MATUKIO YA KIBIBLIA YA
NYAKATI ZA MWISHO
NA: DR. GODWIN GUNEWE
KUTIMIA KWA UNABII WA NYAKATI ZA MWISHO
Dalili ya
Mvua ni mawingu, hivyo kwa mtu mwenye busara, aliyeanika nguo zake nje anapoona
tu mawingu yametanda kila mahali, anajua kwamba mvua wakati wowote inaweza
kunyesha, na hakika atafanya haraka kwenda kuzianua nguo hizo. Vivyo hivyo, Yesu
Kristo anatuonya katika maandiko juu ya kuzitambua ishara za zama hizi yaani
ishara za nyakati hizi za mwisho, na kujua yale yanayokuja hivi karibuni ili
tujiandae vema kuyakabili. Biblia inasema katika Mathayo 16:2-3 “Akajibu,
akawaambia kukiwa jioni, mwasema, kutakuwa na kianga; kwa
maana mbingu ni nyekundu na asubuhi, mwasema, Leo kutakuwa na dhoruba; kwa
maana mbingu ni nyekundu, tena kumetanda. Enyi wanafiki, mwajua kuutambua uso
wa mbingu: lakini Je? Ishara za zama hizi hamwezi kuzitambua?”
DALILI ZA MWISHO WA DUNIA.
Kila kilicho na
mwanzo hakikosi kuwa na mwisho, na mwisho wa dunia umekaribia sana. Dalili
mbalimbali za mwisho wa dunia, zinatajwa katika sehemu mbalimbali katika
Biblia.kwa mfano katika Mathayo 24:3-14 Biblia inasema, “Hata
alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake
wakamwendea kwa faragha, wakasema, Tuambie, mambo hayo
yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho
wa dunia? Yesu kajibu, akawaambia, Angalieni mtu asiwadanganye Kwa sababu wengi
watakuja Kwa jina langu, wakisema, Mimi ni kristo; nao watadanganya wengi. Nanyi
mtasikia habari za vita na matetesi ya vita; angalieni, msitishwe; maana hayo hayana
budi kutukia; lakini ule mwisho bado. Kwa maana taifa litaondoka kupigana na
taifa, ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na njaa, matetemeko ya ardhi mahali
mahali. Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu. Wakati huo watawasaliti ninyi mpate
dhiki, nao wawaua; nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya
jina langu. Ndipo wengi watakapojikwaa nao watasalitiana, na kuchukiana. Na
manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi. Na kwa sababu ya
kuongezaka maasi mengi upendo wa wengi utapoa. Lakini mwenye kuvumilia hata
mwisho, ndiye atakayeokoka. Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu
wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.”
Pia tukiangalia katika kitabu cha 1 Timotheo 4: 1-5 Biblia
inasema “Basi roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho
wengine watajitenga na Imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya
mashetani; kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao
wenyewe; wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu
aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua
hiyo kweli.” Kadhalika tukiangalia katika kitabu cha2 Timotheo
3: 1-5 Biblia inasema, “Lakini ufahamu neno hili yakuwa siku za
mwisho kutakuwako nyakati za hatari. Maana watu watakuwa wenye kujipenda
wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi,wenye kutukana,
wasiotii wazazi wao, wasio taka kufanya suluhu, wasio na shukrani,wasio safi,
wasio wapenda wa kwao, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema,
wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda mungu, wenye
mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake, hao nao ujiepusha nao.” Dalili
zote hizi zimekwishatimia, na zinazidi kuwa dhahiri mbele ya uso wa dunia kila
iitwapo leo. Ni vizuri pia kufahamu kwamba moja ya utendakazi wa nabii wa
uongo, ni ishara na ajabu za uongo, kimsingi dalili hii iko wazi zaidi, kwani
ulimwengu wote sasa, umetekwa na Ishara na miujiza ya uongo kutoka kwa watenda
kazi wa shetani, ingawa ipo miujiza ya kweli inayotoka kwa Mungu.
MAKRISTO WA UONGO.
Katika
kitabu cha Marko 13:22-23 Biblia inasema, “Kwa
maana wataondoka Makristo wa uongo, watatoa Ishara na maajabu, wapate kuwadanganya,
kama yamkini hata hao wateule.Bali ninyi jihadhalini; nimekwisha kuwaonya
yote mbele.” Makristo wengi sana wa uongo wametokea hapa duniani
tangu unabii huu ulipotolewa.Na kila mmoja amekuja kwa sura na mtazamo tofauti
kabisa na jinsi maandiko yanavyozungumza juu ya Kristo wa kweli.Na hii
ilimthibitishia kila mtu kuwa hao ni makristo wa uongo, kwa mfano nchi kama
Zambia, Kongo, Kenya, Tanzania na nchi mbalimbali za jirani, walikwishawahi
kutokea watu waliojiita hao ndiye kristo lakini baadaye waliishia kuaibika. Kwa
ujumla nchi nyingi sana duniani wameibuka makristo wengi sana wa uongo na
wamedanganya wengi. Asilimia kubwa ya wateule katika kanisa la leo, wapo kwenye
hatari kubwa sana ya kuachwa wakati wa unyakuo wa watakatifu, na hii ni kutokana
na wakristo hao kupenda kufuata makanisa yanayohubiri miujiza zaidi kuliko
kufundisha neno la Mungu na hivyo kuwafanya wawe mwilini sana. Pia mafundisho
ya Mashetani yamekuwa kivutio kikubwa sana kwa wateule wengi katika kanisa la
leo, hivyo kupelekea maasi kuongezeka sana yamkini hata nyumbani mwa Mungu, kwa
kuwa neno halisi la Mungu limekuwa adimu sana kwenye makanisa hayo.
WACHAFU WATAZIDI KUWA WACHAFU NA MAASI KUONGEZEKA.
(Ufunuo 22:11, Mathayo 24:12).
Yapo matukio
mengi sana ya aibu na ya kutisha, yanayotokea kila siku katika dunia yetu, na
matukio haya yanadhihirisha wazi kutimia kwa unabii unaosema“Wachafu watazidi
kuwa wachafu”. Uchafu unaotajwa hapa ni ulawiti.Katika nchi yetu,
pamoja na sheria kali ya kujamiiana, ambayo inawafanya watu wanao najisi watoto
wadogo au wabakaji na walawiti, kupewa adhabu ya kifungo cha maisha; bado
vitendo hivi vinaongezeka kwa kasi sana kama vile watu hawajali! Karibu kila
siku tunasikia habari hizi katika vyombo vya habari. Wengine wanaripotiwa
kulawiti watoto wadogo waliowazaa wenyewe! Wengine wanalawiti vikongwe! Wengine
wanalawiti wanyama.Wengine wanawabaka mama zao! Mtu mmoja anaripotiwa kulawiti
watoto wadogo watano wa shule ya msingi zamu kwa zamu! Pia kiongozi mmoja wa
dhehebu la kikristo anaripotiwa kumlawiti mtoto wa kiume wakiwa ndani ya gari
maeneo ya chuo kikuu cha Dar -es- salaam! Waziri mkuu mmoja wa nchi moja ya
Ulaya anataka ushoga uwe halali kupitia bunge la nchi yake. Maaskofu wa dhehebu
moja kubwa la kikristo, hivi karibuni wamepiga kampeni ya kutaka ushoga
uhalalishwe! Hakika wachafu watazidi kuwa wachafu! Katika nchi ya Tanzania
kumeripotiwa matukio mengi sana ya mauaji ya vikongwe na maalbino. Wanaume
wengi hapa duniani wamelipotiwa kuwaacha wake zao, kwa sababu ya ulawiti!. Huko
Marekani na ulaya ndoa za wanaume kwa wanaume (mashoga) na ndoa za wanawake kwa
wanawake (wasagaji) zinazidi kuongezeka kila siku. Mchungaji mmoja wa dhehebu
la kikristo hapa nchini Tanzania anaripotiwa kushiriki biashara haramu ya
viungo vya wanadamu (Albino). Miezi michache iliyopita viongozi wa dhehebu
kubwa la kikristo huko nchini Marekani wameripotiwa kuwalawiti watoto wadogo!
