yanatenda kazi karibu kila nchi duniani ili kuweza kutimiza kusudi la kuwapoteza wateule. Ni vizuri kuwa makini na mwangalifu sana kabla ya kujiunga na kanisa lolote, ni lazima kumuomba Roho Mtakatifu akuongoze ili usije ukaingia kwenye mtego wa shetani na hatimaye ukajikuta unaitazamia jehanum ya moto. Na wachungaji ambao wanapenda urahisi na kutaka kujiunga kwenye makanisa yenye pesa, kwa kudhani kuwa maisha yao na huduma zao zitainuliwa, tafadhali nawaomba muwe makini sana la sivyo utajikuta utumishi wako uliojengwa kwa muda wa miaka mingi unabomoka kwa siku moja. Ni bora ukubali kuteseka, na Mungu wetu ni mwaminifu atakuinua; kuliko kujiunga na kanisa lenye pesa ambalo limeweka mikataba na shetani. 
     Ukweli ni kwamba, wapo watu wengi sana ambao wanafanya kazi kama mitume, wachungaji, manabii, wainjilisti, na walimu lakini kumbe ni watumishi wa shetani. Katika neno lake Bwana Yesu, anatusisitizia na kutuonya kwamba, Baadhi ya watumishi wa Mungu tunaowaona ni mateka wa shetani na wachawi ambao wanafanya kazi hata katika makanisa mbalimbali ya Kipentekoste, Unabii huu ulitolewa na mtumishi wa Mungu mtume Paulo, na hakika kwa sasa unabii huu upo dhahiri kabisa, katika kitabu cha 2 Wakorintho 11: 13-15 Biblia inasema, “ Maana watu hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila,wanaojigeuza wawe mfano wa  mitume wa Kristo wala si ajabu maana shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa Malaika wa Nuru. Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.”
     Kwa ujumla, vitabu vifuatavyo vya Biblia vinaweka wazi, unabii wa dalili za mwisho wa dunia. ( Danieli 12:4, Mathayo 24:3-14, Marko 13:3-27, Luka 21:7-32, 1 Timotheo 4:1-5, 2 Timotheo 3:1-5, Ufunuo 22:6-7).

Orodha ya unabii wa matukio ya nyakati za mwisho.
1         Maarifa kuongezeka (Daniel 12:4).
2         Wengi kuja kwa jina la Kristo na kudanganya wengi (Mathayo 24: 4, Marko13:5).
3        Habari na matetesi ya vita (Mathayo 24:6).
4        Taifa kupigana na taifa, ufalme na ufalme, njaa na metetemeko ya ardhi
   (Mathayo 24:7, Marko 13:8).
5.         Kutokea kwa manabii wa uongo na kudanganya wengi ( Mathayo 24:11,
       Marko 13:22).
6.         Kuongezeka kwa maasi na upendo wa watu kupoa ( Mathayo 24;12)
7.         Wengi watajitenga na Imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na   
   mafundisho ya mashetani (1Timotheo 4:1)
8.      Watu kuzuiliwa kuoa na watu kuamuriwa wajiepushe na vyakula ambavyo mungu aliviumba (1 Timotheo 4:3)
9.         Watu kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi
 (2 Timotheo 3:2, Marko 13:12).
10.     Wasiowapenda wakwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu (2 Timotheo 3:3-4).
11.  Wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake mola. (2 Timotheo 3:5).
12.  Wachafu kuwa wachafu (Ufunuo 22:11).
13.  Magojwa ya kutisha yasiyo na dawa (pestilences) Mathayo 24:7(King James version).
14.  Wengi watajikwaa na kusalitiana, na kuchukiana(Mathayo 24:10)

Je unaijua dalili ya mwisho kabisa ya mwisho wa dunia?
   Ni jambo la kusikitisha sana kuona mkristo aliyesimama vema kiroho anarudi nyuma katika nyakati hizi za mwisho. Pia ni jambo linaloumiza sana kuona mtu aliyeokolewa kwa neema, anafanya mchezo na dhambi katika nyakati hizi za hatari. Ndugu mpenzi msomaji, ni vizuri kutambua kwamba, Yesu Kristo atarudi siku yoyote kuanzia sasa. Kama wewe siyo mwana wa Ufalme, ni ngumu sana kulielewa hili, kama ilivyokuwa Nyakati za Nuhu.
  Pamoja na dalili nyingi kutajwa katika vitabu mbalimbali, Bwana wetu na Mungu wetu Yesu Kristo alitupa dalili moja ambayo ndiyo inayoashiria kufika mwisho kabisa kwa dunia; dalili hii ni Injili kuhubiriwa ulimwenguni mwote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote. Katika kitabu cha Mathayo 24:14 Biblia inasema, “Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote, hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.”
  Ni muhimu kufahamu kwamba madhehebu karibu yote yanahubiri  Injili ulimwenguni, yakishirikiana na stesheni karibu zote za Radio za kikristo ulimwenguni,pia stesheni karibu zote duniani za televisheni kama vile TBN na JCTV zilizopo Marekani, Mashirika karibu yote ulimwenguni ya uchapaji maandiko ya kikristo, wote kwa pamoja kwa nia moja na moyo mmoja, waliungana kama shirika liitwalo “AD 2000 and BEYOND MOVEMENT” wakiwa na lengo la kuhakikisha kwamba ulimwengu wote unahubiriwa Injili kufikia Desemba 31, 2000. Shirika hili liliongozwa na Mmarekani mmoja aitwaye Louis Bush na kuungwa mkono na wahubiri wote duniani kama vile Bill Graham wa Marekani, Dr. David Yongcho wa Korea na wengine wengi. Kadhalika wafanya biashara wakubwa duniani, makampuni ya uchapaji maandiko matakatifu, waigizaji filamu za neno la Mungu, wanasayansi wakubwa duniani na wakristo wengi walio na majina makubwa hapa duniani wote waliweka nguvu zao katika kutimiza maadhimio ya shirika hili.Wote hawa walikaa kwa pamoja nchini Afrika kusini, Pretoria mwaka 1997. Kumekuwa na makusanyiko kama haya tangu mwaka 1974, na lengo kuu la makusanyiko haya ni kupanga mikakati ya kuhubiri injili dunia nzima mpaka kufikia mwaka 2000. Wako wataalamu wa mambo ya takwimu ambao walifanya utafiti na kuweza kuigawa dunia katika makundi ya kijamii elfu kumi na mbili (12,000). Na utafiti huo ulionyesha kwamba mpaka mwaka 1997 makundi elfu kumi (10,000) yalikwishafikiwa na injili. Kwa hiyo nguvu zote zilielekezwa kwa makundi elfu mbili (2,000) yaliyobaki.Kazi hii iliyochochewa na maombi ya watu zaidi ya milioni hamsini kutoka katika makanisa mbalimbali duniani wanaoomba masaa 24 kila siku, kuhakikisha lengo hili linatimia; na pia ilichochewa na matumizi ya tekinologia ya kisasa ya kuhubiri Injili kama “Internet” “satellite” n.k quicken
  Kwa kutumia teknologia ya kisasa, Injili inahubiriwa kwa kasi ya ajabu. Kwa mfano kwa kutumia “satellite” Mwinjilisti Mmoja anayeitwa Billy Graham, tarehe 14 Aprili, 1996, alihubiri Injili na nchi zote ulimwenguni waliweza kusikia kwa wakati huohuo, wakati yeye akiwa marekani. Hivi leo ulimwenguni, stesheni za Radio na Televisheni za kikristo zipo katika kila mikoa na majimbo, na hakika nyakati hizi hakuna ambaye anayeweza kujitetea kwa kusema kwamba, hajasikia habari za Yesu Kristo.Kwenye kikao cha Afrika ya kusini watumishi wa Mungu walikubaliana kwamba baada tu ya Krismasi ya mwaka 2000, wote wangekusanyika pale Yerusalemu ili kwenda kutoa ripoti kwa Bwana Yesu kwamba kazi aliowatuma ya kuhubiri injili ulimwenguni kote wameimaliza, na mkutano huo ulipewa jila la Jesus celebration.
  Kwa upande mwingine, ningeweza kusema kwamba, sasa ulimwengu wote umesikia habari za Yesu, na watumishi wa Mungu wanazidi kukaza mwendo kuhubiri Injili kwa nguvu zaidi. Ni kweli kabisa hakuna mtu aijuaye siku wala saa ya kurudi kwa Yesu Kristo; lakini yote haya ni mawingu, ambayo ni dalili ya Mvua! Maana yake ni kwamba tupo ukingoni kabisa na wakati wowote ule mwisho wa dunia unakuja! Hivyo jiandae kulia kama bado mpaka leo unamkataa Yesu. Kadhalika na kwa wewe uliyempokea Yesu na kuishi maisha matakatifu jiandae kucheka maana yeye ajaye atakuja wala hatakawia (Waebrania 10:37).

KUONGEZEKA KWA KASI YA UTENDAKAZI WA SHETANI DUNIANI.
    Bwana Yesu alituonya kuwa,”Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu” (Ufunuo 12:12). Shetani, ambaye ana muda mfupi sana wa kutawala na kuwalaghai watu, kwa hiyo, nyakati hizi anatenda kazi kwa kasi isiyo ya kawaida, ili tu kutekeleza uharibifu wake kwa kile ambacho Mungu amekiumba. Maasi na uharibifu mkubwa unaofanywa duniani, ni miongoni mwa mipango wa shetani katika kutimiza unabii wa nyakati za mwisho. Siku hizi utaona kuwa, kila mahali, na wakati wote, kuna utendaji mkubwa sana wa kazi za shetani. Yafuatayo ni baadhi tu ya mambo ambayo ni utendaji kazi wa shetani;

1. KUKITHILI KWA NGONO DUNIANI.
  Nguvu ya ngono ni moja ya silaha kubwa sana ambayo shetani anaitumia kumteka na kumtawala mtu kimawazo, kimaneno na kimatendo. Katika nyakati hizi za mwisho, nguvu za giza hushambulia sana katika eneo hili la tamaa ya mwili. Kumefanyika mikakati na mipango, katika ulimwengu wa roho yaani ulimwengu wa mapepo, ili kuwafanya wanadamu wote wapende sana ngono. Roho chafu za ngono, zimemwagwa kwa wingi duniani ili kuwafanya wanadamu wakati wote watafakari ngono mchana na usiku. Kwa kuliboresha hili, shetani amefanikiwa kuharibu ndoa nyingi duniani ili awaweke wanandoa katika himaya ya uzinzi, akijua hakuna mzinzi atakayeurithi ufalme wa Mungu. Katika kitabu chake Iyke Nathan kinachoitwa “Mkuu wa wachawi sasa ampokea Kristo” ukurasa wa 25, kinasema kwamba mwaka 1986 mwezi wa saba, walitumwa viumbe 30,000,000 (Milioni thelathini) kutoka chini ya bahari kuja duniani wakiwa na maumbo ya wasichana wazuri sana, na walianza kufanya kazi kama Malaya katika miji mbalimbali maarufu ya mataifa hapa duniani, wasichana hao kimsingi ni mapepo, waliletwa duniani kuongeza idadi ya wenzao ambayo kazi yao ilikuwa inaisha mwaka 1997 mwezi wa saba. Lengo la viumbe hao kuja duniani ni kuongeza nguvu ya zinaa.

2. KUKITHILI KWA UCHAWI DUNIANI.
  Moja ya taaluma iliyo juu sana hapa ulimwenguni ambayo shetani anaitumia sana katika kuwapoteza watu ni taaluma ya uchawi.Wapo wachungaji na manabii wengi katika kanisa la leo wanaojihusisha na uchawi ili kuwa na kundi kubwa katika makanisa wanayoyachunga.Kwa ujumla kuna aina nyingi sana za uchawi na ushirikina ambao watu wengi wamebobea ili kuweza kutekeleza utumishi na utii wao kwa shetani.
  Ukweli ni kwamba uharibifu mkubwa duniani unafanywa kupitia uchawi. Matukio mbalimbali ya kinyama na ya kutisha yanafanywa hapa duniani kwa kutumia uchawi. Yote haya ni mipango ya shetani ya kufanya uhalifu ili kutimiza unabii, hususani katika nyakati hizi za mwisho; Mfano wa matukio yanayotokana na uchawi ni:-
1        Ajali mbalimbali za ndege, meli, treni, magari nk.
2        Uharibifu wa mimba kwa wanawake.
3        Magonjwa ya kutisha na yasiyopona.
4        Vifo vya watu wengi, hasa vifo vya kutatanisha.
5        Mafarakano ya ndoa.
6        Kupotea kwa watu ghafla kwa njia ya uchawi.
7        Kuwapumbaza wateule wasisimame kwenye wokovu.
8        Kuleta hali ngumu ya kimaisha kwa watoto wa Mungu ili wakate tamaa.
9        Kupunguza kasi ya kuoa na kuolewa ili kuchochea uasherati makanisani.
10    Kuwapumbaza watumishi wa Mungu wasiwe na macho ya rohoni.
11    Kuwafanya watoto wa Mungu kuipenda dunia, hivyo kuwa kama makahaba.
12    Kuwafanya watumishi wa Mungu kupenda fedha hivyo kushindwa kukemea maovu ndani ya kanisa, hatimaye kanisa kupoteza nguvu ya Mungu.
13 Kuwafanya watoto wa Mungu waichukie kweli ya neno la Mungu na kupenda uongo.
14 Kuwafanya wateule wawe mateka wa nguvu za giza na hatimaye kuondoa nguvu za
     mungu kanisani.
    Kwa ujumla, Lengo kuu la jitihada na mikakati yote hii inayofanywa na shetani, ni kuhakikisha kuwa nyakati hizi za mwisho anapeleka wengi sana Jehanamu ya moto, hususani wateule wa Mungu.

TUKIO LA KUTISHA LINALOKUJA HIVI KARIBUNI.
   Watu wengi sana, wamekuwa wakijiuliza, kuwa mwisho wa dunia utakuwaje? Na kwa kukosa ufahamu wa kweli, baadhi ya watu kupitia madhehebu yao, wamekuwa wakijitungia hadithi za uongo juu ya mwisho wa dunia utakavyokuwa (2 Petro1:16; 2 Timotheo 4:4; 1 Timotheo 1:4).
   Kuna mfululizo wa matukio kadhaa ya mwisho wa dunia, lakini kabla ya kuangalia mfululizo wa matukio hayo, kuna tukio zito, na la kutisha, ambalo litatokea ulimwenguni wakati wowote kuanzia sasa. Na hii ni kutokana na dalili ya mwisho kabisa ya mwisho wa dunia kutimia, kama tulivyo kwisha kuona katika sura iliyopita. Tukio hili linaitwa “Kunyakuliwa kwa watu waliookoka” yaanikanisa. Katika 1 Wathesolanike 4:15-17 Biblia inasema, “Kwa kuwa twawambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakao salia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya Malaika mkuu, na parapanda ya Mungu nao walio kufa katika Kristo, watafufuliwa kwanza kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki bwana hewani na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.”
   ‘Kunyakuliwa’ ni tendo la kuchukuliwa kwa kitu ghafla, kwa kasi kubwa na kuondolewa pale kilipokuwa; katika hali ya kuwaacha watu wamepigwa butwaa, kwa jinsi wasivyoweza kukipata kitu hicho tena. Kwa hiyo, watu waliookoka muda si mrefu ujao, watanyakuliwa kwa jinsi hii na Bwana Yesu Kristo. Yesu anakuja kufanya kazi hii, haraka na wala hatokawia (Waebrania 10:37).
   Siku ya kunyakuliwa kwa watu waliookoka sehemu nyingine duniani itakuwa usiku, sehemu nyingine itakuwa mchana, maana majira duniani yanatofautiana. Jua likitua sehemu moja duniani, linachomoza sehemu nyingine ya dunia. Wakati wa kunyakuliwa kwa watu waliookoka hapa Tanzania, hatufahamu itakuwa mchana au usiku, maana siku ile inakuja kama mwizi au kama uchungu umjiavyo mwenye mimba (1 Wathesolanike 5:1-3). Ikiwa ni mchana watu wote waliokufa tangu zamani wakiwa katika hali ya utakatifu na wakawa wamekwenda mbinguni, watafufuliwa na kutokea tena duniani, na kila mmoja atawaona. Watakuwepo watu wengi kwa ghafla, mitaani kila mahali. Hata kama kwenye makaburi ya zamani ambapo siku hizi kuna jengo la ofisi, watatokea humo humo ofisini na kuujaza uso wa dunia. Dakika moja kufumba na kufumbua, watu waliookoka ambao wako hai duniani nao wataungana pamoja nao, na wote kwa pamoja watabadilishwa miili yao na kuvaa miili ya utukufu yaani miili isiyoharibika. Kadhalika katika kitabu cha 1 Wakorintho 15:52-53 Bibilia inasema,” Kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda Italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa.
   Katika wale watakaokuwako duniani, baada tu ya parapanda kulia, wale waliookoka watatwaliwa na kwenda angani kwenye harusi ya mwana kondoo ambayo, itafanyika kwa muda wa miaka saba, na wale watakaoachwa duniani, watakuwa katika mateso ya dhiki kuu muda wa miaka saba. Kadhalika na watakatifu waliofufuliwa, watakwenda angani kwenye harusi ya mwanakondoo, wakati wale waliokufa katika hali ya dhambi wataendelea kubaki kwenye mateso ya Jehanamu ya moto mpaka wakati wa ufufuo wa pili.

RIPOTI YA KUTOWEKA KWA WATU DUNIANI.
  Tukio la unyakuo, litawachanganya akili watu wote duniani yaani wale watakaobaki. Watakuwepo wawili wakilima shambani, mmoja aliyeokoka atanyakuliwa, naye yule ambaye hajaokoka ataachwa, na hakika atashtushwa sana kwa kitendo cha ghafla cha kutoweka kwa mwenzake. Pia watakuwepo wawili wakitwanga nafaka, na ghafla mmoja aliyeookoka atanyakuliwa na wa pili ambaye hajaokoka ataachwa. Tunasoma katika Mathayo 24:40-41 Biblia inasema “Wakati ule watu wawili watakuwa kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa; wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa; mmoja aachwa.”
   Ikiwa tukio hili litakuwa usiku na katika familia fulani kuna mume hajaokoka na mke ameokoka, watoto wakubwa hawajaokoka na kadhalika katika familia hiyo wako watoto wadogo wasiojua mema na mabaya; mume huyo mlevi amayempiga vita mkewe kwa sababu ya wokovu, ataamka asubuhi na kushangaa kuona mkewe kitandani na watoto wadogo wasiojua mema na mabaya hawapo. Atawauliza watoto wakubwa, “Mama yenu yuko wapi?” watajibu “Hatujui”, atatoka nje na kwenda kuuliza. Wakati kuohuo kila mahali itaripotiwa Polisi, kwamba wako watu waliotoweka usiku, pamoja na watoto wote wadogo wasiojua mema na mabaya. Pia kutakuwepo na Polisi waliotwaliwa. Baada ya uchunguzi duniani kote, waandishi wa habari ambao walioachwa watatoa ripoti katika magazeti kama ifuatavyo, “Mamilioni ya watu kote duniani wameripotiwa kutoweka usiku wa jana. Uchunguzi umeonyesha kwamba waliotoweka ni walokole ambao wamekuwa wakidhaniwa kuwa wamechanganyikiwa au kupotea. Taarifa zaidi zinaeleza kwamba watoto wachanga wote pia wametoweka. Taarifa za uchunguzi zinaonyesha kwamba waliotoweka wamenyakuliwa kwenda kumlaki Yesu mawinguni kama walokole walivyokuwa wakihubiri!

JINSI UNYAKUO WA WALOKOLE (KANISA) UTAKAVYOKUWA.
    Hawa watakaotwaliwa, wataungana na wale waliofufuliwa na kisha wote kwa pamoja, watavutwa kama sumaku inavyovuta chuma, na mvuto huu utatoka kwa Yesu mwenyewe atakayekuwa mawinguni. Yeye hataonekana kwa wale watakao kuwapo duniani, na kwa kuwa Yesu ni mtakatifu kadhalika watakaovutwa ni watakatifu tu, na siyo wenye dhambi. Sumaku itawavuta waliookoka tu, kama jinsi sumaku inavyovuta vyuma peke yake na kuacha mchanga au udongo! Na ndiyo maana Bwana Yesu anatusisitiza katika Mathayo 5:48 kwamba tuwe wakamilifu kama Baba yetu alivyo mkamilifu. Itakuwa kama kuku na ndege wanaposhtushwa na kishindo, ingawa wote wana mabawa, lakini ndege hupaa juu angani na kuku akijaribu kupaa juu huishia kwenye kichanja cha kuanikia vyombo!.
   Nguvu ya kiungu kutoka kwa Yesu akiwa mawinguni itawafanya waliookoka kisawasawa kuishinda nguvu ya uvutano ya dunia (Gravitational force) hivyo watapaa kama tai kwenda kumlaki Bwana Yesu mawinguni huku wakiimba wimbo wa Musa na wimbo wa Mwana kondoo (Ufunuo 15:3-4), huo ndiyo utakuwa mwisho wa huzuni na mateso kwa watakatifu watakaokuwapo hapa duniani.
   Baada ya wenye dhambi kuachwa, ndipo kitakapokuwapo kilio na kusaga meno hapa duniani. Itafuata dhiki kubwa ya miaka saba; ambayo namna yake haijawahi kutokea tangia misingi ya dunia kuwekwa. Biblia inasema katika Mathayo 24:21, “Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe.”
  Wenye dhambi watateswa kwa namna ya kutisha. Watu watatamani kufa kutokana na mateso na maumivu, lakini mauti ya namna hiyo itakuwa imeondolewa (Ufunuo 9:2-6). Wataiambia milima na miamba, tuangukieni, watamwomba Mungu awahurumie, lakini huruma na uvumilivu wake Mungu utakuwa umekoma (Ufunuo 6:15-17Isaya 26:16-18). Wale walionyakuliwa, huko juu watakuwa katika karamu ya arusi ya Mwanakondoo baada ya kupewa kila mtu taji zake (Ufunuo 19:5-9; 2Wakorintho 5:8-10).

MIFANO YA KIBLIA KAMA KIVULI CHA KUNYAKULIWA KWA
WALIOOKOKA (KANISA).
  Mungu katika hekima yake iliyo juu sana, hakuacha kutupa mifano ya yale yatakayotokea mbeleni ili tuyaelewe vema kabla ya dhiki kuu, mifano ifuatayo inatupa picha halisi ya unyakuo itakavyokuwa;
1.Nuhu na wanawe saba, walikwenda safinani kwanza, kabla ya Mungu kuleta gharika juu ya wenye dhambi, na wakati wote safina ilikuwa juu, gharika chini (Mwanzo 7:11-18).
2.Lutu alishikwa mkono na kutolewa nje ya mji wa Sodoma na Gomora kabla Bwana kuleta uhalibifu juu ya nchi (Mwanzo 19:12-16, Mwanzo 19:23-24).
3.Kabla ya Bwana, kuwaangamiza wana wa Kora, alihitaji kuona Musa na Haruni na wengine wasiokuwa waasi wametengwa mbali nao (Hesabu 16:20-21, 16:23-27, 16:31-35).
4.Kama Henoko na Eliya walivyotwaliwa na kwenda mbinguni bila kufa, ndivyo watakatifu, walio hai, waliosalia watakavyotwaliwa bila kufa (Mwanzo 5:24, 2 Wafalme 2:11-12).
5.Kama Bwana Yesu alivyopaa kwenda mbinguni ndivyo watakatifu nao watakavyoondoka kwa jinsi hiyo (Marko 16:19, Luka 24:50).

   Yapo baadhi ya madhehebu, ambayo yanawapotosha watu na kuwafundisha uongo, kwamba watu wote watakuwepo kwenye dhiki kuu, hivyo unyakuo utafanyika baada ya dhiki kuu. Huu ni uongo ulio wazi, kwani asiye na hatia kamwe hawezi kuingizwa kwenye adhabu (Ufunuo 3:10Luka 21:22-23, Luka 21:34-36, 1 Wathesolanike 1:10). Hata katika mazingira yetu ya kawaida hapa duniani, mara zote mwenye hatia anapopewa adhabu anatengwa na mwenye haki, na ndiyo maana zikawekwa mahabusu (Selo). Ili uweze kulielewa hili kwa mapana na marefu, ni vizuri ukijua kusudi la Mungu la kuileta dhiki kuu. Hebu sasa fuatana nami katika sura ifuatayo ili uweze kupata mwanga zaidi.

SIFA ZA WALE WATAKAONYAKULIWA.
Wale watakaonyakuliwa ni lazima wawe na sifa zifuatazo:-
1.      Ni wale tu walioziungama dhambi zao na kuziacha ndiyo watakaopata rehema ya kunyakuliwa, bali wale wazifichao dhambi zao hawatafanikiwa (Mithali 28:13)
2.      Ni wale tu waliomfanya Yesu kuwa Bwana yaani mtawala wa maisha yao yote, na kulitii kila neno analoliagiza katika maandiko matakatifu, bila kuchagua ya kufanya
 (Zaburi 119:6; Luka 6:46; Kumb 1:35-36).
3.      Ni wale tu waliookoka na kuishi katika utakatifu mpaka mwisho, bila waa wala kunyanzi wala hila (Waefeso 5:27; Waebrania 12:14; 1 Yohana 3:2-3).

Jiweke tayari kuonana na Mungu (Amosi 4:12).

DHIKI KUBWA.
   Baada ya kunyakuliwa kwa kanisa (watu waliookoka) Dhiki kubwa, itafunika dunia nzima. Wote walioachwa watakuwa katika kipindi hiki kizito sana cha dhiki kuu. Hii itakuwa ni pamoja na wale wote ambao hawakukubali kuacha dhambi na kuokolewa, pamoja na wale wote waliokuwa wameookoka, lakini maisha yao yalikuwa vuguvugu, yaani kwa Yesu kidogo,kwa shetani kidogo, utii kidogo na uasi kidogo. Ni muhimu sana kujifunza kwa undani zaidi juu ya kipindi hiki cha hatari sana, ili tuweze kujihadhari na kuhakikisha hatuwi miongoni mwa watu watakaoachwa katika unyakuo.

MAANA NA MAJINA MBALIMBALI YANAYOTUMIKA
KUIZUNGUMZIA DHIKI KUU.
   Dhiki kuu ni Uangamivu, taabu, ghadhabu, pigo au hukumu ya adhabu ambayo itaachiliwa kwa wote ambao hawakumkubali Yesu (Wokovu). Dhiki hii itakuwa kwa muda wa juma moja la Danieli, (juma la sabini) – Danieli 9:24-27. Katika unabii wa Danieli, juma moja humaanisha miaka saba (Mwanzo 29:27). Nusu juma hili, ni nusu ya miaka saba yaani miaka 3½ au miezi 42, au siku 1,260. Miaka mitatu na nusu ya mwisho ya kipindi hiki, itakuwa ya kutisha sana kwa Waisraeli baada ya mpinga Kristo kuvunja agano nao (Ufunuo 11: 2-3; Ufunuo 12:6; Ufunuo13:5). Katika kuleta uzito na utisho wa dhiki hii, Dhiki kuu imepewa majina mbalimbali ya kutisha kama ilivyo:-
a)      Ghadhabu itakayokuja (1 Wathesolanike 1:10).
b)      Saa ya hukumu (Ufunuo 14:7).
c)      Adhabu ya ghadhabu (Isaya 24:21; Isaya 26:21).
d)     Saa ya kujaribiwa (Ufunuo 3:10).
e)      Taabu yake Yakobo (Yeremia 30:7).
f)       Uangamivu (Yoeli 1:15).
g)      Siku ya giza na weusi, siku ya mawingu na giza kuu (Yoeli 2:1-12).
h)      Siku ya uharibifu, fadhaa, dhiki, giza, utusitusi, (Sefania 1:15).

MAKUSUDI YA DHIKI KUBWA.
   Kuna makusudi makuu mawili yanayompelekea Mungu kuileta dhiki kuu;
i.           Kuleta hukumu ya adhabu juu ya wote ambao hawakubali wokovu
        (Isaya 26:20- 21, 2 Wathesolanike 2:7-12).
ii.         Kuliandaa Taifa la Israeli kumpokea Yesu kama Masihi wao
         (Kumbukumbu 4:30-31; Yeremia 30:7, Ezekieli 20:37-39; Warumi 11:25-27).

DHIKI KUU TOFAUTI NA DHIKI ZOTE.
            Wanadamu wanapita katika dhiki nyingi sana duniani. Tangu zamani, vizazi hadi vizazi, kumekuwa na shida, taabu,dhiki na mateso mazito kwa wanadamu. Mfano watu waliompokea Yesu, wanapata dhiki na mateso kwa sababu ya wokovu wao. Dhiki hizi kwa mtu aliyempokea Yesu inaweza ikawa kupigwa na mume, au kuachwa na mume, kukataliwa na wazazi, kunyimwa fedha za matumizi na wazazi, au hata kutengwa na wazazi, au jamii kuyumba kiuchumi nk. Yesu Kristo alijua kwamba mtu aliyeookoka atapata dhiki, na akasema,” Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo” (Yohana 16:33). Pia maandiko yanasema tumepewa sio kumwamini Yesu tu ila kuteswa kwa ajili yake (Wafilipi 1:29). Hata hivyo, pamoja na dhiki hizi ambazo watu wanakumbana nazo, lakini zote hizi tunaziita ni “dhiki nyepesi” ukilinganisha na dhiki kubwa. Katika kitabu cha 2 Wakorintho 4:17 Biblia inasema, “Maana dhiki yetu ni nyepesi iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana.” Sasa basi dhiki kubwa itakuwa haina mfano wake tangu kuumbwa ulimwengu. Mathayo 24:21, Biblia inasema, “Kwa kuwa wakati huo kutakuwepo dhiki kubwa ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwepo kamwe.” Pia katika kitabu cha Danieli 12:1 Biblia inasema, “ Wakati huo mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako; na kutakuwa na taabu, mfano wake hautakuwepo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo; na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile.

WATAKAO HUSIKA KUILETA DHIKI KUBWA.
         Kama tulivyo kwisha kuona katika maandiko mbalimbali katika Biblia, kwamba dhiki hii itakuwa kubwa mfano wake hakuna, kutokana na nguvu tatu zitakazohusika kuileta dhiki hii kwa wanadamu; yaani Mungu, shetani na Mpinga Kristo.