Hata hivyo makanisa mengi, katika nyakati za leo, yanahusianishwa na nguvu za
kishetani na hata kupelekea kupoteza wateule wengi. Katika kitabu chake Iyke
Nathan Uzorma Kiitwacho Mkuu wa wachawi sasa ampokea Kristo Ukurasa
wa 38 na 39 anataja kwa uwazi kabisa kuwa makanisa yafuatayo kuwa ni makanisa
ya shetani:- Kanisa la shetani San Francisco nchini Marekani
lililoanzishwa mwaka 1996 na kuhani mkuu wa shetani, aliyeitwa Anton
Laveyambaye pia ndiye mwandishi wa biblia ya shetani, kadhalika kanisa
la Wicca la California Marekani lililoanzishwa na Askofu Mkuu aitwaye Frost ambaye
pia ni mwandishi wa kitabu kiitwacho “Sanaa ya Wachawi”. Yapo
makundi mengi sana ya Imani potofu (Cults) hapa ulimwenguni ambayo yanatenda
kazi karibu kila nchi duniani ili kuweza kutimiza kusudi la kuwapoteza wateule.
Ni vizuri kuwa makini na mwangalifu sana kabla ya kujiunga na kanisa lolote, ni
lazima kumuomba Roho Mtakatifu akuongoze ili usije ukaingia kwenye mtego wa
shetani na hatimaye ukajikuta unaitazamia jehanum ya moto. Na wachungaji ambao
wanapenda urahisi na kutaka kujiunga kwenye makanisa yenye pesa, kwa kudhani
kuwa maisha yao na huduma zao zitainuliwa, tafadhali nawaomba muwe makini sana
la sivyo utajikuta utumishi wako uliojengwa kwa muda wa miaka mingi unabomoka
kwa siku moja. Ni bora ukubali kuteseka, na Mungu wetu ni mwaminifu atakuinua;
kuliko kujiunga na kanisa lenye pesa ambalo limeweka mikataba na shetani.
Ukweli ni kwamba, wapo watu wengi sana ambao wanafanya kazi kama mitume,
wachungaji, manabii, wainjilisti, na walimu lakini kumbe ni watumishi wa
shetani. Katika neno lake Bwana Yesu, anatusisitizia na kutuonya kwamba, Baadhi
ya watumishi wa Mungu tunaowaona ni mateka wa shetani na wachawi ambao
wanafanya kazi hata katika makanisa mbalimbali ya Kipentekoste, Unabii huu
ulitolewa na mtumishi wa Mungu mtume Paulo, na hakika kwa sasa unabii huu upo
dhahiri kabisa, katika kitabu cha 2 Wakorintho 11: 13-15 Biblia
inasema, “ Maana watu hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa
hila,wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo wala si ajabu maana
shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa Malaika wa Nuru.
Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano
wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.”
Kwa ujumla, vitabu vifuatavyo vya Biblia vinaweka wazi, unabii wa dalili za
mwisho wa dunia. ( Danieli 12:4, Mathayo 24:3-14, Marko 13:3-27, Luka
21:7-32, 1 Timotheo 4:1-5, 2 Timotheo 3:1-5, Ufunuo 22:6-7).
Orodha ya unabii wa matukio ya nyakati za mwisho.
1 Maarifa
kuongezeka (Daniel 12:4).
2 Wengi
kuja kwa jina la Kristo na kudanganya wengi (Mathayo 24: 4, Marko13:5).
3 Habari na
matetesi ya vita (Mathayo 24:6).
4 Taifa kupigana
na taifa, ufalme na ufalme, njaa na metetemeko ya ardhi
(Mathayo
24:7, Marko 13:8).
5. Kutokea
kwa manabii wa uongo na kudanganya wengi ( Mathayo 24:11,
Marko
13:22).
6. Kuongezeka
kwa maasi na upendo wa watu kupoa ( Mathayo 24;12)
7. Wengi
watajitenga na Imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na
mafundisho
ya mashetani (1Timotheo 4:1)
8. Watu kuzuiliwa kuoa na
watu kuamuriwa wajiepushe na vyakula ambavyo mungu aliviumba (1
Timotheo 4:3)
9. Watu
kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye
kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi
(2 Timotheo 3:2, Marko
13:12).
10. Wasiowapenda wakwao, wasiotaka
kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, wasaliti,
wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu (2
Timotheo 3:3-4).
11. Wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake
mola. (2 Timotheo 3:5).
12. Wachafu kuwa wachafu (Ufunuo 22:11).
13. Magojwa ya kutisha yasiyo na dawa (pestilences)
Mathayo 24:7(King James version).
14. Wengi watajikwaa na kusalitiana, na kuchukiana(Mathayo
24:10)
Je unaijua dalili ya mwisho kabisa ya mwisho wa dunia?
Ni jambo la
kusikitisha sana kuona mkristo aliyesimama vema kiroho anarudi nyuma katika
nyakati hizi za mwisho. Pia ni jambo linaloumiza sana kuona mtu aliyeokolewa
kwa neema, anafanya mchezo na dhambi katika nyakati hizi za hatari. Ndugu mpenzi
msomaji, ni vizuri kutambua kwamba, Yesu Kristo atarudi siku yoyote kuanzia
sasa. Kama wewe siyo mwana wa Ufalme, ni ngumu sana kulielewa hili, kama
ilivyokuwa Nyakati za Nuhu.
Pamoja na dalili
nyingi kutajwa katika vitabu mbalimbali, Bwana wetu na Mungu wetu Yesu Kristo
alitupa dalili moja ambayo ndiyo inayoashiria kufika mwisho kabisa kwa dunia;
dalili hii ni Injili kuhubiriwa ulimwenguni mwote kuwa ushuhuda kwa mataifa
yote. Katika kitabu cha Mathayo 24:14 Biblia inasema,
“Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda
kwa mataifa yote, hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.”
Ni muhimu kufahamu
kwamba madhehebu karibu yote yanahubiri Injili ulimwenguni,
yakishirikiana na stesheni karibu zote za Radio za kikristo ulimwenguni,pia stesheni
karibu zote duniani za televisheni kama vile TBN na JCTV zilizopo Marekani,
Mashirika karibu yote ulimwenguni ya uchapaji maandiko ya kikristo, wote kwa
pamoja kwa nia moja na moyo mmoja, waliungana kama shirika liitwalo “AD
2000 and BEYOND MOVEMENT” wakiwa na lengo la kuhakikisha kwamba
ulimwengu wote unahubiriwa Injili kufikia Desemba 31, 2000. Shirika
hili liliongozwa na Mmarekani mmoja aitwaye Louis Bush na
kuungwa mkono na wahubiri wote duniani kama vile Bill Graham wa Marekani, Dr.
David Yongcho wa Korea na wengine wengi. Kadhalika wafanya biashara wakubwa
duniani, makampuni ya uchapaji maandiko matakatifu, waigizaji filamu za neno la
Mungu, wanasayansi wakubwa duniani na wakristo wengi walio na majina makubwa
hapa duniani wote waliweka nguvu zao katika kutimiza maadhimio ya shirika
hili.Wote hawa walikaa kwa pamoja nchini Afrika kusini, Pretoria mwaka 1997.
Kumekuwa na makusanyiko kama haya tangu mwaka 1974, na lengo kuu la makusanyiko
haya ni kupanga mikakati ya kuhubiri injili dunia nzima mpaka kufikia mwaka
2000. Wako wataalamu wa mambo ya takwimu ambao walifanya utafiti na kuweza
kuigawa dunia katika makundi ya kijamii elfu kumi na mbili (12,000). Na utafiti
huo ulionyesha kwamba mpaka mwaka 1997 makundi elfu kumi (10,000)
yalikwishafikiwa na injili. Kwa hiyo nguvu zote zilielekezwa kwa makundi elfu
mbili (2,000) yaliyobaki.Kazi hii iliyochochewa na maombi ya watu zaidi ya milioni
hamsini kutoka katika makanisa mbalimbali duniani wanaoomba masaa 24
kila siku, kuhakikisha lengo hili linatimia; na pia ilichochewa na matumizi ya
tekinologia ya kisasa ya kuhubiri Injili kama “Internet” “satellite” n.k
quicken
Kwa kutumia
teknologia ya kisasa, Injili inahubiriwa kwa kasi ya ajabu. Kwa mfano kwa
kutumia “satellite” Mwinjilisti Mmoja anayeitwa Billy
Graham, tarehe 14 Aprili, 1996, alihubiri
Injili na nchi zote ulimwenguni waliweza kusikia kwa wakati huohuo, wakati yeye
akiwa marekani. Hivi leo ulimwenguni, stesheni za Radio na Televisheni za
kikristo zipo katika kila mikoa na majimbo, na hakika nyakati hizi hakuna
ambaye anayeweza kujitetea kwa kusema kwamba, hajasikia habari za Yesu
Kristo.Kwenye kikao cha Afrika ya kusini watumishi wa Mungu walikubaliana kwamba
baada tu ya Krismasi ya mwaka 2000, wote wangekusanyika pale Yerusalemu ili
kwenda kutoa ripoti kwa Bwana Yesu kwamba kazi aliowatuma ya kuhubiri injili
ulimwenguni kote wameimaliza, na mkutano huo ulipewa jila la Jesus
celebration.
Kwa upande mwingine,
ningeweza kusema kwamba, sasa ulimwengu wote umesikia habari za Yesu, na
watumishi wa Mungu wanazidi kukaza mwendo kuhubiri Injili kwa nguvu zaidi. Ni
kweli kabisa hakuna mtu aijuaye siku wala saa ya kurudi kwa Yesu Kristo; lakini
yote haya ni mawingu, ambayo ni dalili ya Mvua! Maana yake ni kwamba tupo
ukingoni kabisa na wakati wowote ule mwisho wa dunia unakuja! Hivyo jiandae
kulia kama bado mpaka leo unamkataa Yesu. Kadhalika na kwa wewe uliyempokea
Yesu na kuishi maisha matakatifu jiandae kucheka maana yeye ajaye atakuja wala
hatakawia (Waebrania 10:37).
KUONGEZEKA KWA KASI YA UTENDAKAZI WA SHETANI DUNIANI.
Bwana
Yesu alituonya kuwa,”Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi
ameshuka kwenu mwenye ghadabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu”
(Ufunuo 12:12). Shetani, ambaye ana muda mfupi sana wa kutawala na
kuwalaghai watu, kwa hiyo, nyakati hizi anatenda kazi kwa kasi isiyo ya
kawaida, ili tu kutekeleza uharibifu wake kwa kile ambacho Mungu amekiumba.
Maasi na uharibifu mkubwa unaofanywa duniani, ni miongoni mwa mipango wa
shetani katika kutimiza unabii wa nyakati za mwisho. Siku hizi utaona kuwa,
kila mahali, na wakati wote, kuna utendaji mkubwa sana wa kazi za shetani.
Yafuatayo ni baadhi tu ya mambo ambayo ni utendaji kazi wa shetani;
1. KUKITHILI KWA NGONO DUNIANI.
Nguvu ya
ngono ni moja ya silaha kubwa sana ambayo shetani anaitumia kumteka na
kumtawala mtu kimawazo, kimaneno na kimatendo. Katika nyakati hizi za mwisho,
nguvu za giza hushambulia sana katika eneo hili la tamaa ya mwili. Kumefanyika
mikakati na mipango, katika ulimwengu wa roho yaani ulimwengu wa mapepo, ili
kuwafanya wanadamu wote wapende sana ngono. Roho chafu za ngono, zimemwagwa kwa
wingi duniani ili kuwafanya wanadamu wakati wote watafakari ngono mchana na usiku.
Kwa kuliboresha hili, shetani amefanikiwa kuharibu ndoa nyingi duniani ili
awaweke wanandoa katika himaya ya uzinzi, akijua hakuna mzinzi atakayeurithi
ufalme wa Mungu. Katika kitabu chake Iyke Nathan kinachoitwa “Mkuu
wa wachawi sasa ampokea Kristo” ukurasa wa 25, kinasema kwamba mwaka 1986
mwezi wa saba, walitumwa viumbe 30,000,000 (Milioni thelathini) kutoka chini ya
bahari kuja duniani wakiwa na maumbo ya wasichana wazuri sana, na walianza
kufanya kazi kama Malaya katika miji mbalimbali maarufu ya mataifa hapa
duniani, wasichana hao kimsingi ni mapepo, waliletwa duniani kuongeza idadi ya
wenzao ambayo kazi yao ilikuwa inaisha mwaka 1997 mwezi wa saba. Lengo la
viumbe hao kuja duniani ni kuongeza nguvu ya zinaa.
2. KUKITHILI KWA UCHAWI DUNIANI.
Moja ya taaluma
iliyo juu sana hapa ulimwenguni ambayo shetani anaitumia sana katika kuwapoteza
watu ni taaluma ya uchawi.Wapo wachungaji na manabii wengi katika kanisa la leo
wanaojihusisha na uchawi ili kuwa na kundi kubwa katika makanisa wanayoyachunga.Kwa
ujumla kuna aina nyingi sana za uchawi na ushirikina ambao watu wengi wamebobea
ili kuweza kutekeleza utumishi na utii wao kwa shetani.