(i) Mungu.
       Nguvu ya kwanza, itakayohusika kikamilifu kuleta ghadhabu na mapigo juu ya wote walioachwa ni Mungu mwenyewe. Katika kitabu cha Isaya 26:21 Biblia inasema, “Kwa maana tazama Bwana anakuja kutoka mahali pake, ili kuwaadhibu wakaao duniani, kwa sababu ya uovu wao; ardhi nayo itafunua damu yake, wala haitawafunika tena watu wake waliouawa.” Pia katika kitabu cha Sefania 1:17-18 Biblia inasema, “ Nami nitawaletea wanadamu dhiki, hata watakwenda kama vipofu sababu wamemtenda Bwana dhambi; na damu yao itamwagwa kama mavumbi,na nyama yao kama mavi. Fedha yao wa dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku ile ya ghadhabu ya Bwana.” Kadhalika katika kitabu cha Yoeli 1:15 Biblia inasema, “Ole wake siku hii! Kwa maana siku ya Bwana inakaribia, nayo itakuja kama uangamivu utokao kwake aliye mwenyezi.” Soma pia katika (Ufunuo 14:7, Ufunuo15:7).

(ii) Shetani.
  Nguvu ya pili, itatoka kwa shetani.Shetani atawashukia watu walioachwa kwa ghadhabu nyingi huku akijua ni wakati wake wa mwisho. Katika kitabu chaUfunuo 12:12 Biblia inasema, “Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua kuwa ana wakati mchache.”

            (iii)  Mpinga Kristo.
         Nguvu ya tatu, itakayochangia kuileta dhiki kuu ni Mpinga Kristo (Yohana 2:8)ambaye anajulikana pia kwa majina ya Mpingamizi, Asi, chukizo la uharibifu au mnyama, katika kitabu cha Mathayo 24:15 Biblia inasema, “Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (Asomaye na afahamu).” Pia katika kitabu cha 2 Wathesolanike 2:3-4 Biblia inasema, “Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yoyote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengefu; akafunuliwe yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu. Yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kile kiitwacho mungu ama kuabudiwa, hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akajionyesha nafsi kama kwamba yeye ndiye Mungu.” Katika Ufunuo 13:1-6 tunaona juu ya Mnyama atokaye katika bahari. Bahari katika Lugha ya kinabii inawakilishwa na watu, au mkutano mkubwa wa watu; katika kitabu chaIsaya 17:12 Biblia inasema, “Aha! Uvumi wa watu wengi! Wanavuma kama uvumi wa bahari; Aha!  Ngurumo ya mataifa! Wananguruma kama ngurumo ya maji mengi.” Pia katika kitabu cha Ufunuo 17: 12 Biblia inasema,” Kisha akaniambia, yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha.” Hivyo basi mnyama anayetoka katika bahari ni mtu au mwanadamu halisi. Katika kitabu chaUfunuo 13:18 Biblia inasema, “Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili na aihesabu hesabu ya Mnyama huyo maana ni hesabu ya kibinadamu na hesabu yake ni mia sita sitini na sita” Mtu huyu au mnyama atakuwa amepewa uwezo na shetani mwenyewe na atafanya yote chini ya usimamizi wake kama inavyoelezwa katika Ufunuo 13:4 Biblia inasema,”Wakamsujudu Yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo; nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye?” Na katika Mnyama huyo, imezungumziwa, vichwa, pembe na vilemba; hizi ni alama za nguvu na utawala wake utakao kuwa dunia nzima (Ufunuo 17:3, Ufunuo 17:9-13). Kutokana na ishara zake na mateso yake atawafanya watu wengi walioachwa kumwabudu shetani au sivyo kuuawa (Ufunuo 13:13-17) Ili litimie Neno la Yesu Kristo Katika Yohana 5:43, “Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, wala ninyi hamnipokei; Mwingine akija kwa jina lake mwenyewe mtampokea huyo.”

JE PAPA NDIYE MPINGA KRISTO KAMA WASEMAVYO
WAADVENTISTA WASABATO?
   Ni wazi kabisa jibu ni kwamba, Papa wa kanisa Katoliki siye mpinga Kristo (Mnyama) kama yanavyosema mafundisho ya unabii ya Waadventista wasabato. Nina ujasiri kusema kuwa, aliyetoa tafsiri ya unabii huu, hakuwa na ufahamu mpana wa maandiko matakatifu katika kuutafuta ukweli huu, na ni dhahiri alitumia macho ya damu na nyama na siyo macho ya rohoni.
          Ni vizuri kufahamu kwamba, Mungu anapotupa unabii katika maandiko matakatifu, na akamzungumzia mtu fulani atakaye timiza unabii huo, mara zote Mungu huwa hamweki wazi mtu huyo mpaka wakati wa kutimia unabii huo utakapofika. Mfano, Yuda Iskariote aliyemsaliti Yesu, Alizungumziwa miaka mingi iliyopita kabla ya Yesu kuja duniani katika Zaburi 41:9 kwamba, “Msiri wangu tena niliyemtumaini, aliyekula chakula changu, ameniinulia kisigino chake” Pamoja na unabii huu kutolewa muda mrefu uliopita juu ya atakayemsaliti Yesu lakini bado Yuda Iskariote hakuwekwa wazi mpaka ilipofika wakati wenyewe, nikiwa na maana kwamba hata wanafunzi wenzake kumi na moja hawakumjua kama yeye ndiye msaliti, mpaka Bwana Yesu alipomdhihirisha. Pia kuna mtu tajiri alitabiriwa katika Isaya 53:9 kuwa atamzika Yesu, mtu huyu au tajiri huyu hakujulikana mpaka wakati ulipotimia ndipo tukajua ni Yusuph wa Arimathaya (Mathayo 27:57-60). Kadhalika katika Isaya 40:3 Alizungumziwa “sauti ya mtu aliye nyikani” yaani Yohana mbatizaji mwana wa Zakaria. Lakini haikujulikana kama “Sauti ya mtu aliaye nyikani”, angekuja kuwa ni Yohana, mpaka wakati ulipofika ndipo Mungu aliliweka wazi. Mara zote, unabii wa Mungu unakuwa na siri kubwa sana mpaka wakati unapofika ndipo mtu au muhusika anafunuliwa. Tunajua kuwa Mungu wetu si Mungu wa machafuko, hivyo muhusika anapokuwa wazi mapema, usalama unakuwa mdogo sana.
  Sasa, ebu jaribu kuwaza na kujiuliza juu ya mafundisho ya waadventista wasabato kudai kwamba Papa wa kanisa Katoliki ndiye mpinga Kristo, Je mahusiano ya waumini wa pande hizi mbili yaani Wakatoliki na Waadventista yanakuwaje? Je ni kweli ufunuo wa Kimungu unaleta uhasama? Mungu wetu hatoi unabii ili kugombanisha watu bali kutimiza neno lake na kwa wakati wake.


JE NI MWANADAMU GANI ATAKAYEKUWA MPINGA KRISTO?
  Ukweli ni kwamba, mpaka sasa hakuna anayejua kuwa mpinga Kristo atakuwa nani, isipokuwa ni Mungu peke yake ndiye anayejua. Katika kitabu cha Ufunuo 13:18 Biblia inasema, “Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili na aihesabu hesabu ya mnyama huyo, maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni 666.” Unabii unaonyesha kuwa mpinga Kristo, atakuwa ni mwanadamu, lakini atapewa uwezo wa kufanya mambo ya kutisha na shetani na atatumia nembo ya namba 666, sasa ni mwanadamu yupi basi? Hilo analijua Mungu peke yake, na atakuja kumweka wazi wakati ukifika, kwani ni uwezo wa Mungu kuamua ni unabii upi utimie wakati gani na ni nani atakayetimiza unabii huo.
  Ni vizuri kufahamu kwamba katika kuihesabu hesabu ya mnyama huyu, inahitaji hekima na akili. Hekima na akili inayozungumziwa hapa si ya kidunia, bali ni ufahamu mpana katika ulimwengu wa Roho. Wala si swala la kufikiria na kumshuku mtu fulani. Ningependa nikuweke wazi mpenzi msomaji wa kitabu hiki kuwa alama au nembo ya 666 inatumika katika ulimwengu wa nguvu za giza. Tukirejea katika kitabu cha Mkuu wa wachawi sasa ampokea Kristo cha Iyke Nathan, kinazungumzia juu ya ngazi za juu za utenda kazi wa nguvu za giza. Shetani hufanya kazi na makundi 400,000 ya roho za giza kwa kushirikiana. Makundi hayo yamejigawa katika ngazi tano na kila ngazi hujulikana kwa nembo yenye namba. Ngazi hizo ni kama ifuatavyo:-
i.        Ngazi ya 333.
ii.      Ngazi ya 666.
iii.    Ngazi ya 999 (liber 007 sagna seal-liber 777).
iv.    Ngazi ya 1330 (Bavara seal).
v.      Ngazi ya 003(Liber 003-Tuzassotama seal).
   Kwa upande wangu, ningependa kuizungumzia ngazi ya kichawi ya pili yaani ngani ya 666. Mwanadamu yeyote anayefikia ngazi hii ya juu ya kichawi ni lazima awe amepitia mafunzo mazito sana ya nguvu za giza. Ngazi hii yenye nembo 666 inahitaji digrii za kichawi 30,000 ili kuifikia. Anayekuwa amepata nembo hiyo anakuwa na cheo cha kuweza kutawala roho chafu 160,000 ambazo hufanya kazi chini yake na kwa mamlaka na amri yake. Hii inakuwa tayari ni ngazi ya Mpinga kristo. Watu wenye ngazi hiyo wamesababisha maafa makubwa ya kihistoria hapa duniani. Mifano ya watu waliofikia ngazi hii ya kichawi hapa duniani ni kamaAdolf Hitler ambaye alikuwa mtawala wa kiimra (kidikteta) nchini Ujerumani miaka ya nyuma. Pia mwanasayansi mkubwa aliyejulikana sana duniani aliye tangaza kuwa hakuna Mungu mwaka 1859 ambaye ni Charles Darwin. Kadhalika Idd Amini aliyekuwa Rais wa Uganda na wengine wengi. Hawa wote ndiyo waliofikia ngazi hii ya pili ya kichawi yenye nembo 666, na waliweza kufanya mambo yote ya kutisha wakiwezeshwa na roho chafu 160,000. Watu wengi wenye majina makubwa kama wanasiasa, wakuu wa majeshi, wakuu wa dini mbalimbali na watu wazito wengi hapa duniani, waliopo katika mtandao wa nguvu za giza, ndiyo wanaopewa cheo hiki cha pili na shetani. Kwahiyo, Mpinga Kristo atakuwa ni miongoni mwa wanadamu walio na majina makubwa hapa duniani, na ni mshiriki katika ufalme wa giza akiwa na ngazi ya pili ya kichawi yenye nembo ya 666. kwa vile, aliye na ngazi hii humiliki roho chafu 160,000 tu kumuwezesha kutenda kazi, hivyo shetani atamuongezea nguvu zaidi, yaani roho chafu nyingine, ili aweze kufanya mambo ya ajabu na ya kutisha katika kipindi cha dhiki kuu. Mpiga Kristo atakuwa mtu hatari sana mara nyingi zaidi ya Adolf Hitler au Idd Amini. Na siri kuu iliyopo kwa wenye ngazi ya pili ya kichawi yenye nembo ya 666, huwa wanapinga sana uwepo wa Taifa teule la Mungu yaani Waisraeli, kama ilivyokuwa kwa Adolf Hitler na Idd amini, kwani 666 ni nembo ya Mpinga Kristo, na Kristo anatokea taifa  la Waisraeli. Hivyo kwa kuwapinga wana wa Israeli tayari wanampinga Kristo.

HALI HALISI ITAKAVYOKUWA WAKATI WA DHIKI KUBWA.
   Wakati wa dhiki kubwa kutakuwa na mateso na dhiki yasiyoelezeka. Itakuwa ni kilio na kusaga meno kwa wale walioachwa. Watu watapata mateso makali kwa muda mrefu na hatimaye watauawa, na damu yao itamwangwa kama mavumbi na nyama zao kama mavi, wala hatakuwepo watu wa kuwalilia wala kuwazika (Sefania 1:15-18; Yeremia 25:33). Hasira ya Mungu iliyojiwekea akiba itafunuliwa wakati wa dhiki kubwa ( Sefania 2:1-3). Watu wataiambia milima iwaangukie iwasitiri, haitafanya hivyo (Ufunuo 6:15-17). Watu watakuwa katika maumivu mchana na usiku wakinywea kikombe cha mvinyo ya kadhabu ya Mungu isiyochanganya na maji (Ufunuo 14:9-11). Watu watatamani kujiua, lakini mauti ya namna hiyo haitakuwepo, mpaka wateswe na kuuawa (Ufunuo 9:2-6). Mapigo ya Mungu yatatimizwa kwa kumwangwa kwa mapingo saba ya kutisha juu ya wanadamu (Ufunuo 15:1; Ufunuo 16:1-21). Kutokana na taabu watakayopata, wanadamu watamwomba Mungu hili awahurumie, lakini huruma ya Bwana itakuwa imekoma (Isaya 26:16-18). Wachungaji, mitume, manabii, waalimu na wainjilisti ambao hawakukubali kuishi katika wokovu, na wanaowapoteza watu, watakuwepo wenye mateso hayo (Isaya 24:1-6). Hakika itakuwa dhiki kubwa sana (Isaya 24:17-18). Katika miaka 31/ya mwanzo kutakuwa na nafuu kidogo kwa Taifa la Israeli kutokana na Angano la uongo ambalo mpiga Kristo atakuwa amelifanya na Israeli. Miaka 31/iliyosalia chukizo la uharibifu litasimama kikamilifu juu ya taifa la Israeli (Danieli 9:27). Kimsingi dhiki kuu inakuwa kama kujiokoa kwa damu yako mwenyewe, kwasababu ya kukataa kuokolewa kwa damu ya Yesu.
  Ghadhabu juu ya Israeli itakuwa kubwa sana kiasi cha kuwafanya Waisraeli wakimbie nchi yao (Mathayo 24:15-16). Kwa ajili ya wateule, siku za dhiki kubwa zitafupishwa (Mathayo 24:21-22). Wateule wanaotajwa hapa siyo sisi tuliokoka Leo. Neno “mteule” au “wateule” linatumika katika Biblia kwa maana nne tofauti,
(a)    Yesu Kristo (Isaya 42:1)
(b)   Malaika watiifu (1Timotheo 5:21)
(c)    Sisi tuliookoka (Tito 1:1; 1Petro 1:1-2, Warumi 8:33, Luka 18:7)
(d)   Taifa la Israeli (Isaya 65:8-9; 45:4) kwa hiyo wateule katika Mathayo 24:21-22, ni taifa la Israeli.
JINSI YA KUIKWEPA DHIKI KUBWA.
   Katika Isaya 26:20 Biblia inasema, “Njoni, watu wangu, ingia wewe ndani ya vyumba vyako ukafunge mlango nyuma yako ujifiche kitambo kidogo mpaka ghadhabu hii itakapopita” Kila anayetaka kuikwepa dhiki hii kubwa inambidi kujificha ndani ya vyumba na kufunga nyumba kama wakati wa Safina ya Nuhu kwa kufanya yafuatayo:-
(i)     Kuhakikisha umetubu dhambi na kuziacha na kuokolewa kwa kumwamini Yesu Kristo. (Mithali 28:13; Yohana 3:36, Ufunuo 13:10, Isaya 33:1)
(ii)   Kukaa ndani yake Yesu kwa kufuata Neno lake na maagizo yake yote kwa gharama yoyote, siyo kukaa ndani ya mapokeo ya wanadamu au ndani ya dhehebu (1Yohana 2:28; Zaburi 119:6,9)
(iii) Kukaa mahali ambapo pana waalimu wenye mafundisho yote ya kweli ili tujue nini mapenzi ya Mungu (Isaya 30:20-21). Kuwa mbali na viongozi wanaofundisha uongo (Isaya 9:14-15).