Ukweli ni kwamba
uharibifu mkubwa duniani unafanywa kupitia uchawi. Matukio mbalimbali ya
kinyama na ya kutisha yanafanywa hapa duniani kwa kutumia uchawi. Yote haya ni
mipango ya shetani ya kufanya uhalifu ili kutimiza unabii, hususani katika
nyakati hizi za mwisho; Mfano wa matukio yanayotokana na uchawi ni:-
1 Ajali
mbalimbali za ndege, meli, treni, magari nk.
2 Uharibifu
wa mimba kwa wanawake.
3 Magonjwa
ya kutisha na yasiyopona.
4 Vifo
vya watu wengi, hasa vifo vya kutatanisha.
5 Mafarakano
ya ndoa.
6 Kupotea
kwa watu ghafla kwa njia ya uchawi.
7 Kuwapumbaza
wateule wasisimame kwenye wokovu.
8 Kuleta
hali ngumu ya kimaisha kwa watoto wa Mungu ili wakate tamaa.
9 Kupunguza
kasi ya kuoa na kuolewa ili kuchochea uasherati makanisani.
10 Kuwapumbaza
watumishi wa Mungu wasiwe na macho ya rohoni.
11 Kuwafanya
watoto wa Mungu kuipenda dunia, hivyo kuwa kama makahaba.
12 Kuwafanya watumishi wa Mungu kupenda
fedha hivyo kushindwa kukemea maovu ndani ya kanisa, hatimaye kanisa kupoteza
nguvu ya Mungu.
13 Kuwafanya watoto wa
Mungu waichukie kweli ya neno la Mungu na kupenda uongo.
14 Kuwafanya wateule wawe
mateka wa nguvu za giza na hatimaye kuondoa nguvu za
mungu kanisani.
Kwa
ujumla, Lengo kuu la jitihada na mikakati yote hii inayofanywa na shetani, ni
kuhakikisha kuwa nyakati hizi za mwisho anapeleka wengi sana Jehanamu ya moto,
hususani wateule wa Mungu.
TUKIO LA KUTISHA LINALOKUJA HIVI KARIBUNI.
Watu wengi
sana, wamekuwa wakijiuliza, kuwa mwisho wa dunia utakuwaje? Na kwa kukosa
ufahamu wa kweli, baadhi ya watu kupitia madhehebu yao, wamekuwa wakijitungia
hadithi za uongo juu ya mwisho wa dunia utakavyokuwa (2 Petro1:16; 2
Timotheo 4:4; 1 Timotheo 1:4).
Kuna
mfululizo wa matukio kadhaa ya mwisho wa dunia, lakini kabla ya kuangalia
mfululizo wa matukio hayo, kuna tukio zito, na la kutisha, ambalo litatokea
ulimwenguni wakati wowote kuanzia sasa. Na hii ni kutokana na dalili ya mwisho
kabisa ya mwisho wa dunia kutimia, kama tulivyo kwisha kuona katika sura
iliyopita. Tukio hili linaitwa “Kunyakuliwa kwa watu waliookoka” yaanikanisa.
Katika 1 Wathesolanike 4:15-17 Biblia inasema, “Kwa kuwa
twawambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakao salia hata
wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala
mauti. Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na
sauti ya Malaika mkuu, na parapanda ya Mungu nao walio kufa katika Kristo,
watafufuliwa kwanza kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao
katika mawingu, ili tumlaki bwana hewani na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana
milele.”
‘Kunyakuliwa’
ni tendo la kuchukuliwa kwa kitu ghafla, kwa kasi kubwa na kuondolewa pale
kilipokuwa; katika hali ya kuwaacha watu wamepigwa butwaa, kwa jinsi
wasivyoweza kukipata kitu hicho tena. Kwa hiyo, watu waliookoka muda si mrefu
ujao, watanyakuliwa kwa jinsi hii na Bwana Yesu Kristo. Yesu anakuja kufanya
kazi hii, haraka na wala hatokawia (Waebrania 10:37).
Siku ya
kunyakuliwa kwa watu waliookoka sehemu nyingine duniani itakuwa usiku, sehemu
nyingine itakuwa mchana, maana majira duniani yanatofautiana. Jua likitua
sehemu moja duniani, linachomoza sehemu nyingine ya dunia. Wakati wa
kunyakuliwa kwa watu waliookoka hapa Tanzania, hatufahamu itakuwa mchana au
usiku, maana siku ile inakuja kama mwizi au kama uchungu umjiavyo mwenye mimba
(1 Wathesolanike 5:1-3). Ikiwa ni mchana watu wote waliokufa tangu
zamani wakiwa katika hali ya utakatifu na wakawa wamekwenda mbinguni,
watafufuliwa na kutokea tena duniani, na kila mmoja atawaona. Watakuwepo watu
wengi kwa ghafla, mitaani kila mahali. Hata kama kwenye makaburi ya zamani
ambapo siku hizi kuna jengo la ofisi, watatokea humo humo ofisini na kuujaza
uso wa dunia. Dakika moja kufumba na kufumbua, watu waliookoka ambao wako hai
duniani nao wataungana pamoja nao, na wote kwa pamoja watabadilishwa miili yao
na kuvaa miili ya utukufu yaani miili isiyoharibika. Kadhalika katika kitabu
cha 1 Wakorintho 15:52-53 Bibilia inasema,” Kwa
dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana
parapanda Italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.
Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa.”
Katika wale
watakaokuwako duniani, baada tu ya parapanda kulia, wale waliookoka watatwaliwa
na kwenda angani kwenye harusi ya mwana kondoo ambayo, itafanyika kwa muda wa
miaka saba, na wale watakaoachwa duniani, watakuwa katika mateso ya dhiki kuu
muda wa miaka saba. Kadhalika na watakatifu waliofufuliwa, watakwenda angani
kwenye harusi ya mwanakondoo, wakati wale waliokufa katika hali ya dhambi
wataendelea kubaki kwenye mateso ya Jehanamu ya moto mpaka wakati wa ufufuo wa
pili.
RIPOTI YA KUTOWEKA KWA WATU DUNIANI.
Tukio la unyakuo,
litawachanganya akili watu wote duniani yaani wale watakaobaki. Watakuwepo
wawili wakilima shambani, mmoja aliyeokoka atanyakuliwa, naye yule ambaye
hajaokoka ataachwa, na hakika atashtushwa sana kwa kitendo cha ghafla cha
kutoweka kwa mwenzake. Pia watakuwepo wawili wakitwanga nafaka, na ghafla mmoja
aliyeookoka atanyakuliwa na wa pili ambaye hajaokoka ataachwa. Tunasoma katika Mathayo
24:40-41 Biblia inasema “Wakati ule watu wawili watakuwa
kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa; wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja
atwaliwa; mmoja aachwa.”
Ikiwa tukio
hili litakuwa usiku na katika familia fulani kuna mume hajaokoka na mke
ameokoka, watoto wakubwa hawajaokoka na kadhalika katika familia hiyo wako
watoto wadogo wasiojua mema na mabaya; mume huyo mlevi amayempiga vita mkewe
kwa sababu ya wokovu, ataamka asubuhi na kushangaa kuona mkewe kitandani na
watoto wadogo wasiojua mema na mabaya hawapo. Atawauliza watoto wakubwa, “Mama
yenu yuko wapi?” watajibu “Hatujui”, atatoka nje na
kwenda kuuliza. Wakati kuohuo kila mahali itaripotiwa Polisi, kwamba wako watu
waliotoweka usiku, pamoja na watoto wote wadogo wasiojua mema na mabaya. Pia
kutakuwepo na Polisi waliotwaliwa. Baada ya uchunguzi duniani kote, waandishi
wa habari ambao walioachwa watatoa ripoti katika magazeti kama ifuatavyo, “Mamilioni
ya watu kote duniani wameripotiwa kutoweka usiku wa jana. Uchunguzi umeonyesha
kwamba waliotoweka ni walokole ambao wamekuwa wakidhaniwa kuwa
wamechanganyikiwa au kupotea. Taarifa zaidi zinaeleza kwamba watoto wachanga
wote pia wametoweka. Taarifa za uchunguzi zinaonyesha kwamba waliotoweka
wamenyakuliwa kwenda kumlaki Yesu mawinguni kama walokole walivyokuwa
wakihubiri!”
JINSI UNYAKUO WA WALOKOLE (KANISA) UTAKAVYOKUWA.
Hawa
watakaotwaliwa, wataungana na wale waliofufuliwa na kisha wote kwa pamoja,
watavutwa kama sumaku inavyovuta chuma, na mvuto huu utatoka kwa Yesu mwenyewe
atakayekuwa mawinguni. Yeye hataonekana kwa wale watakao kuwapo duniani, na kwa
kuwa Yesu ni mtakatifu kadhalika watakaovutwa ni watakatifu tu, na siyo wenye
dhambi. Sumaku itawavuta waliookoka tu, kama jinsi sumaku inavyovuta vyuma peke
yake na kuacha mchanga au udongo! Na ndiyo maana Bwana Yesu anatusisitiza
katika Mathayo 5:48 kwamba tuwe wakamilifu kama Baba yetu
alivyo mkamilifu. Itakuwa kama kuku na ndege wanaposhtushwa na kishindo, ingawa
wote wana mabawa, lakini ndege hupaa juu angani na kuku akijaribu kupaa juu
huishia kwenye kichanja cha kuanikia vyombo!.
Nguvu ya
kiungu kutoka kwa Yesu akiwa mawinguni itawafanya waliookoka kisawasawa
kuishinda nguvu ya uvutano ya dunia (Gravitational force) hivyo watapaa
kama tai kwenda kumlaki Bwana Yesu mawinguni huku wakiimba wimbo wa Musa na
wimbo wa Mwana kondoo (Ufunuo 15:3-4), huo ndiyo utakuwa mwisho wa
huzuni na mateso kwa watakatifu watakaokuwapo hapa duniani.
Baada ya
wenye dhambi kuachwa, ndipo kitakapokuwapo kilio na kusaga meno hapa duniani.
Itafuata dhiki kubwa ya miaka saba; ambayo namna yake haijawahi kutokea tangia
misingi ya dunia kuwekwa. Biblia inasema katika Mathayo 24:21, “Kwa
kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa ambayo haijatokea namna yake tangu
mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe.”
Wenye dhambi
watateswa kwa namna ya kutisha. Watu watatamani kufa kutokana na mateso na
maumivu, lakini mauti ya namna hiyo itakuwa imeondolewa (Ufunuo 9:2-6).
Wataiambia milima na miamba, tuangukieni, watamwomba Mungu awahurumie, lakini
huruma na uvumilivu wake Mungu utakuwa umekoma (Ufunuo 6:15-17, Isaya
26:16-18). Wale walionyakuliwa, huko juu watakuwa katika karamu ya arusi ya
Mwanakondoo baada ya kupewa kila mtu taji zake (Ufunuo 19:5-9; 2Wakorintho
5:8-10).
MIFANO YA KIBLIA KAMA KIVULI CHA KUNYAKULIWA KWA
WALIOOKOKA (KANISA).
Mungu katika
hekima yake iliyo juu sana, hakuacha kutupa mifano ya yale yatakayotokea
mbeleni ili tuyaelewe vema kabla ya dhiki kuu, mifano ifuatayo inatupa picha
halisi ya unyakuo itakavyokuwa;
1.Nuhu na wanawe saba, walikwenda safinani kwanza, kabla ya
Mungu kuleta gharika juu ya wenye dhambi, na wakati wote safina ilikuwa juu,
gharika chini (Mwanzo 7:11-18).
2.Lutu alishikwa mkono na kutolewa nje ya mji wa Sodoma na
Gomora kabla Bwana kuleta uhalibifu juu ya nchi (Mwanzo 19:12-16, Mwanzo
19:23-24).
3.Kabla ya Bwana, kuwaangamiza wana wa Kora, alihitaji kuona
Musa na Haruni na wengine wasiokuwa waasi wametengwa mbali nao (Hesabu
16:20-21, 16:23-27, 16:31-35).
4.Kama Henoko na Eliya walivyotwaliwa na kwenda mbinguni bila
kufa, ndivyo watakatifu, walio hai, waliosalia watakavyotwaliwa bila kufa (Mwanzo
5:24, 2 Wafalme 2:11-12).
5.Kama Bwana Yesu alivyopaa kwenda mbinguni ndivyo watakatifu
nao watakavyoondoka kwa jinsi hiyo (Marko 16:19, Luka 24:50).
Yapo baadhi
ya madhehebu, ambayo yanawapotosha watu na kuwafundisha uongo, kwamba watu wote
watakuwepo kwenye dhiki kuu, hivyo unyakuo utafanyika baada ya dhiki kuu. Huu
ni uongo ulio wazi, kwani asiye na hatia kamwe hawezi kuingizwa kwenye adhabu (Ufunuo
3:10, Luka 21:22-23, Luka 21:34-36, 1 Wathesolanike 1:10). Hata
katika mazingira yetu ya kawaida hapa duniani, mara zote mwenye hatia anapopewa
adhabu anatengwa na mwenye haki, na ndiyo maana zikawekwa mahabusu (Selo). Ili
uweze kulielewa hili kwa mapana na marefu, ni vizuri ukijua kusudi la Mungu la
kuileta dhiki kuu. Hebu sasa fuatana nami katika sura ifuatayo ili uweze kupata
mwanga zaidi.
SIFA ZA WALE WATAKAONYAKULIWA.
Wale
watakaonyakuliwa ni lazima wawe na sifa zifuatazo:-
1. Ni wale tu walioziungama
dhambi zao na kuziacha ndiyo watakaopata rehema ya kunyakuliwa, bali wale
wazifichao dhambi zao hawatafanikiwa (Mithali 28:13)
2. Ni wale tu waliomfanya
Yesu kuwa Bwana yaani mtawala wa maisha yao yote, na kulitii kila neno
analoliagiza katika maandiko matakatifu, bila kuchagua ya kufanya
(Zaburi 119:6;
Luka 6:46; Kumb 1:35-36).