Mtu akiwa na sikio na asikie (Ufunuo 13:9).

TAJI NA HARUSI YA MWANAKONDOO.
   Katika sura iliyopita, tumeona jinsi watu wenye dhambi watakaoachwa katika mateso na maumivu ya kutisha kwa miaka saba. Sasa basi, katika sura hii tunakwenda kujifunza juu ya yale yatakayoambatana na wale watakaokuwa wamenyakuliwa kwenda kumlaki Bwana Yesu mawinguni.
KUONDOKA KWA SHANGWE KWA WATAKATIFU.
  Wakati wa kunyakuliwa kwa watakatifu hapa duniani kwa muda mfupi sana watafundishwa nyimbo mbili na Mungu mwenyewe, wimbo mmoja unaitwa wimbo wa Musa na mwingine wimbo wa mwanakondoo, katika kitabu chaUfunuo15:3-4 Biblia inasema,”Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu,na wimbo wa mwanakondoowakisemaNi makuu na ya ajabu matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi ni za haki na za kweli, njia zako, Ee mfalme wa mataifa. Ni nani asiyekucha, Ee Bwana, Ee Bwana na kulitukuza jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako umtakatifu; Kwa maana mataifa yote watakuja kusujudu mbele zako; kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha kufunuliwa”. Mungu alimfundisha Musa wimbo na kumwambia awafundishe Waisraeli ili waukumbuke wakati Mungu atakapowaka hasira juu yao na kuwaacha (Kumbukumbu 31:17-19; Kumbukumbu 32). Hiki kilikuwa ni kivuli cha mambo yajayo wakati watakatifu watakapoimba wimbo wa Musa na wa Mwanakondoo na  kuondoka huku nyuma yao hasira ya Mungu ikidhihirika kwa wenye dhambi waliobaki wakati wa dhiki kubwa. Vilevile, Musa na wana wa Israeli baada ya kuwaona wamisri wamekuja na kuteganishwa nao kabisa waliimba wimbo wa Musa wakiwa wanaanza kwenda Kanaani (Kutoka 15:1-20) Watakatifu nao itakuwa hivyohivyo. Wataimba wimbo wa Musa watakapoanza kwenda Kanaani. Siyo hilo tu, Yesu Kristo alikuwa akiimba na wanafunzi wake hivyo alikuwa mwimbaji, katika kitabu cha Marko 14:26 Biblia inasema, “Nao walipokwisha kuimba walitoka kwenda mlima wa mizeituni”. Wimbo huu ndiyo wimbo wa mwanakondoo. Watakatifu watauimba wakiwa wanapaa juu mawinguni baada ya kumshinda shetani na majaribu yake yote.
KITI CHA THAWABU.
   Neno la Mungu yaani Biblia mara zote inazungumzia juu ya kulipwa kwa kazi inayofanywa na watumishi wa Mungu hapa duniani.Biblia inasema tutapewa taji au thawabu (Ruthu 2:12; Zaburi 58:11; Mithali 13:13; Isaya 40:10; Yeremia 31:16; Mathayo 5:12; 1Wakorintho 3:8; 1Wakorintho 9:25; 1Wakorintho 15:58; Waebrania 10:35; 2Yohana 1:8, Yohana 4:35-36). Thawabu au taji hizi atakuja nazo Yesu mwenyewe mawinguni na kila mmoja atalipwa kulingana na utumishi aliomfanyia Mungu katika kipindi chake chote cha wokovu hapa duniani.Taji hizi zitatolewa mawinguni mara tu baada ya kumlaki Yesu (Ufunuo 22:12; 2Timotheo 4:8; Luka 14:12-13). Wakati wa kutoa taji hizi, Bwana Yesu atakalia kiti maalumu kinachoitwa Kiti cha hukumu cha Kristo (2Wakorintho 5:10), kiti hiki kwa kiyunani kinaitwa “Bema”. Ni kiti atakachokalia Yesu na kutoa hukumu kwamba nani apewe thawabu au taji ipi.Kwa upande mwingine tungeweza kukiita “Kiti cha Thawabu au taji.”

KUJARIBIWA KWA KAZI YA KILA MTU.
   Katika mchakato mzima wa kujua nani apewe taji ipi, kazi ya kila mtu aliyeokoka aliyoifanya katika kumtumikia Mungu, itajaribiwa kwa moto ili ipate kufahamika thawabu ipi mtu atakayopata, katika kitabu cha 1Wakorintho 3:10-15 Biblia inasema, “Kwa kadri ya neema ya Mungu, niliyopewa mimi kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima naliuweka msingi na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake. Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa yaani Yesu Kristo, lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huo dhahabu au fedha au mawe ya thamani au miti au majani au manyasi kazi ya kila mtu itakuwa dhahiri, maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto na ule moto wenyewe utaijaribu kazi ya kila mtu ni ya namna gani, kazi ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa atapata thawabu. Kazi ya mtu ikiteketea, atapata hasara ila yeye mwenyewe ataokolewa lakini ni kama kwa moto”. Ikiwa kazi aliyoifanya mtu ni ya thamani sana kama dhahabu, fedha au mawe ya thamani, itakapopitishwa katika moto itazidi kung’aa na wengine wote watashangilia pamoja na malaika. Ikiwa kazi aliyoifanya mtu ilikuwa duni, itakapopitishwa katika moto itateketea kama miti, majani au manyasi na itakuwa ni aibu! Ingawa mtu ataendelea kuwepo mbinguni; atakuwa kama mhalifu msalabani bila kuwa na taji yoyote na daraja yake itakuwa ya chini.

AINA ZA TAJI ZITAKAZOTOLEWA KWA WATAKATIFU.
   Haitafurahisha kabisa kumuona mtu ambaye hakupewa taji yoyote wakati alikuwa na muda wa kumfanyia kazi Mungu tofauti na yule mwizi pale msalabani. Ni wajibu wetu kutamani sana kupata taji zozote zifuatazo tena kwa gharama yoyote katika maisha yetu ya wokovu. Kwa hiyo zifuatazo ndizo taji zitakazotolewa na Yesu Kristo kwa watakatifu katika harusi ya mwanakondoo.
1: Taji isiyoharibika (Incorruptible Crown) (Wakorintho 9:23-25).
  Taji hii watapewa watakatifu ambao walifanya mambo yote kwa ajili ya injili, walijizuia yote katika maombi yao kwa ajili ya injili ili kushiriki pamoja na wengine. Walijizuia yote katika utoaji wao kwa ajili ya injili, walijizuia yote katika maombi yao kwa ajili ya injili na pia walitumia vyote walivyo navyo; muda, ujuzi, vipawa, cheo chao, uwezo wao wote, nguvu zao n.k kuishiriki injili pamoja na wengine.

2: Taji ya kujionea fahari (Crown of Rejoicing)( 1Wathesalonike 2:19, Daniel 12:3).
  Taji hii inaitwa taji ya kujionea fahari kwa sababu watakaopata taji hii watang’ara kama nyota tofauti na wengine watakavyong’ara. Fahari yao itakuwa kubwa kuliko ya wengine. Mng’ao wao wa utukufu utakuwa mkubwa kuliko wengine. Taji hii watapewa wale waliowaleta watu wengi kwa Kristo, kutokana na kushuhudia kwao au kuhubiri injili. Washuhudiaji wale waliozaa watoto wengi katika injili yao ya nyumba kwa nyumba au vinginevyo na wakahakikisha watoto hao wanakuwa kiroho kwa kuwafundisha au kuwaongoza kwa walimu wazuri watakaowafundisha watapewa taji hii.

3: Taji ya uzima (Crown of life) (Ufunuo 2:10).
 Taji hii ni maalum kwa wale waliopita katika majaribu au mitihani mikubwa ya maudhi na kuchukiwa kwa ajili ya Kristo na wakashinda au hata kufa, hawakupenda maisha yao kufa, lakini walifanya hivyo kwa ajili ya Kristo (Yakobo 1:2; Ufunuo 12:11; Mathayo 5:11 – 12 Waebrania 11:24-26; Zaburi 129:2).

4: Taji ya haki (Crow of Righteousness) (2Timotheo 4:6-8).
  Taji hii ni kwa wale waliopenda kufunuliwa kwake Yesu Kristo.Wakati wote walikubali kutii kila neno aliloagiza Bwana Yesu. Walikuwa na utakatifu wakati wote. Kila neno walilojifunza walilitendea kazi, kwao hakukuwa na kurudirudi nyuma na kwenda duniani kwanza, halafu wakaendelea tena na wokovu kidogo.Hivyo Yesu akawakuta katika hali ya utakatifu. Taji hii pia ni kwa wale waliowatendea mema adui zao (Luka 6:34-36).

5: Taji ya utukufu, ile isiyokauka (Crown of Glory) (1Petro 5:2-4).
(a)     Taji hii watapewa wachungaji, waalimu au watumishi wa Mungu wanaojitaabisha kuwafundisha wengine na kuwalea kiroho kwa njia zozote, kuwafundisha kanisani na kuwapa huduma za kichungaji, kuandika vitabu au tracts za mafundisho ya neno la Mungu yanayowasaidia watu wakue kiroho.
(b)    Taji hii pia watapewa wale wanaowahudumia mitume, wachungaji, manabii, wainjilisti na waalimu ili wapate urahisi wa kuzifanya kazi zao(Mathayo 10:41-42).
(c)     Taji hii watapewa wote wanaochukua muda wao wote kuwasaidia watu kukua kiroho kama kuwaazima au kuwanunulia vitabu, CD au kaseti za mafundisho, kuwapa nauli ili waende kanisani, kazi za kuhudumia kanisani n.k.

HARUSI YA MWANAKONDOO.
    Watakatifu walionyakuliwa wanaitwa Bikira safi wa Kristo, katika2Wakorintho 11:2 Biblia inasema, “Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu kwa kuwa naliwaposea mume mmoja ili nimletee Kristo bikira safi”. Lakini pia wanaitwa Bibi harusi wa Kristo, katika Yohana 3:29Biblia inasema, “Aliye naye bibi harusi ndiye bwana harusi lakini rafiki yake Bwana harusi yeye anayesimama na kumsikia alifurahia sana sauti yake bwana harusi.”Hivyo baada ya kupewa taji, Yesu atawafanyia watakatifu karamu ya kuwapongeza. Hii ndiyo karamu ya mwanakondoo (Ufunuo 19:7-9). Hii itafanyika katika kipindi hichohicho cha miaka saba wakati huku duniani wakiwa katika dhiki kuu.

JINSI YA KUSHIRIKI HAYA YOTE.
(i)                 Kuwa miongoni mwa watakatifu (Waebrania 12:14)
(ii)               Kuifanya kazi ya Mungu kwa bidii zote na nguvu zote (Muhubiri 9:10;
Yohana 4:34-36 Warumi 12:11, 1Wakorintho 7:29-35).


Tumeokolewa ili tumtumikie Mungu
(Kutoka 8:1; Kutoka 10:24-26; Kutoka 12:31)


KUJA KWA YESU MARA YA PILI DUNIANI.
   Tukiangalia katika sura zilizopita, kwamba dhiki kubwa au dhiki kuu itachukua kipindi cha miaka saba (07). Katika kipindi hiki pia watakatifu walionyakuliwa watakuwa katika kipindi cha kupewa taji na kufanyiwa karamu ya harusi ya mwanakondoo. Hivyo ni makusudi ya sura hii kujifunza tukio litakalofuata mwisho wa miaka saba. Tukio hili ni kuja kwa Yesu Kristo mara ya pili Duniani.
KUJA KWA YESU MARA YA PILI DUNIANI.
   Yesu Kristo, mara ya kwanza alikuja hapa duniani katika hali ya udhaifu na unyonge kwa kuzaliwa na Mariamu na kulazwa katika holi ya kulia ng’ombe. Kwa Waisraeli ambao hawakujua maandiko vema, hawakutambua kwamba Kristo ndiye Yesu, kutokana na mazingira yake ya umasikini na unyonge, katika kitabu cha Luka 9:58 Biblia inasema, “Yesu akamwambia, mbweha wana pango na ndege wa angani wana viota, lakini mwana wa Adamu hana pa kujilaza kichwa chake.” pia katika kitabu cha 2Wakorintho 8:9 Biblia inasema, “Maana mmejua neema ya bwana wetu Yesu Kristo jinsi alivyokuwa masikini kwa ajili yenu ingawa alikuwa tajiri ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umasikini wake.” Wana wa Israeli walidhani kwamba wakati ule wa kwanza angekuja kama mfalme, kumbe kwa Kristo kuja kama mfalme ilikuwa ni wakati wa kuja mara ya pili duniani. Wakati wa kuja kwa Yesu mara ya pili, atakuja katika mazingira tofauti kabisa na pale mwanzoni.Atakuja katika hali zifuatazo;
(a)    Atakuja kama umeme (Mathayo 24:27).
(b)   Atakuja pamoja na Malaika na uwezo wake (2Wathesalonike 1:7-8).
(c)    Atakuja juu ya mawingu pamoja na nguvu na utukufu mwingi
(Mathayo 24:30; Mwanzo 25:31).
(d)   Atakuja kama mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana (Ufunuo 19:16).

HALI HALISI YA KUJA KWA YESU MARA YA PILI DUNIANI.
   Mara tu baada ya harusi ya mwanakondoo, mwishoni mwa ile miaka saba, Yesu Kristo atawachukua watakatifu wote aliowanyakua na kuanza nao safari kuja duniani.Bwana Yesu atakuwa amepanda farasi mweupe akiongoza. Watakatifu nao kila mmoja atakuwa amepanda farasi mweupe wakifuata maelfu kwa maelfu pamoja na malaika, katika kitabu cha Yuda 1:14 Biblia inasema,” Na Heroko, mtu wa saba baada ya Adamu alitoa maneno ya unabii juu ya hao akisema, Angalia Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu na maelfu”. Pia katika kitabu cha Ufunuo 19:11-14 Biblia inasema, “Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye mwaminifu na wa kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita. Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto na juu ya kichwa chake vilemba vingi naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe. Naye amevikwa vazi lililochonya katika damu na jina lake aitwa, Neno la Mungu. Na majeshi yaliyo mbinguni yakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe safi”.
   Bwana Yesu atakuwa amezungukwa na mwali wa moto na atakuja kama umeme unaonekana pande zote. Na mara tu safari ya kuja duniani itakapoanza, jua litatiwa giza na mwezi hautatoa mwanga na nyota zitaanguka kutoka mbinguni kwa ajili ya kupamba sherehe ya kifalme. Nyota hizi ni zile zipitazo upesi mawinguni (Meteros) au kwa kiswahili “Vimondo” (Mathayo 24:29-30).
   Bwana Yesu atakuja na kukanyaga mlima mizeituni, mahali palepale alipopaa kwenda mbinguni wakati Yesu alipotoka duniani mara ya kwanza (Matendo 1:10-12). Katika kitabu cha Zekaria 14:4 Biblia inasema, “Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa Mizeituni unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki, nao mlima wa Mizeituni utapasuka katikati yake upande wa mashariki na upande wa magharibi, litakuwapo huko bonde kubwa sana na nusu ya mlima ule utaondoka kwenda upande wa kaskazini na nusu yake utaondoka kwenda upande wa kusini
   Mara tu baada ya kushuka, kazi ya kwanza atakayofanya Bwana Yesu itakuwa kuwatuma malaika ili kuwakusanya Waisraeli wote waliotawanyika duniani kote wakikimbia dhiki nzito juu ya Israeli katika ile miaka 3½ ya mwisho wa dhiki kubwa. Wale wote waliokwepa kupotezwa na Kristo wa uongo (Mpinga Kristo) watakusanywa (Mathayo 24:23-27;
Mathayo 24:29-31).

Tofauti kati ya kuja kwa Yesu wakati wa unyakuo wa kanisa na kuja kwa Yesu mara ya pili Duniani.
   Watu wengi huwa wanachanganya matukio haya mawili, lakini ni matukio yaliyo tofauti kabisa, lifuatalo ni jedwali linaloonyesha utofauti huo;

KUJA KWA YESU WAKATI WA KUNYAKULIWA KWA KANISA.
KUJA KWA YESU MARA YA PILI.
·    Anakuja kama Bwana Arusi kumchukua Bibi Arusi wake yaani kanisa tukufu lisilo na waa wala doa
 (Waefeso 5:27; Yohana 14: 1 – 3).
·    Bwana Harusi Yesu Kristo anakuja pamoja na bibi harusi kutoka huko juu na kuja hapa duniani kutawala na watakatifu wake (Yuda 1:14; Ufuno 1:7).
·    Anakuja na kukutana na watakatifu wake mawinguni hatakanyaga dunia na waliopo duniani hawatamwona wakati huu (1Wathesalonike 4:17).
·    Anakuja duniani na kukanyaga mlima Mizeituni na waliopo duniani watamwona (Zekaria 14:4-5: Mathayo 24:27).
· Kunyakuliwa kwa kanisa ni kabla ya Dhiki kubwa (Ufunuo3:10; Luka 21:22-23; Luka 21:34-36; 1Wathesalonike 1:10).
·    Kuja kwa Yesu mara ya pili duniani ni mara baada ya dhiki kubwa
 (Mathayo 24:29-30;2 Wathesalonike2:1-4).

MAKUSUDI YA KUJA KWA YESU MARA YA PILI DUNIANI.
  Yapo makusudi makuu matatu ya kuja kwa Yesu mara pili duniani;
a)      Kutawala mataifa yote duniani miaka 1,000 pamoja na watakatifu wake, kama mfalme wa wafalme na Bwana wa Mabwana (Ufunuo 11:15; Ufunuo 2:26; Ufunuo 5:10;
Ufunuo 20: 4-5).
b)      Kuwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu na wao wasioitii injili ya Bwana wetu Yesu Kristo (2Wathesalonike 1:8; Yuda 1:14-15)
c)      Kuwakusanya Waisraeli na kuwabagua Waisraeli (kondoo) mbali na mataifa waliosalia katika dhiki kubwa (mbuzi) Waisraeli wote watakaokusanywa wataokolewa na Yesu
 (Mathayo 24:31; Isaya 11:12; Mathayo 25:31 – 34; Warumi 11:25-31).

   Wana wa Israeli au Wayaudi, watabadilisha kabisa msimamo wao kuhusu masihi Yesu Kristo. Watalia kwa uchungu na wakiomboleza huku wakijilaumu kwa nini walimkataa na kumchoma kwa mkuki ubavuni na kisha watamkubali kuwa Masihi na mwokozi wao
(Ufunuo 1:7; Zekaria 12:10-14; Zekaria 13:6; Isaya 3:9; Zekaria 13:9).

VITA VYA HAR-MAGEDONI NA KUFUNGWA KWA SHETANI
MIAKA ELFU MOJA.
   Kabla ya utawala wa Kristo miaka 1000 pamoja na watakatifu wake kutatokea vita ijulikanayo kama vita vya Har-magedoni (Ufunuo 16:14-16). Vita hivi vitatokana na mpango wa shetani wa kutaka kuchukua ufalme kutoka kwa Yesu Kristo kama alivyojaribu kufanya mbinguni (Ufunuo 12:7-8).
   Kabla ya kuja kwa Yesu mara ya pili duniani kwa jitihada za pamoja; shetani, mpinga Kristo (Mnyama) na nabii wa uongo watatuma roho chafu ambazo zitawaandikisha watu wa mataifa yaliyobaki katika dhiki kuu kutoka duniani kote na kuweka tayari kwa vita ili kupigana na majeshi ya Yesu Kristo mahali paitwapo kwa kiebrania “Har-magedoni” Hapa ni bonde la Megido ambalo limekuwa mahari pa vita muda mrefu sana. Bonde hili lipo kusini magharibi mwa mlima karmeli, katika kitabu 2Nyakati 35:22 Biblia inasema, “Walakini Yosia hakukubali kumgeuzia uso mbali, akajibadilisha apate kupigana naye asiyasikilize maneno ya Neko, yaliyotoka kinywani mwa Mungu, akaja kupigana bondeni mwa Megido”. Pia katika kitabu chaZekaria 12:11 Biblia inasema” Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu kama maombolezo ya hadadrimoni katika bonde la Megido
   Kwa ujumla katika bonde hili, Yoshua alifanya vita na kumshinda mfalme wa mji huu wa wakanaani; katika eneo hili pia Sisera na jeshi lake walishindwa na hatimaye kukimbia, katika eneo hili Sulemani aliuimarisha mji, kadhalika Ahazia alikufa mahali hapa; pia Yosia aliuawa katika eneo hili katika vita na Farao Neko (Yoshua 12:21, Waamuzi 5:19-20; 1Wafalme 9:15; 2Wafalme 9:27, 2 Wafalme 9:23:29).
   Katika vita hiyo kutakuwa na mauaji makuu. Wenye dhambi watauwa kwa maangamizo makuu (Ufunuo 17:12-14, Ufunuo 14:19-20; Ufunuo 19:11-21; Isaya 13:9; Isaya 29: 5-8). Hapo ndipo Bwana Yesu ataonekana kuwa mtu wa vita na Bwana wa vita halisi, kama maandiko yanavyosema katika kitabu chaKutoka 15:3, “Bwana ni mtu wa vita Bwana ndilo jina lake” Baada ya vita hivi, shetani atashikwa na kufungwa miaka elfu moja (Ufunuo 20:1-3), na hapa ndipo utakapoanza utawala wa miaka elfu moja wa Yesu Kristo duniani.

Je ungependa kupanda farasi mweupe pamoja na Yesu?
 (Ufunuo 19:11-14).

MIAKA 1,000 YA UTAWALA WA YESU DUNIANI.
   Tulijifunza katika sura iliyopita jinsi ambavyo Yesu Kristo atakavyokuwa mtu wa vita au Bwana wa vita halisi. Yesu atawauwa wenye dhambi wote waliojipanga kupigana naye mahali paitwapo kwa Kiebrania Har-magedoni. Wale wote watakaouawa hapa, ndege watashiba nyama zao; kisha yule mnyama yaani mpinga Kristo na yule nabii wa uongo watakamatwa na kutupwa wangali hai katika ziwa la moto. Katika kitabu cha Ufunuo 19:20-21 Biblia inasema “Yule mnyama akakamatwa na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti na wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake yeye aliyeketi juu ya yule farasi, upanga utokao katika kinywa chake. Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao.”
   Baada ya tukio hilo, shetani naye atakamatwa na kutupwa kwenye shimo refu sana na kufungiwa humo kwa miaka 1,000. Biblia zote za Kiswahili limetumika neno shimo la kuzimu hata hivyo ni muhimu kufahamu kwamba hapa hawakumaanisha Jehanamu ya moto. Biblia za Kiingereza linatumika nenoBottomless pit (Ufunuo 20:1-3). Baada ya kufungwa shetani ndipo utawala wa Yesu Kristo duniani pamoja na watakatifu wake utakapoanza (Ufunuo 20:4-6).

MAKUSUDI YA UTAWALA WA YESU KRISTO MIAKA 1,000 DUNIANI.
   Ni vizuri tukifahamu kwamba mwanzoni kabisa katika mpango wa Mungu, mwanadamu alikusudiwa kuishi maisha ya amani, furaha na mafanikio chini ya utawala wa Mungu mwenyewe. Adamu alipotenda dhambi aliukatisha mpango huu kwa Mwanadamu na kutolewa katika bustani ya Edeni. Hapo ndipo maisha magumu kwa mwanadamu yalipoanza. Ardhi ililaaniwa na tukaanza kula chakula kwa jasho, na kuishi maisha ya taabu tofauti kabisa na mpango wa Mungu kwa mwanadamu (Mwanzo 3:13-19). Ndipo Mungu alipoanza mpango wa kumrudisha mwanadamu katika amani na furaha aliyomkusudia na hatimaye akaja Yesu Kristo duniani mara ya kwanza na kufa kwa ajili ya dhambi zetu. Hata hivyo katika kukamilisha kile alichokikatisha Adamu, Mungu katika mpango wake amekusudia kuuonyesha ulimwengu maisha yale aliyoyakusudia kwa mwanadamu kama wasingekubali kuacha utawala wake na kuugeukia utawala wa shetani. Kwa kuwa shetani atakuwa amefungwa miaka elfu moja, wanadamu wataweza kutawaliwa bila kushawishiwa na ibilisi kutenda dhambi na kuwa katika serikali moja duniani kote, iliyo chini ya mtawala Yesu Kristo. Utawala huu utawaongezea majuto wanadamu wenye dhambi waliomkataa Mungu atawale kwa kuona wema na uzuri wake.

HALI YA MAISHA ITAKAVYOKUWA DUNIANI WAKATI WA UTAWALA WA
YESU KRISTO DUNIANI.

1        FURAHA ITAJAA KABISA ULIMWENGUNI.
      Hakutakuwa na huzuni wala masikitiko kabisa ulimwenguni
      (Isaya 9:3-4; Yeremia 31:13).
2        UTAKATIFU UTATAWALA DUNIANI.
      Kama ilivyokuwa kipindi cha waamuzi katika agano la kale, watakatifu watakaotawala na Kristo watakuwa ni waamuzi. Watashauri watu na kuwahukumu kwa hekima kuu itakayoleta maisha ya uaminifu na yote yanayompendeza Mungu (Isaya 1:26)
3        HAKUNA KUUGUA DUNIANI.
Magonjwa ni ya shetani, kwa kuwa shetani atakuwa amefungwa, kutakuwa hakuna magonjwa kabisa na hosipitali zitakuwa hazina kazi. Isaya 33:24Biblia inasema, “Wala hapana mwenyeji atakayesema, mimi mgonjwa; watu wakaao humo watasamehewa uovu wao.”
4        LAANA JUU YA ARDHI ITAONDOLEWA.
Laana ya mwanzo (Mwanzo 3:17-19) itaondolewa hakutakuwa na miiba wala magugu. Mvua itakuwa ya manyunyu safi. Ukilima kidogo utavuna sana. Kutakuwa hakuna kula kwa jasho (Ezekieli 34:26-27).
5        Utakuwa utawala wa haki tupu wala watu hawatasikia upendeleo, rushwa, ufisadi nk. (Isaya 9.7; Isaya 11:5; Yeremia 23; 5 ; Isaya 33:15).
6        KUTAKUWA HAKUNA KUFA.
      Watu watazaliwa tu, lakini hakuna kufa. Watu watakuwa wengi mno duniani (Amosi 9:15; Zekaria 14:9-11)
7        Hakuna kuonewa, njaa, kiu wala mateso (Isaya 49:10; Isaya 14:3-7). Nyakati hizo zitajaa kuimba tu  hakuna jua kali wala baridi kali.
8        Dunia itapendeza mno na hakutakuwa na umasikini. Kila sehemu kutakuwa na maua mazuri mno wala hakutakuwa na magonjwa kabisa (Isaya 65:21-24; Isaya 35:1-2)
9        DUNIA ITAJAWA NA KUMJUA BWANA.
      Kila mtu atamjua Mungu yaani wema wake, uzuri wake, haki yake n.k kila mtu atamjua Yesu kuwa ni Mungu na kujawa maarifa kamili ya mpango wake kwa mwanadamu
      (Isaya 11:9; Habakuki 2:14).
10    HAKUTAKUWA NA VILEMA, VIZIWI, MABUBU DUNIANI.
      Kazi zote hizi zilitokana na shetani kupewa nafasi kumtawala Adamu. Zitamalizwa katika utawala wa Yesu duniani (Isaya 29:18; Isaya 35:3-6).
11    Hakutakuwa na vita kabisa kati ya mwanadamu na mwanadamu.Silaha zitabadilishwa kuwa vyombo vya amani kama maandiko yanavyosema katikaIsaya 2:4,” Naye atafanya hukumu kati ya mataifa mengi, atawakemea watu wa kabila nyingi; nao watafua panga zao ziwe majembe, mikuki yao iwe miundu, taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe.”(Zekaria 9:10; Mika 4:3). Juhudi za kuleta amani zimeshindikana kuletwa na umoja wa mataifa hivi sasa.Haya yote yatatimia wakati wa utawala wa Yesu duniani.Katika utawala huu hakutakuwa na mbu,funza,kunguni au wadudu wowote wabaya kama bacteria n.k.Vilevile hakutakuwa na ndege wa kula nafaka wala wanyama waharibifu.Katika kitabu cha Hosea 2:18 Biblia inasema,” Nami siku hiyo nitafanya agano na wanyama wa mashamba kwa ajili yao,tena na ndege wa angani,tena na wadudu wa nchi,nami nitavivunja upinde na upanga na silaha vitoke katika nchi, nami nitawalalisha salama salmini.” Kutakuwa na amani kati ya mnyama na mnyama.Simba atakula majani, chui atalala pamoja na mwanambuzi, simba na ng’ombe watakula pamoja.Nyoka hawatakuwa na madhara tena (Isaya 11:6-9). Hakutakuwa na wizi au unyang’anyi.Wakati huo hakutakuwa na haja ya kufunga milango na makufuli
(Ezekieli 34:25-28).

VITA VYA GOGU NA MAGOGU.
   Mwishoni mwa miaka elfu moja, shetani atafunguliwa kutoka kifungoni, na ataanza kuwadanganya watu wote na kuwashawishi ili wafanye vita na kupigana na Yesu pamoja na watakatifu wake. Watu wote kwa kuwa wana asili ya dhambi watashawishika na waasi watajikusanya nchi ya Gogu na Magogu iliyo Kaskazini ya Palestina mashariki ya kati na kuja kuishambulia maskani kuu ya watakatifu yaani Yerusalemu. Hapo ndipo itatokea vita vya Gogu na Magogu. Hasira ya Mungu itawaka na wanadamu wote wataangamizwa kwa kuliwa na moto utakaoshuka kutoka mbinguni. Watasalia tu watakatifu pamoja na Yesu. Shetani naye atakamatwa na kutupwa katika ziwa la moto (Ufunuo 20:7-10). Wale wote walioliwa na moto, watakuwa wote Jehanamu ya moto kusubiri ufufuo wa pili au ufufuo wa hukumu.

Je ungependa kutawala pamoja na Yesu Duniani?
 (Ufunuo 20:6).