3. Ni wale tu waliookoka na
kuishi katika utakatifu mpaka mwisho, bila waa wala kunyanzi wala hila (Waefeso
5:27; Waebrania 12:14; 1 Yohana 3:2-3).
Jiweke tayari kuonana na Mungu (Amosi 4:12).
DHIKI KUBWA.
Baada ya
kunyakuliwa kwa kanisa (watu waliookoka) Dhiki kubwa, itafunika dunia nzima.
Wote walioachwa watakuwa katika kipindi hiki kizito sana cha dhiki kuu. Hii
itakuwa ni pamoja na wale wote ambao hawakukubali kuacha dhambi na kuokolewa,
pamoja na wale wote waliokuwa wameookoka, lakini maisha yao yalikuwa vuguvugu,
yaani kwa Yesu kidogo,kwa shetani kidogo, utii kidogo na uasi kidogo. Ni muhimu
sana kujifunza kwa undani zaidi juu ya kipindi hiki cha hatari sana, ili tuweze
kujihadhari na kuhakikisha hatuwi miongoni mwa watu watakaoachwa katika unyakuo.
MAANA NA MAJINA MBALIMBALI YANAYOTUMIKA
KUIZUNGUMZIA DHIKI KUU.
Dhiki kuu ni
Uangamivu, taabu, ghadhabu, pigo au hukumu ya adhabu ambayo itaachiliwa kwa
wote ambao hawakumkubali Yesu (Wokovu). Dhiki hii itakuwa kwa muda wa juma moja
la Danieli, (juma la sabini) – Danieli 9:24-27. Katika unabii wa
Danieli, juma moja humaanisha miaka saba (Mwanzo 29:27). Nusu juma
hili, ni nusu ya miaka saba yaani miaka 3½ au miezi
42, au siku 1,260. Miaka mitatu na nusu ya mwisho ya
kipindi hiki, itakuwa ya kutisha sana kwa Waisraeli baada ya mpinga Kristo
kuvunja agano nao (Ufunuo 11: 2-3; Ufunuo 12:6; Ufunuo13:5). Katika
kuleta uzito na utisho wa dhiki hii, Dhiki kuu imepewa majina mbalimbali ya
kutisha kama ilivyo:-
a) Ghadhabu
itakayokuja (1 Wathesolanike 1:10).
b) Saa
ya hukumu (Ufunuo 14:7).
c) Adhabu
ya ghadhabu (Isaya 24:21; Isaya 26:21).
d) Saa
ya kujaribiwa (Ufunuo 3:10).
e) Taabu
yake Yakobo (Yeremia 30:7).
f) Uangamivu
(Yoeli 1:15).
g) Siku
ya giza na weusi, siku ya mawingu na giza kuu (Yoeli 2:1-12).
h) Siku
ya uharibifu, fadhaa, dhiki, giza, utusitusi, (Sefania 1:15).
MAKUSUDI YA DHIKI KUBWA.
Kuna
makusudi makuu mawili yanayompelekea Mungu kuileta dhiki kuu;
i. Kuleta
hukumu ya adhabu juu ya wote ambao hawakubali wokovu
(Isaya 26:20- 21, 2 Wathesolanike 2:7-12).
ii. Kuliandaa
Taifa la Israeli kumpokea Yesu kama Masihi wao
(Kumbukumbu 4:30-31; Yeremia 30:7, Ezekieli 20:37-39; Warumi 11:25-27).
DHIKI KUU TOFAUTI NA DHIKI ZOTE.
Wanadamu wanapita katika dhiki nyingi sana duniani. Tangu zamani, vizazi hadi
vizazi, kumekuwa na shida, taabu,dhiki na mateso mazito kwa wanadamu. Mfano
watu waliompokea Yesu, wanapata dhiki na mateso kwa sababu ya wokovu wao. Dhiki
hizi kwa mtu aliyempokea Yesu inaweza ikawa kupigwa na mume, au kuachwa na
mume, kukataliwa na wazazi, kunyimwa fedha za matumizi na wazazi, au hata
kutengwa na wazazi, au jamii kuyumba kiuchumi nk. Yesu Kristo alijua kwamba mtu
aliyeookoka atapata dhiki, na akasema,” Ulimwenguni mnayo dhiki;
lakini jipeni moyo” (Yohana 16:33). Pia maandiko yanasema
tumepewa sio kumwamini Yesu tu ila kuteswa kwa ajili yake (Wafilipi 1:29).
Hata hivyo, pamoja na dhiki hizi ambazo watu wanakumbana nazo, lakini zote hizi
tunaziita ni “dhiki nyepesi” ukilinganisha na dhiki kubwa. Katika
kitabu cha 2 Wakorintho 4:17 Biblia inasema, “Maana
dhiki yetu ni nyepesi iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele
uzidio kuwa mwingi sana.” Sasa basi dhiki kubwa itakuwa haina mfano
wake tangu kuumbwa ulimwengu. Mathayo 24:21, Biblia inasema, “Kwa
kuwa wakati huo kutakuwepo dhiki kubwa ambayo haijatokea namna yake tangu
mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwepo kamwe.” Pia katika kitabu
cha Danieli 12:1 Biblia inasema, “ Wakati huo
mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako; na
kutakuwa na taabu, mfano wake hautakuwepo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata
wakati uo huo; na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana
ameandikwa katika kitabu kile.”
WATAKAO HUSIKA KUILETA DHIKI KUBWA.
Kama tulivyo
kwisha kuona katika maandiko mbalimbali katika Biblia, kwamba dhiki hii itakuwa
kubwa mfano wake hakuna, kutokana na nguvu tatu zitakazohusika kuileta dhiki
hii kwa wanadamu; yaani Mungu, shetani na Mpinga Kristo.
(i) Mungu.
Nguvu ya kwanza,
itakayohusika kikamilifu kuleta ghadhabu na mapigo juu ya wote walioachwa ni
Mungu mwenyewe. Katika kitabu cha Isaya 26:21 Biblia inasema,
“Kwa maana tazama Bwana anakuja kutoka mahali pake, ili kuwaadhibu wakaao
duniani, kwa sababu ya uovu wao; ardhi nayo itafunua damu yake, wala
haitawafunika tena watu wake waliouawa.” Pia katika kitabu cha Sefania
1:17-18 Biblia inasema, “ Nami nitawaletea wanadamu dhiki,
hata watakwenda kama vipofu sababu wamemtenda Bwana dhambi; na damu yao
itamwagwa kama mavumbi,na nyama yao kama mavi. Fedha yao wa dhahabu yao
havitaweza kuwaokoa katika siku ile ya ghadhabu ya Bwana.” Kadhalika
katika kitabu cha Yoeli 1:15 Biblia inasema, “Ole wake
siku hii! Kwa maana siku ya Bwana inakaribia, nayo itakuja kama uangamivu
utokao kwake aliye mwenyezi.” Soma pia katika (Ufunuo 14:7,
Ufunuo15:7).
(ii) Shetani.
Nguvu ya
pili, itatoka kwa shetani.Shetani atawashukia watu walioachwa kwa ghadhabu
nyingi huku akijua ni wakati wake wa mwisho. Katika kitabu chaUfunuo 12:12 Biblia
inasema, “Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa
nchi na bahari! Kwa maana yule ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi,
akijua kuwa ana wakati mchache.”
(iii) Mpinga Kristo.
Nguvu ya tatu,
itakayochangia kuileta dhiki kuu ni Mpinga Kristo (Yohana 2:8)ambaye
anajulikana pia kwa majina ya Mpingamizi, Asi, chukizo la uharibifu au mnyama,
katika kitabu cha Mathayo 24:15 Biblia inasema, “Basi
hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli,
limesimama katika patakatifu (Asomaye na afahamu).” Pia katika kitabu
cha 2 Wathesolanike 2:3-4 Biblia inasema, “Mtu awaye
yote asiwadanganye kwa njia yoyote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengefu;
akafunuliwe yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu. Yule mpingamizi, ajiinuaye
nafsi yake juu ya kile kiitwacho mungu ama kuabudiwa, hata yeye mwenyewe kuketi
katika hekalu la Mungu, akajionyesha nafsi kama kwamba yeye ndiye Mungu.”
Katika Ufunuo 13:1-6 tunaona juu ya Mnyama atokaye katika
bahari. Bahari katika Lugha ya kinabii inawakilishwa na watu, au mkutano mkubwa
wa watu; katika kitabu chaIsaya 17:12 Biblia inasema, “Aha!
Uvumi wa watu wengi! Wanavuma kama uvumi wa bahari; Aha! Ngurumo ya
mataifa! Wananguruma kama ngurumo ya maji mengi.” Pia katika kitabu cha Ufunuo
17: 12 Biblia inasema,” Kisha akaniambia, yale maji
uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha.”
Hivyo basi mnyama anayetoka katika bahari ni mtu au mwanadamu halisi. Katika
kitabu chaUfunuo 13:18 Biblia inasema, “Hapa ndipo penye
hekima. Yeye aliye na akili na aihesabu hesabu ya Mnyama huyo maana ni hesabu
ya kibinadamu na hesabu yake ni mia sita sitini na sita” Mtu huyu
au mnyama atakuwa amepewa uwezo na shetani mwenyewe na atafanya yote chini ya
usimamizi wake kama inavyoelezwa katika Ufunuo 13:4 Biblia
inasema,”Wakamsujudu Yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo; nao
wakamsujudu yule mnyama, wakisema ni nani afananaye na
mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye?” Na katika
Mnyama huyo, imezungumziwa, vichwa, pembe na vilemba; hizi ni alama za nguvu na
utawala wake utakao kuwa dunia nzima (Ufunuo 17:3, Ufunuo 17:9-13).
Kutokana na ishara zake na mateso yake atawafanya watu wengi walioachwa
kumwabudu shetani au sivyo kuuawa (Ufunuo 13:13-17) Ili litimie Neno la
Yesu Kristo Katika Yohana 5:43, “Mimi nimekuja kwa jina la
Baba yangu, wala ninyi hamnipokei; Mwingine akija kwa jina lake mwenyewe
mtampokea huyo.”
JE PAPA NDIYE MPINGA KRISTO KAMA WASEMAVYO
WAADVENTISTA WASABATO?
Ni wazi
kabisa jibu ni kwamba, Papa wa kanisa Katoliki siye mpinga Kristo (Mnyama) kama
yanavyosema mafundisho ya unabii ya Waadventista wasabato. Nina ujasiri kusema
kuwa, aliyetoa tafsiri ya unabii huu, hakuwa na ufahamu mpana wa maandiko
matakatifu katika kuutafuta ukweli huu, na ni dhahiri alitumia macho ya damu na
nyama na siyo macho ya rohoni.
Ni vizuri
kufahamu kwamba, Mungu anapotupa unabii katika maandiko matakatifu, na
akamzungumzia mtu fulani atakaye timiza unabii huo, mara zote Mungu huwa
hamweki wazi mtu huyo mpaka wakati wa kutimia unabii huo utakapofika. Mfano,
Yuda Iskariote aliyemsaliti Yesu, Alizungumziwa miaka mingi iliyopita kabla ya
Yesu kuja duniani katika Zaburi 41:9 kwamba, “Msiri
wangu tena niliyemtumaini, aliyekula chakula changu, ameniinulia kisigino chake”
Pamoja na unabii huu kutolewa muda mrefu uliopita juu ya atakayemsaliti Yesu
lakini bado Yuda Iskariote hakuwekwa wazi mpaka ilipofika wakati wenyewe,
nikiwa na maana kwamba hata wanafunzi wenzake kumi na moja hawakumjua kama yeye
ndiye msaliti, mpaka Bwana Yesu alipomdhihirisha. Pia kuna mtu tajiri
alitabiriwa katika Isaya 53:9 kuwa atamzika Yesu, mtu huyu au
tajiri huyu hakujulikana mpaka wakati ulipotimia ndipo tukajua ni Yusuph wa
Arimathaya (Mathayo 27:57-60). Kadhalika katika Isaya 40:3 Alizungumziwa
“sauti ya mtu aliye nyikani” yaani Yohana mbatizaji mwana wa Zakaria. Lakini
haikujulikana kama “Sauti ya mtu aliaye nyikani”, angekuja kuwa ni Yohana,
mpaka wakati ulipofika ndipo Mungu aliliweka wazi. Mara zote, unabii wa Mungu
unakuwa na siri kubwa sana mpaka wakati unapofika ndipo mtu au muhusika
anafunuliwa. Tunajua kuwa Mungu wetu si Mungu wa machafuko, hivyo muhusika
anapokuwa wazi mapema, usalama unakuwa mdogo sana.
Sasa, ebu jaribu
kuwaza na kujiuliza juu ya mafundisho ya waadventista wasabato kudai kwamba
Papa wa kanisa Katoliki ndiye mpinga Kristo, Je mahusiano ya waumini wa pande
hizi mbili yaani Wakatoliki na Waadventista yanakuwaje? Je ni kweli ufunuo wa
Kimungu unaleta uhasama? Mungu wetu hatoi unabii ili kugombanisha watu bali
kutimiza neno lake na kwa wakati wake.
JE NI MWANADAMU GANI ATAKAYEKUWA MPINGA KRISTO?
Ukweli ni kwamba,
mpaka sasa hakuna anayejua kuwa mpinga Kristo atakuwa nani, isipokuwa ni Mungu
peke yake ndiye anayejua. Katika kitabu cha Ufunuo 13:18 Biblia
inasema, “Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili na aihesabu hesabu
ya mnyama huyo, maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni 666.”
Unabii unaonyesha kuwa mpinga Kristo, atakuwa ni mwanadamu, lakini atapewa
uwezo wa kufanya mambo ya kutisha na shetani na atatumia nembo ya namba 666,
sasa ni mwanadamu yupi basi? Hilo analijua Mungu peke yake, na atakuja kumweka
wazi wakati ukifika, kwani ni uwezo wa Mungu kuamua ni unabii upi utimie wakati
gani na ni nani atakayetimiza unabii huo.
Ni vizuri kufahamu
kwamba katika kuihesabu hesabu ya mnyama huyu, inahitaji hekima na akili.