JEHANUM YA MOTO.
   Watu wengi, mamekuwa wakijiuliza kwamba, Je, watu wanaokufa katika hali ya dhambi wanakwenda wapi? Jibu ni kwamba wanakwenda Jehanum ya moto na ndiyo maana Bwana wetu Yesu Kristo anatufundisha waziwazi kuhusu Jehanum ya moto akituonya kumuogopa Mungu mwenye uwezo wa kututupa Jehanum. Anaendelea kutuonya kwamba ni heri kukubali lolote lile litupate kuliko kwenda kwenye mateso makali ya Jehanum. Katika kitabu cha Luka 12:5 Biblia inasema, “Lakini nitawaonya mtakayemuogopa; mwogopeni yule ambaye akiisha kumuua mtu ana uweza wa kumtupa katika Jehanum, naam nawaambia mwogopeni huyo.” Soma pia (Mathayo 5:2, Mathayo 5:29-30). Maandiko pia yanaendelea kusisitiza kwa msisitizo mkubwa kwamba ni jambo la kutisha kuanguka katika mkono wa Mungu aliyehai na kutupwa katika Jehanam ya moto (Waebrania 10:26 – 31).
   Jehanum ya moto inaitwa pia “kuzimu”. Katika kitabu cha Zaburi 9:17 Biblia inasema, “Wadhalimu watarejea kuzimu, naam mataifa yote wanaomsahau Mungu.” Jehanum ya moto pia inaitwa “Tofethi”; katika kitabu cha Isaya 30:33 Biblia inasema, “Maana tofethi imewekwa tayari tokea zamani, naam imewekwa tayari kwa mfalme huyo; ameifanya kubwa, inakwenda chini sana, tanuru yake ni moto na kuni nyingi pumzi ya Bwana, kama moto wa kiberiti huiwasha”Kamwe hatupaswi kulipuuzia jambo hili na kulifahamu jambo hili kijuujuu tu. Hivyo basi ningeomba uendelee kufuatana nami ili uweze kujifunza kwa undani sana kuhusu eneo hili la hatari sana.

HUKUMU BAADA YA KUFA.
   Biblia inaeleza waziwazi kwamba mtu anapokufa sekunde ileile ya kufa kwake anakabiliwa na hukumu, katika kitabu cha Waebrania 9:27 Biblia inasema, “Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja na baada ya kufa hukumu.” Kuna watu wanafundisha kinyume na kweli ya neno la Mungu, hufundisha kwamba mtu anapokufa analala tu na hakuna lolote la hukumu ya mara moja. Wanatumia maandiko yanayozungumzia kulala kwa kuyatafsiri isivyo (Mathayo 27:52; 1Wakorintho 15:20; Yohana 11:11 – 14) na pia huwadanganya watu kwa kusema kuwa wafu hawajui lolote kwa kutumia maandiko kama Mhubiri 9:5.
   Ukweli ni kwamba, kinachobaki kaburini ni mwili tu, Nafsi na roho ya mtu huondoka na kuvalishwa mwili mwingine kabisa kama Biblia inavyosema katika1Wakorintho 15:40, “Tena kuna miili ya mbinguni na miili ya duniani, lakini fahari yake ile ya mbinguni ni mbali na fahari yake ile ya duniani ni mbali.”Mwili unaobaki kaburini ndiyo ambao umelala haujui lolote na hauna kumbukumbu, lakini pasipo mwili huo, mtu atamwona Mungu ikiwa ameishi katika mapenzi yake (Ayubu 19:26). Mwili hubaki kaburini lakini roho ya mtu huondoka (Muhubiri 12:7). Ikiwa mtu ameishi katika mapenzi ya Mungu, mara tu baada ya kufa huchukuliwa mbinguni na malaika kwa kutumia magari maalumu ya mbinguni,katika kitabu cha  Zaburi 68:17 Biblia inasema, “Magari ya Mungu ni ishirini elfu, maelfu maelfu; Bwana yumo kati yao kama katika Sinai katika patakatifu”.Soma pia (Luka 16:22; 2Wafalme 2:11-12). Lakini ikiwa mtu huyu ameishi katika dhambi hukumu yake huwa kutupwa katika Jehanam ya moto mara baada ya kufa (Mithali 9:13-18; Isaya 5:11-15; Mithali 7:24-27).

JEHANUM YA MOTO IKO WAPI?
   Mara mtu anapokufa tu huwa kwenye njia panda. Kila mmoja hupenda kwenda mbinguni hata hivyo ikiwa jina lake halimo katika kitabu cha uzima cha mbinguni, hulazimika kwenda Jehanum ya moto. Mtu anayetakiwa kwenda Jehanam ya moto huchachamaa na kukataa kwenda kwenye njia mbaya inayotisha ya motoni na hulazimika kukamatwa na kutupwa Jehanam kwa nguvu (Ufunuo 19:20; Ufunuo 20:10).Kuzimu au Jehanam ya moto ipo chini yaani pande za chini za nchi, katika kitabu cha Mithali 15:24, Biblia inasema, “Kwa mtu mwenye akili njia ya uhai huenda juu, ili atoke katika kuzimu chini.”(Zaburi 63:9; Ezekieli 31:14)

HALI HALISI YA JEHANUM YA MOTO NA WALE WALIOKO HUKO.
   Jehanum ya moto ni shimo kubwa na refu sana lililojaa moto. Moto huu huwashwa mfululizo kwa pumzi ya Bwana (Isaya 14:15; Isaya 30:33). Moto huu ni mkali sana kuliko moto wowote tunaoufahamu hapa duniani, uwe wa gesi, umeme, makaa ya mawe au lolote jingine, kitabu cha Waebrania 10:27 Biblia inasema, “Bali kuna kuitazama hukumu yenye kutisha na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.” Moto huu ni mweusi sana unaosababisha giza na kufanya mtu awaone wenzake wachache tu wa karibu naye (Mathayo 8:11-12; Yuda 1:6). Moto huu una uwezo wa kula na kutafuna, hivyo huwala na kuwatafuna wale walioko motoni na kufanywa milio mikubwa kama milipuko ya mabomu. Wakati wote watu walio katika moto huu ndimi zao huwa ziko nje kama mbwa wakitamani wadondoshewe angalau tone la maji, kitabu chaLuka 16:23-24 Biblia inasema, “Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake alipokuwa katika mateso akamwona Ibrahimu kwa mbali na Lazaro kifuani mwake Akalia, akasema Ee baba Ibrahimu nihurumie umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini auburudishe ulimi wangu kwa sababu ninateswa katika moto huu.”Hata hivyo, kama jinsi ambavyo chumvi inavyozuia nyama kuharibika, vivyo hivyo na moto huu humtafuna mtu lakini hamaliziki (Marko 9:43-49) Huu ni moto wa milele (Mathayo 25:41).

MAFUNDISHO POTOFU JUU YA MOTO WA MILELE.
   Kuna mafundisho potofu yanayowafariji watu na kusema eti mtu ataunguzwa na moto na kutoweshwa au kupotea na kuangamia kabisa na hivyo kufikia mwisho. Haya ni mafundisho potofu yanayoletwa na shetani kupitia watu fulani ili kuwadanganya watu. Wanatumia maandiko kama Mathayo 10:28(kuangamizwa) na Yohana 3:18 (Kupotea). Kuangamizwa hakumaanishi kutoweka kabisa kama alivyolitumia neno hili Esta wakati anataka kwenda kuonana na mfalme (Esta 4:16). Mfano Kondoo akipotea haimaanishi hayupo kabisa bali ametengwa na mchungaji (Isaya 57: 1-3). Kadhalika neno “Kuharibu” linapotumika kuhusiana na adhabu ya milele halina maana ya kufanya kitu kisiwepo bali ni kuadhibu vikali (1Wakorintho 3:16-17).
   Walimu hawa wa uongo hufundisha pia kwamba ati watu watatoweshwa kama moshi baada ya kuungua na wanatumia andiko la Zaburi 37:20; Kutoweshwa hapa ni kutenganishwa mbali na Mungu. Pia wapo wanaojifariji kwa kusema kuwa Mungu hawezi kumchoma moto mwanadamu kwani yeye ni Mungu wa huruma, hivyo wenye dhambi watahurumiwa. Ni kweli Mungu ana huruma sana, lakini ni wakati huu ambao unahubiriwa injili ili upate kutubu wakati ukiwa duniani, lakini baada ya hapo, ghadhabu ya Mungu itamkalia kila aliyetenda dhambi. Angalia gharika ya Nuhu katika kitabu cha Mwanzo 7:1-24 jinsi Mungu alivyowaharibu wanadamu wote wakubwa kwa wadogo na akabaki Nuhu na familia yake. Pia angalia miji ya Sodoma na Gomora (Mwanzo19:1-26).Mungu alivyoiharibu kwa moto na akapona Ruthu na watoto wake tu na katika miji hiyo walikuwepo wakubwa kwa watoto.

MAKALI YA JEHANUM YA MOTO.
   Moto huu wa milele huambatana na madini yanayoitwa kiberiti au kwa lugha ya kitaalamu yanaitwa “Sulphur”. Madini haya yakiwaka huwa kama mpira na hutoa harufu mbaya kama mayai viza (mayai yaliyooza). Harufu ya namna hii inaifunika kuzimu yote. Lakini pia katika moto huu wamo funza maalum ambao huwatafuna watu na kuifanya miili yao iwe na matundu mengi na funza hawa huingia katika miili yao na kutoka. Hii hufanya miili ya watu na sura zao kuwa mbaya mno kama madude ya kutisha! (Isaya 14:11; Marko 9:43-49; Isaya 66:24). Kutokana na moto huu kuwa mweusi hufanya miili yao kuwa myeusi kama mkaa. Watu walioko motoni hujawa na wakati wote na vilio na tena husaga meno yao kama mtu anayehisi baridi kali sana (Mathayo 8:12), hivyo kuwafanya waonekane wamechakaa sana. Hakika kuzimu ni pigo lifurikalo ambalo huwachukua wenye dhambi asubuhi, mchana na usiku (Isaya 28:15, Isaya 28:18-19). Walioko motoni hujifahamu sana zaidi hata walipokuwa duniani na kuwakumbuka ndugu, marafiki na majirani zao (Luka 16:19-24).
   Juu ya yote hayo, katika vilio vyao humwomba Mungu awahurumie na kuwasamehe lakini Mungu mwenyewe amekwisha sema, “Nami jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma”. (Ezekieli 9:10; Ezekieli 8:18)

USEMI NA FIKRA ZA WALE WALIOKO MOTONI.
11    Watu walioko motoni hutamani sana mtu mmoja kati yao aje awashuhudie ndugu zao duniani ili waache dhambi na kukwepa mateso yao (Luka 16:27-31).
12    Wale walioko motoni ambao walilijua kweli neno la Mungu na wakateleza, husema maneno yafuatayo, “Jinsi nilivyochukia maonyo na moyo wangu ukadharau kukemewa, wala sikuisikia sauti ya waalimu wangu, wala sikuwategea sikio langu walionifundisha.”(Mithali 5:11-13).
13    Watu walioko motoni wakimwona mtu yeyote ametumbukia huko waliko humwambia huku wanalia, “Je, wewe nawe umekuwa dhaifu kama sisi! Wewe nawe umekuwa kama sisi!” (Isaya 14:9-10).
Lakini pia wale watakaokuwepo mbinguni watapewa nafasi kidogo ya kuwaangalia waliopo motoni (Isaya 66:24), lakini hawatakuwa na huzuni wala machozi yoyote juu yao.

TOFAUTI KATI YA JEHANUM YA MOTO NA ZIWA LA MOTO.
   Jehanum ya moto ni tofauti kabisa na ziwa la moto linalotajwa katika Ufunuo 20:14-15; Ufunuo 21:8; kwa jinsi ileile mbingu ya sasa ilivyo tofauti na mbingu mpya inayotajwa katika Ufunuo 21:1. Ziwa la moto kwa sasa halina mkazi ndani yake. Watakaokuwa wa kwanza kuingia humo watakuwa Mnyama (Mpinga Kristo) na nabii wa uongo (Ufunuo 19:20). Kisha atafuata Ibilisi ambaye atatupwa humo baada ya vita vya Gogu na Magogu (Ufunuo 20: 7-10). Baada ya hapo kutafuata hukumu ya kiti cha enzi cheupe kikubwa. Hukumu hii itatolewa baada ya ufufuo wa pili au ufufuo wa hukumu ambao utawafufua walioko Jehanam ya moto. Baada ya hawa kuelezwa kwa nini wamehukumiwa adhabu ya mateso ya milele ndipo watakapotupwa katika ziwa la moto. Mateso yaliyoko katika ziwa la moto ni zaidi sana kuliko mateso ya Jehanam ya moto. Ni kama Jehanam walikuwa mahabusu na sasa wanapelekwa gerezani. Kama mbingu mpya itakavyokuwa nzuri zaidi kuliko mbingu ya sasa, vivyohivyo ziwa la moto litakuwa na mateso yaliyokithiri kuliko Jehanum ya moto, maana mauti na kuzimu vyote vitatupwa humo (Ufunuo 20:14).


JINSI YA KUIKWEPA JEHANUM YA MOTO.
1.      Kuungama dhambi na kuziacha (Mithali 28:13).
2.      Kulishika neno la Mungu kwa kufanya maagizo yote ya Mungu na kuwakataa wafariji wenye kutaabisha wanaosema kufanya hili na lile siyo lazima (Yohana 8:5; Zaburi 119:6;
 Ayubu 16: 1-2)
3.      Kutoihesabu sheria kuwa kitu kigeni. Kukubali kuongozwa na sheria ya Kristo. Hakuna mwanafunzi asiyeishi kwa sheria. (Hosea 8:12; Wagalatia 6:2; Isaya 8:16)
4.      Kuwa mtakatifu na kutoifuatisha namna ya dunia hii katika mavazi, usemi, matendo n.k (Waebrania 12:14; Warumi 12:2; Yakobo 4:4; 1Yohana 2:15-17).

Je nawe utakuwa dhaifu kama walio Jehanam ya moto
(Isaya 14:9-10).

UFUFUO WA WAFU.
   Mtu anapokufa moja kwa moja anakwenda kukutana na hukumu yake (Waebrania 9:27). Kama mtu amekufa akiwa ameokoka na kuishi katika utakatifu mpaka dakika yake ya mwisho, sekunde ileile anakwenda peponi (Luka 23:39-43; Matendo 7:54-59; Wafilipi 1:21-23). Ikiwa mtu amekufa akiwa hajaokoka sekunde ileile anakwenda katika mateso ya moto wa Jehanum (Luka 16:19-28). Ingawa mwili wa mtu anayekufa unabaki kaburini, roho yake pamoja na nafsi yake vinaambatana na mwili mpya kwa kuwa kuna miili ya duniani tena kuna miili ya mbinguni (1Wakorintho 15:40-44; Ayubu 19:25-27; Mhubiri 12:7). Katika mwili mpya, mtu anakwenda motoni au mbinguni. Akiwa huko atajijua kabisa. Atakuwa anaona, kuhisi, kusikia na kuwa na kumbukumbu hata ya ndugu zake waliobaki duniani (Luka 16:27-31)

UHAKIKA WA UFUFUO WA WAFU.
   Ufufuo wa wafu ni moja ya masomo ya msingi sana katika ukristo na pia ni mafundisho ya kwanza ambayo kila mkristo inampasa kuyafahamu (Waebrania 6:1-2). Kiyama cha wafu au ufufuo wa wafu, umetabiriwa mapema katika neno la Mungu kwenye vitabu vya Luka 14:13-14; Yohana 5:28-29; Wafilipi 3:10-11; 1Wathesalonike 4:16. lakini hata hivyo, Yesu Kristo ndiye kielelezo cha ufufuo wa wafu na uhakika wa ufufuo wa wafu kwa watu wote. Katika kitabu cha1Wakorintho 15:20, Biblia inasema, “Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu limbuko lao waliolala.” Yesu Kristo alitabiri mapema juu ya kufufuka kwake kabla hata hajafa (Mathayo 16:21; Mathayo 17:22-23, Mathayo 20:17-19; Marko 8:31-32, Marko 10:32-34; Luka 9:20-22, Luka 18:31-34), lakini kutokuamini kwa wayahudi hakukuzuia kufufuka kwa Yesu, vivyo hivyo hata leo pamoja na kuwepo kwa watu wasioamini kwamba kutakuwa na ufufuo wa wafu, kutokuamini kwao hakutaweza kuzuia jambo hilo kutokea (Warumi 3:3-4). Uongo wa askari walinzi wa kaburi la Yesu walioutawanya baada ya kupokea rushwa na kufundishwa kusema uongo kwa kuambiwa, “Semeni ya kwamba wanafunzi wake walikuja usiku, wakamwiba, sisi tulipokuwa tumelala”, ni uongo ulio dhahiri (Mathayo 28:11-15). Ikiwa walinzi walikuwa wamelala usingizi waliwaona namna gani watu waliokuja kuuiba mwili wa Yesu na kufahamu kwa hakika ni wanafunzi wake? Na kama waliwaona kwa nini waliwaacha wakauiba mwili huo na wasiwazuie kufanya hivyo?. Ni uongo ulio wazi. Ni jambo lililo dhahiri kwamba Yesu alifufuka! Kwa jinsi hiyohiyo, ufufuo wa wafu wote ni jambo lililo dhahiri kabisa kutokea.

UFUFUO WA WAFU UNAVYOFANYIKA.
   Ufufuo wa wafu ni kama kuvua nguo mpya na kuvaa nguo ya zamani. Kwa jinsi ambavyo mtu alivyokufa na kuacha mwili wake duniani, ndivyo itakavyokuwa tena. Katika ufufuo wa wafu mtu atatoka katika Jehanam ya moto na kuurudia mwili wake wa duniani au atatoka peponi au mbinguni na kuurudia mwili wake wa duniani. Hata kama mwili ule umekuwa udongo baada ya miaka mingi ni muhimu kukumbuka kwamba Mungu aliyemuumba mwanadamu kutoka katika mavumbi, hashindwi kufanya mwili uliokuwa udongo urudie hali ya mwili tena (1Wakorintho 15:42-44).

AINA ZA UFUFUO WA WAFU.
Katika mpango wa Mungu wa ufufuo wa wafu, kuna aina mbili za ufufuo wa wafu;
1: Ufufuo wa kwanza au ufufuo wa uzima.
   Ufufuo huu umepewa majina mengine pia katika Biblia kama ufufuo ulio bora au ufufuo wa wenye haki (Yohana 5:28-29; Ufunuo 20:4-6; Luka 14:13-14; 1Wathesalonike 4:16; Waebrania 11:35). Ufufuo wa kwanza unajumuisha wale wote waliokufa na kwenda mbinguni yaani wenye haki au watakatifu. Hawa ndiyo wenye sehemu katika ufufuo wa kwanza. Huu ni ufufuo wa uzima kwa sababu wale wote watakaokuwa katika ufufuo huu watakuwa katika uzima wa milele katika mbingu mpya na nchi mpya. Huu ndiyo ufufuo ulio bora. Ufufuo huu umegawanyika katika sehemu mbili.

(a)   Ufufuo wa watakatifu wote walio mbinguni wakati wa kunyakuliwa kwa kanisa.
Hawa watafufuliwa kwanza kisha kufumba na kufumbua miili yao itabadilishwa na kuwa ya utukufu kisha wote kwa pamoja watakwenda kumlaki Bwana Yesu mawinguni (1Wathesalonike 4:16).

 (b)  Ufufuo wa watakatifu wa wakati wa dhiki kuu.
Hawa ni watakatifu ambao hawakumsujudia yule mnyama yaani mpinga Kristo wala sanamu yake na kukataa kabisa kupokea chapa ya 666 katika vipaji vya nyuso zao na hivyo kuteswa na kuuawa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu na neno la Mungu wakati wa dhiki kuu. Hawa watafufuliwa wakati wa kuja kwa Yesu Kristo mara ya pili pamoja na watakatifu wake walionyakuliwa. Watakatifu hawa baada ya kufufuliwa huku moja kwa moja watatawala pamoja na Kristo miaka elfu moja duniani (Ufunuo 20:4-6).

2: Ufufuo wa pili au ufufuo wa hukumu.
   Ufufuo huu pia unaitwa ufufuo wa aibu na kudharauliwa (Yohana 5:29; Danieli 12:2). Huu ni ufufuo wa watenda mabaya au wenye dhambi wote ambao watakuwa Jehanam hivi sasa hadi wale watakaokwenda huko baada ya vita vya Gogu na Magogu itakayofanyika mwishoni mwa miaka elfu ya utawala wa Yesu Kristo duniani, ambayo itawamaliza wenye dhambi wote na kisha waende wote motoni. Wote hawa watafufuliwa katika ufufo huu wa pili utakaofanyika muda mfupi baada ya miaka elfu ya utawala wa Kristo miaka elfu duniani. Walipokwenda motoni walikuwa hawajaelezwa waziwazi makosa yaliyowapeleka motoni sasa hapa ndipo Yesu Kristo mhukumu wa haki atakapo waonyesha waziwazi mbele ya watu wote. Hapa ndipo watu watajitetea, “Bwana Bwana hatukufanya unabii kwa jina lako na kwa jina lako kutoa pepo …………” naye Yesu mhukumu wa haki atawaambia dhahiri, sikuwajua ninyi kamwe! ondokeni kwangu ninyi mtendao maovu wote watatupwa kwenye ziwa la moto.

Je baada ya maisha ya duniani utakuwa katika ufufuo upi?

HUKUMU YA MWISHO
   Baada tu ya vita vya Gogu na Magogu vitakavyofanyika mwishoni mwa miaka elfu moja ya utawala wa Yesu Kristo duniani, kutafuata ufufuo wa pili unaoitwa pia ufufuo wa Hukumu (Yohana 5:28-29). Huu ni ufufuo wa wale waliotenda mabaya, yaani wote wenye dhambi waliokufa pasipo utakatifu, tangu nyakati za mwanzo kabisa za vizazi vya Adamu hadi wale wote watakaoliwa kwa moto kwenye vita vya Gogu na Magogu (Ufunuo 20:7-9). Hawa wote baada ya kufa kwao wamekuwa katika kipindi chote hicho kwenye mateso makali katika Jehanam ya moto. Hawa watafufuliwa na kurudia miili yao ya asili na kusimama mbele ya kiti cha enzi kikubwa cheupe cha hukumu.

HAKIMU ATAKAYEHUKUMU.
   Hakimu huyu ni Yesu Kristo. Maandiko yanaelezea jambo hili waziwazi, Biblia inasema katika kitabu cha Yohana 5:22, “Tena Baba hamhukumu mtu yeyote, bali amempa Mwana hukumu yote.” Neno la Mungu pia linasema katika 2Timotheo 4:1, “Nakuagiza mbele za Mungu,na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu walio hai na waliokufa ;kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake.” Soma pia (Matendo 10:36; Warumi 2:16).
   Wakati wa hukumu, Bwana Yesu atakikalia kiti cha enzi kikubwa cheupe cha hukumu. Hivyo yeyote anayemkana Yesu leo kuwa siyo Mungu atafahamu hapa kwamba hukumu yote iko chini yake (Yohana 5:22;  Matendo 10:38-41, Warumi 2:16; 2Timotheo 4:1). Ni heri kufahamu mapema hivi leo kwamba Yesu ndiye hakimu na kuomba msamaha kwake, yeye yuko tayari na kurehemu na kusamehe kabisa (Isaya 55:6-7). Yesu atakapokikalia kiti cha enzi kikubwa cheupe atakuwa mwenye hasira, huruma itakuwa mbali naye kabisa (Ezekieli 7:4, Ezekieli 8:18; Warumi 2:4-5).

LENGO LA HUKUMU HII.
   Hukumu hii haitakuwa na lengo la kuwaweka huru wenye dhambi fulani. Hivyo ni kwamba yeyote yule asiyemwamini Yesu hadi kufa kwake ghadhabu ya Mungu inamkalia kama Biblia inavyosema katika Yohana 3:36, “Amwaminiye mwana yuna uzima wa milele, asiye mwamini Mwana hatauona uzima bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.” Kawaida mtu yeyote mwenye dhambi anapokufa huenda motoni moja kwa moja. Mtu huyu huenda huko bila kuelezwa ni kwa nini anapelekwa kwenye mateso hayo. Makusudi ya hukumu hii itakuwa kumfahamisha kila mmoja aliye katika mateso ya Jehanam uhalali wa yeye kupewa hiyo adhabu ya milele. Itadhihirishwa kwa kila mmoja kwamba adhabu ya moto wa milele ni malipo halisi aliyoyapata kadri ya matendo yake (Warumi 2:6). Yesu hapa anasimama kama mhukumu wa haki kama Biblia inavyotueleza katika Matendo 17:31, “Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki …………….”

IDADI KUBWA YA WATU WATAKAOHUKUMIWA.
   Watu wanaokwenda Jehanam ni wengi sana kuliko wengi wanavyofikiria (Mathayo 7:13-14). Mbinguni kuna vitabu vya aina mbili; Kitabu cha uzima ambamo huandikwa majina ya wale waliookoka ambao hudumu kutenda mapenzi ya Mungu,katika kitabu cha Luka 10:20 Biblia inasema, “Lakini msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii, bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.” Soma pia (Wafilipi 4:3). Wale waliookoka wasiodumu kutenda mapenzi ya Mungu, hufutwa majina yao na kuondolewa katika Kitabu cha uzima, kitabu cha Kutoka 32:33 Biblia inasema, “BWANA akamwambia Musa, mtu yeyote aliyenitenda dhambi ndiye nitakayemfuta katika kitabu changu”.Soma pia (Ufunuo 3:5).
   Wale wote watendao dhambi na kuwa mbali na wokovu majina yao yamo katika vitabu vya kumbukumbu vya hukumu. Kwa kuwa watu hawa ni wengi sana, majina yao yapo katika vitabu vingi, lakini wale wa mbinguni wapo katika “Kitabu kimoja cha uzima” (Ufunuo 20:12). Kamwe hatupaswi kudanganyika kutokana na watu wengi wanaosema wameokoka huku maisha yao hayako nuruni na kufikiria kwamba wote hawa wataingia mbinguni. Gharika iliwaangamiza wote duniani na kubakiza wanane tu Safinani. Viwango vya Mungu vya utakatifu havibadiliki (Mathayo 5:48; Waebrania 12:14; 1Petro 1:15-17).

WATOTO WADOGO PIA KUHUKUMIWA.
  Wakubwa kwa wadogo watakuwepo kwenye hukumu hii, kama Biblia inavyosema katika kitabu cha Ufunuo 20:12, “Nikaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi na vitabu vikafunguliwa na kitabu kingine kikafunguliwa ambacho ni cha uzima na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.” Ni muhimu kuwashuhudia injili watoto wetu wadogo walio na akili ya kujua mema na mabaya na kuwapa nafasi ya kutubu na kuokolewa au sivyo tutahuzunika kuwaona wakiwa kwenye hukumu hii, wakiwa wametoka kwenye mateso ya moto. Kwa mtoto mdogo anayeweza kufahamuhesabu ya 59 + 68, ana upeo mkubwa wa kufahamu mema na mabaya. Katika injili yetu kwa watoto wa jinsi hii tunatakiwa kutaja dhambi wanazoweza kuzielewa kama vile wizi wa penseli, uongo, kutokuwatii wazazi, kiburi, ukaidi n.k. Ni muhimu kukumbuka kwamba ni watoto wadogo kabisa wasiofahamu sheria ambao ufalme wa Mungu ni wao umri wa kukumbatiwa (Marko 10:13-16; Warumi 4:15; 5:13).

KIPIMO KITAKACHOTUMIWA KATIKA HUKUMU.
  Watu wengi wanafanya makosa makubwa sana pale wanapojifariji na kufikiria kwamba watakwenda mbinguni kutokana na kufanya mambo yaliyo sawa na mafundisho ya madhehebu yao au wachungaji wao. Hiki siyo kipimo kitakachotumiwa na Yesu katika kuhukumu. Wengi wanaojifariji kwa kutenda yaliyo halali kwa wachungaji, manabii, mitume, walimu au wainjilisti au madhehebu yao, ingawa yapo tofauti na maagizo ya neno la Mungu, watakwenda katika mateso ya moto wa milele.
  Kipimo atachotumia Yesu katika hukumu ni neno la Mungu kama Biblia inavyosema katika Warumi 2:16,”Katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu sawasawa na injili yangu kwa Kristo Yesu.”Ni jambo la msingi sana kulinganisha yale tunayofanya au kuyafundisha na neno la Mungu na siyo na mafundisho ya madhehebu yetu au wachungaji na maaskofu wanaotuambia kufanya hili na lile siyo lazima (Utafikiri wanambingu ya kukupeleka), wakati neno la Mungu linatuambia, “Ndipo mimi sitoaibika nikiyatafuta maagizo yako yote” (Zaburi 119:6). Siyo hilo tu, kwa vile kipimo cha Yesu katika hukumu kitakuwa ni neno la Mungu hivyo wale ambao waliokaa katika makanisa ambayo hayakuwa na mafundisho pamoja na wale ambao walikatazwa na wazazi wao kuwa wakristo, wote hawa watapotea pasipo sheria. Kukosa kuifahamu yaliyo halali, siyo udhuru utakaokubalika, kwani kama uliweza kuwa na juhudi katika kutafuta chakula cha mwili ulishindwa nini kutafuta chakula cha kiroho, pia kama uliweza kuwa na juhudi ya kutafuta elimu ya duniani, ulishindwa nini kuwa na juhudi ya kutafuta kuyajua mapenzi ya Mungu. Wale wanaofahamu mafundisho ya kweli lakini hawayatendi na kuyafundisha, watapigwa sana yaani kuteswa zaidi kuliko wale ambao hawakuyajua, kama maandiko yanavyosema katika kitabu cha Luka 12:48, “Na yule asiyejua naye amefanya yastahiliyo mapigo atapigwa kidogo. Na kila aliyepewa vingi; kwake huyo vitatakwa vingi; kwake huyo watataka na zaidi.” Soma pia (Warumi 2:11-14; Walawi 5:17). Mungu anamtarajia kila mwanadamu kuyatafuta mafundisho ya kweli hata iwe mbali kiasi gani kama alivyotayari kuifuata elimu Ulaya au biashara nchi za nje. Katika kitabu cha Mathayo 12:42 Biblia inasema, “Malkia wa kusini atasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki naye atawahukumu kuwa wamekosa kwa sababu yeye alikuja kutoka pande za mwisho za dunia ili asikie hekima ya Sulemani na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani.” Hivyo, hata kama eneo ambalo wanafundisha kweli lipo mbali nawe anza kutia bidii kuanzia leo, ili usije ukahukumiwa kwa ushuhuda wa Malkia wa kusini.

KUFUNULIWA KWA SIRI ZOTE MBELE YA MASHAHIDI WA MUNGU.
   Mwenye dhambi mmoja baada ya mwingine, watasimama mbele ya kiti cha enzi kikubwa cheupe. Mahali hapo itakuwa mahali pa aibu na kudharauliwa (Danieli 12:2). Kila mmoja ataonyeshwa matendo yake, maneno yake, mawazo yake na nia yake kwa mfano wa video iliyotunza kumbukumbu zake. Siri zote za wanadamu zitakuwa wazi mahali hapo. (Mithali 26:26; Mhubiri 12:14; Luka 12:2; 1Wakorintho 4:5; Ayubu 20:27). Mahali hapo tutawaona wachungaji na maaskofu wazinzi na wataonyeshwa wazi wazi wakifanya tendo la uzinzi na wenzao, ingawa tuliwajua kuwa watakatifu. Hatua zote za mtu za kumshawishi mwanamke wa mtu hadi kufanya naye uzinzi, vyote vitaonyeshwa. Jinsi unavyotamani wake au waume za watu vyote vitaonyeshwa kwa mfumo wa video na watu wote wataona uchafu huo. Lolote lile lililo ovu ambalo lilifanywa pasipo watu kujua, siku hiyo litajulikana. Hakika itakuwa ni aibu kubwa sana. Maneno yote mtu anayotamka yatawekwa wazi hapo na kwa mtu anayotamka yatawekwa wazi hapo na kwa kila neno mtu atahukumiwa (Mathayo 12:36-37). Mtu aliyekuwa anahudhuria mikutano ya injili bila kukata shauri kuokolewa atajiona picha yake akiwa katika mikutano hiyo na atajiona anasema “Siwezi kuokoka”. Wale walioshindwa kufanya hili na lile kwa visingizio kuwa ni wanajeshi, ni vijana wadogo n.k. wataona mashaidi wa Mungu waliofanya waliyokataa kuyafanya wakiwa na hali kama zao. Watakatifu watakuwepo kuona kila kitu na kuwa mashahidi wa Mungu (Waebrania 12:1; Mathayo 12:42; Malaki 3:18; Malaki 4: 1-2).

HUKUMU YA MWISHO.
   Watu watalia na kujitetea, wanaojiita manabii, wachungaji, mitume, wainjilisti watalia na kusema "Mimi nilifanya miujuza kwa jina lako" wengine watajitetea mimi nilitoa pepo kwa jina lako kadhalika wengine watajitetea "Mimi nilishuudia na kufuatilia" n.k, lakini Yesu atasema "Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu" (Mathayo 7:22-23). Kila mtu atatolewa hapo na kukamatwa kwa nguvu kisha atatupwa kwenye ziwa la moto (Ufunuo 20:15). Ziwa la moto ni tofauti na Jehanum ya moto (Kuzimu). Ziwa la moto kwa sasa halina mtu yeyote ndani yake, wa kwanza kutupwa humo watakuwa mnyama (Mpinga Kristo) na nabii wa uongo (Ufunuo 19:20). Kisha atafuata shetani (Ufunuo 20:10). Mateso ya ziwa la moto ni mazito zaidi kuliko Jehanamu, kama jinsi mtu anavyotolewa mahabusu na kutupwa gerezani. Mauti na Jehanamu (Kuzimu) ya sasa vyote pia vitatupwa katika ziwa la moto pamoja na wenye dhambi wote (Ufunuo 20:14-15, Ufunuo 21:8). Hapo itakuwa ni kwa heri ya kutoonana tena kwa wenye dhambi na watakatifu. Watumishi waliokuwa wanafundisha watu uongo kwa kusudi la kuwafariji watu watakumbuka na kujuta sana.

Wakati wa kwaheri ya kutoonana utakuwa katika kundi lipi?

MBINGU MPYA NA NCHI MPYA.
   Baada ya kujifunza masomo mengi kwa mfululizo kuhusu matukio ya mwisho wa dunia katika sura zilizopita, sasa katika sura hii tunakwenda kujifunza somo la mwisho kabisa katika mfululizo huu. Baada tu ya hukumu ya kiti cha enzi kikubwa cheupe, ndipo utakapofuata "MWISHO WA MIISHO YOTE" yaani kuharibiwa kwa dunia ya sasa na mbingu ya sasa ili tupate mbingu mpya na nchi mpya.

KUUNGUZWA NA KUFUMULIWA KWA MBINGU NA NCHI YA SASA.
   Mara tu baada ya hukumu ya kiti cha enzi kikubwa cheupe, ndipo utakapofuata mwisho wa miisho yote. Bwana wetu Yesu Kristo katika mafundisho yake alirudia tena na tena akieleza kwamba, mbingu na nchi za sasa zitapita. Katika kitabu chaMathayo 24:35 Biblia inasema, "Mbingu na nchi zitapita lakini maneno yangu hayatapita kamwe."Soma pia (Marko 13:31; Luka 21:33), hivyo basi wakati wa tukio hilo ndiyo huu. Pia tangu mapema kabisa Mungu wetu anatufundisha kwamba, mbingu na nchi za sasa zitachakaa na kuaribiwa na kama mavazi Mungu atazibadilisha kama tunavyoweza kusoma katika Zaburi 102: 25-26, "Hapo Mwanzo uliutia msingi wa nchi na mbingu ni kazi ya mikono yako. Hizi zitaharibika bali wewe utadumu Naam, hizi zitachakaa kama nguo, Na kama mavazi utazibadilisha, Nazo zitabadilika.” Pia tukiangalia katika kitabu cha Isaya 66:22 Biblia inasema, "Kama vile mbingu mpya na nchi mpya nitakazofanya zitakavyokaa mbele zangu asema BWANA, ndiyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa" (Isaya 65:17; 2Petro 3:13; Ufunuo 21:1-7). Mbingu mpya na nchi npya zitakuwa ni nzuri mno, hakuna mfano wake uliowahi kuwako au utakao kuwako. Ufundi wote wa uumbaji wa Mungu utaishia hapa.
   Miji yote ya dunia hii imebuniwa na kujengwa na wanadamu wenye upungufu wa ubunifu wa michoro, fedha, vifaa n.k; Mbingu mpya ni mji uliobuniwa na mbunifu mkuu, Mungu mwenyewe mwenye uwezo wote. Barabara zake sio lami bali dhahabu tupu.

SABABU ZA KUUNGUZWA NA KUFUMULIWA
KWA NCHI NA MBINGU ZA SASA.
  Nchi ya sasa yaani dunia hii au ulimwengu huu umechosha na kuchakaa mno baada ya kukaliwa na mamilioni ya wenye dhambi wanaofanya machukizo mbele za Mungu. Dunia hii imechakazwa kwa gharika wakati wa Nuhu na vita vya kila namna mpaka vita ile ya mwisho ya “Gogu na Magogu”. Miti yake mizuri imetumika kutengeneza sanamu za kuabudu, pia hata kumsulubisha mwana wa Mungu katika mti, kila namna ya matambiko na machukizo yanafanywa ulimwenguni. Damu za watu zimemwagika kwa wingi wake, tangu damu ile ya Habili. Dunia imejaa harufu ya damu na haifai kukaliwa tena. Pia mbingu hizi zilizo juu yetu yaani anga na sayari vyote vimejaa rekodi ya maneno ya wanadamu ya matusi na Lugha chafu za kumkufuru Mungu, vimejaa harufu ya uzinzi na usherati na za matendo ya sodoma. Mbingu hii ya kwanza na ya pili vyote havifai. Hata mbingu ya tatu yaani mbinguni aliko Mungu kwa sasa hakufai pia. Hapa ndipo mahali palipotunzwa kumbukumbu zote za dhambi za wanadamu katika vitabu vya hukumu kwa maelfu ya miaka. Rekodi au kumbukumbu hizi zimeifanya mbingu hii pia kuchukiza haifai nayo!. Kwa hiyo Mungu atazikamata nchi na mbingu hizi za sasa na kuziunguza na kila kitu ndani yake kitafumuliwa na kutoweka kama moshi kwa mshindo mkuu (2Petro 3:7; 2 Petro 3:10-12; Isaya 51:6). Mamilioni ya tani za gesi za oksijeni, haidrojeni, Acetylene n.k, zilizoko ulimwenguni na angani zitashika moto na madini ya kila namna yatayeyuka. Kila kitu, majengo miti yote na vinginevyo kama bahari n.k, vyote vitateketea na kuyeyushwa kabisa. Kisha vitatoweka kama moshi na kutoonekana kabisa.

MAISHA KATIKA MBINGU MPYA (YERUSALEMU MPYA).
   “Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari kama bibi harusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.” (Ufunuo 21:2). Yerusalemu inatokana na maneno ya kiebrania Y’ru-shalaim maana yake “Misingi ya amani”. Hivyo Y’r-shalaim maana yake “Kuwekwa misingi ya amani”. Pia Yerusalemu inatokana na maneno “Jireh-shalom”. Neno “Jire” maana yake “atawapa” na neno “Shalom” maana yake “Amani”. Hivyo “Jire-shalom” maana yake “Atawapa Amani”. Yerusalemu ya sasa, iliitwa hivyo kwa sababu ndipo ambapo Yesu Kristo alipokuja kutuwekea misingi ya Amani kwa kutupatanisha na Mungu kwa damu yake kisha akasema, “Amani nawaachieni, amani yangu nawapa” (Yohana 14:27). Baada ya mtu kuwa na amani ya Mungu ipitayo fahamu zote, hatimaye ataingia Yerusalemu mpya, mji uliojengwa juu ya misingi ya Amani.
   Katika kitabu cha Yohana 14:2, Yesu anasema katika mji huu kuna “makao” mengi. Neno la Kiyunani linalotafsiriwa hapa “Makao” ni “Mone” lenye tafsiri ya kiingereza “Mansion” katika Biblia ya tafsiri ya King James Version, “Mansion” ni jumba kubwa la kifahari (mansion house). Vivyohivyo mbinguni kuna majumba mengi ya kifahari. Kila mtu atakayeingia mbinguni atapewa “Kao” au jumba mojawapo la kifahari la kuishi.

MUUNDO WA MJI WA YERUSALEMU MPYA.
(Ufunuo 21:11-27).
  Mji huu una ukuta mkubwa, mrefu wenye milango kumi na mbili (12) na majina yameandikwa ambayo ni majina ya kabila kumi na mbili za Waisraeli. Upande wa mashariki milango mitatu, upande wa magharibi milango mitatu, upande wa kasikazini milango mitatu na upande wa kusini milango mitatu. Na ile milango kumi na miwili ni Lulu kumi na mbili, kila mlango ni lulu moja. Madini ya Lulu yanapatikana duniani yana umbo dogo sana kama mawe madogo tu na wala siyo ukubwa wa milango mikubwa kama hii. Lulu ni aina fulani ya madini ya thamani kubwa sana ambayo hupatikana katika wanyama fulani wa baharini wenye gamba au kobe aina ya chaza (Oyster). Thamani ya Lulu moja ni karibu dola za kimarekani laki nne ($ 400,000) ambazo ni sawa na Tsh. 270,000,000/=
  Ukuta wa mji huu una misingi kumi na mbili (12) juu ya misingi hiyo yameandikwa majina ya wale mitume kumi na mbili wa Yesu. Mji huu marefu yake, mapana na kwenda juu ni sawasawa yaani maili 1,500. Ukuta wake ni dhiraa 144 sawa na futi 300. kuta zake zimejengwa na madini ya ajabu!. Dhahabu safi mfano wa kioo safi. Msingi wa kwanza umejengwa kwa Yaspi, ambayo ni madini yanayonga’ara sana yenye rangi ya kijani iliyochanganyika na bluu. Msingi wa pili umejengwa kwa yakuti samawi, haya ni mawe ya bluu, mazuri sana yenye ugumu unaofanana na madini ya almasi. Msingi wa tatu umejengwa kwa madini ya kalkedoni, haya ni aina ya madini mazuri sana yenye rangi aina nne mbalimbali, yaani nyekundu iliyochanganyika na njano,hudhurugi (Brown) iliyochanganyika na nyeusi, bluu iliyochanganyika na nyeupe, na rangi ya maziwa. Msingi wa nne ni zumaridi, haya ni madini yenye rangi ya kijani. Msingi wa tano umejengwa kwa madini ya Sardoniki, madini yenye rangi ya bluu, nyeupe na nyekundu. Msingi wa sita umejengwa kwa akiki madini yenye rangi ya damu. Na msingi wa saba umejengwa kwa madini ya Krisolitho, haya ni madini yaliyo kama dhahabu ila yana rangi ya kijani iliyochanyika na njano, msingi wa nane umejengwa kwa zabarajadi, haya ni madini maangavu (transparent) yenye rangi ya bluu iliyochanganyika na kijani. Msingi wa tisa umejengwa kwa Yakuti ya manjano, ni madini ya njano iliyochanganyika na kijani, msingi wa kumi umejengwa kwa madini ya Krisopraso, haya ni madini yenye rangi tatu pamoja yaani njano, kijani na bluu. Msingi wa kumi na moja umejengwa na madini yaHiakintho.Na msingi wa kumi na mbili umejengwa kwa madini ya amethisto,haya ni madini yenye rangi ya zambarau, yenye bluu na wekundu ndani yake. Barabara za mji huu siyo lami bali nidhahabu safi kama kioo.
    Mji hauhitaji jua wala mwezi kuangaza kwani utukufu wa Yesu unatosha! Hakuna usiku humo! Maisha yatakuwa ya kupumzika (Ufunuo 14:13), furaha tele wala hakuna maombolezo wala kilio (Ufunuo 21:4), katika mji huo kutakuwa na kumwabudu na kumsifu Mungu tu (Ufunuo 19:1; Ufunuo 7:9-12; Ufunuo 5:11-14), Leo tunafahamu kwa sehemu yale tu tuliyofunuliwa lakini tukifika mbinguni tutajua yote (Kumbukumbu 29:29; 1 Wakorintho 13:12). Pia mavazi meupe ya wale waliopo mbinguni hubadilikadilika rangi mara kwa mara kutokana na rangi ya mwanga inayoakisi kutoka katika majengo,hivyo kufanya watu kupendeza sana.Chemichemi za maji na mito ya maji ya uzima, inauzunguka mji.Pia mbinguni kuna kula na kunywa, hakuna mauti wala maumivu au taabu(Luka 22:14-16,Luka 22:29-30; Ufunuo 2:17;Ufunuo 21:4-5;Ufunuo 14:13), Kuna kuimba nyimbo za sifa na vinanda (Ufunuo 14:2-3;Ufunuo 15:2-4), Pia ufahamu wetu utaongezeka(1 Wakorintho 13:12).Kwa ujumla mbinguni kuna mengi yasiyoweza kutamkika kwa lugha za duniani (2 Wakorintho 12:4).Majibu mengine ya maswali yako utayapata ukifika huko mbinguni.


Yeye ashindaye atayarithi haya (Ufunuo 21:7).

NA: DR. GODWIN GUNEWE


Share:

USCF-SJUT NEWS

Designed by Joel Elphas @ 2015. Powered by Blogger.

Recent Posts