Hekima na akili inayozungumziwa hapa si ya kidunia, bali ni ufahamu mpana
katika ulimwengu wa Roho. Wala si swala la kufikiria na kumshuku mtu fulani.
Ningependa nikuweke wazi mpenzi msomaji wa kitabu hiki kuwa alama au nembo ya
666 inatumika katika ulimwengu wa nguvu za giza. Tukirejea katika kitabu cha Mkuu
wa wachawi sasa ampokea Kristo cha Iyke Nathan,
kinazungumzia juu ya ngazi za juu za utenda kazi wa nguvu za giza. Shetani
hufanya kazi na makundi 400,000 ya roho za giza kwa kushirikiana. Makundi hayo
yamejigawa katika ngazi tano na kila ngazi hujulikana kwa nembo yenye namba.
Ngazi hizo ni kama ifuatavyo:-
i. Ngazi
ya 333.
ii. Ngazi
ya 666.
iii. Ngazi
ya 999 (liber 007 sagna seal-liber 777).
iv. Ngazi
ya 1330 (Bavara seal).
v. Ngazi ya 003(Liber
003-Tuzassotama seal).
Kwa upande
wangu, ningependa kuizungumzia ngazi ya kichawi ya pili yaani ngani ya 666.
Mwanadamu yeyote anayefikia ngazi hii ya juu ya kichawi ni lazima awe amepitia
mafunzo mazito sana ya nguvu za giza. Ngazi hii yenye nembo 666 inahitaji
digrii za kichawi 30,000 ili kuifikia. Anayekuwa amepata nembo hiyo anakuwa na
cheo cha kuweza kutawala roho chafu 160,000 ambazo hufanya kazi chini yake na
kwa mamlaka na amri yake. Hii inakuwa tayari ni ngazi ya Mpinga kristo. Watu
wenye ngazi hiyo wamesababisha maafa makubwa ya kihistoria hapa duniani. Mifano
ya watu waliofikia ngazi hii ya kichawi hapa duniani ni kamaAdolf Hitler ambaye
alikuwa mtawala wa kiimra (kidikteta) nchini Ujerumani miaka ya nyuma. Pia
mwanasayansi mkubwa aliyejulikana sana duniani aliye tangaza kuwa hakuna Mungu
mwaka 1859 ambaye ni Charles Darwin. Kadhalika Idd Amini aliyekuwa
Rais wa Uganda na wengine wengi. Hawa wote ndiyo waliofikia ngazi hii ya pili
ya kichawi yenye nembo 666, na waliweza kufanya mambo yote ya kutisha
wakiwezeshwa na roho chafu 160,000. Watu wengi wenye majina makubwa kama
wanasiasa, wakuu wa majeshi, wakuu wa dini mbalimbali na watu wazito wengi hapa
duniani, waliopo katika mtandao wa nguvu za giza, ndiyo wanaopewa cheo hiki cha
pili na shetani. Kwahiyo, Mpinga Kristo atakuwa ni miongoni mwa wanadamu walio
na majina makubwa hapa duniani, na ni mshiriki katika ufalme wa giza akiwa na
ngazi ya pili ya kichawi yenye nembo ya 666. kwa vile, aliye na ngazi hii
humiliki roho chafu 160,000 tu kumuwezesha kutenda kazi, hivyo shetani
atamuongezea nguvu zaidi, yaani roho chafu nyingine, ili aweze kufanya mambo ya
ajabu na ya kutisha katika kipindi cha dhiki kuu. Mpiga Kristo atakuwa mtu
hatari sana mara nyingi zaidi ya Adolf Hitler au Idd Amini. Na siri kuu iliyopo
kwa wenye ngazi ya pili ya kichawi yenye nembo ya 666, huwa wanapinga sana
uwepo wa Taifa teule la Mungu yaani Waisraeli, kama ilivyokuwa kwa Adolf Hitler
na Idd amini, kwani 666 ni nembo ya Mpinga Kristo, na Kristo anatokea
taifa la Waisraeli. Hivyo kwa kuwapinga wana wa Israeli tayari wanampinga
Kristo.
HALI HALISI ITAKAVYOKUWA WAKATI WA DHIKI KUBWA.
Wakati wa
dhiki kubwa kutakuwa na mateso na dhiki yasiyoelezeka. Itakuwa ni kilio na
kusaga meno kwa wale walioachwa. Watu watapata mateso makali kwa muda mrefu na
hatimaye watauawa, na damu yao itamwangwa kama mavumbi na nyama zao kama mavi,
wala hatakuwepo watu wa kuwalilia wala kuwazika (Sefania 1:15-18; Yeremia
25:33). Hasira ya Mungu iliyojiwekea akiba itafunuliwa wakati wa dhiki
kubwa ( Sefania 2:1-3). Watu wataiambia milima iwaangukie
iwasitiri, haitafanya hivyo (Ufunuo 6:15-17). Watu watakuwa katika
maumivu mchana na usiku wakinywea kikombe cha mvinyo ya kadhabu ya Mungu
isiyochanganya na maji (Ufunuo 14:9-11). Watu watatamani kujiua, lakini
mauti ya namna hiyo haitakuwepo, mpaka wateswe na kuuawa (Ufunuo 9:2-6).
Mapigo ya Mungu yatatimizwa kwa kumwangwa kwa mapingo saba ya kutisha juu ya
wanadamu (Ufunuo 15:1; Ufunuo 16:1-21). Kutokana na taabu
watakayopata, wanadamu watamwomba Mungu hili awahurumie, lakini huruma ya Bwana
itakuwa imekoma (Isaya 26:16-18). Wachungaji, mitume, manabii, waalimu
na wainjilisti ambao hawakukubali kuishi katika wokovu, na wanaowapoteza watu,
watakuwepo wenye mateso hayo (Isaya 24:1-6). Hakika itakuwa dhiki kubwa
sana (Isaya 24:17-18). Katika miaka 31/2 ya
mwanzo kutakuwa na nafuu kidogo kwa Taifa la Israeli kutokana na Angano la
uongo ambalo mpiga Kristo atakuwa amelifanya na Israeli. Miaka 31/2 iliyosalia
chukizo la uharibifu litasimama kikamilifu juu ya taifa la Israeli (Danieli
9:27). Kimsingi dhiki kuu inakuwa kama kujiokoa kwa damu yako mwenyewe,
kwasababu ya kukataa kuokolewa kwa damu ya Yesu.
Ghadhabu juu ya
Israeli itakuwa kubwa sana kiasi cha kuwafanya Waisraeli wakimbie nchi yao (Mathayo
24:15-16). Kwa ajili ya wateule, siku za dhiki kubwa zitafupishwa (Mathayo
24:21-22). Wateule wanaotajwa hapa siyo sisi tuliokoka Leo. Neno “mteule”
au “wateule” linatumika katika Biblia kwa maana nne tofauti,
(a) Yesu Kristo (Isaya 42:1)
(b) Malaika watiifu (1Timotheo 5:21)
(c) Sisi tuliookoka (Tito 1:1; 1Petro
1:1-2, Warumi 8:33, Luka 18:7)
(d) Taifa la Israeli (Isaya 65:8-9; 45:4)
kwa hiyo wateule katika Mathayo 24:21-22, ni taifa la Israeli.
JINSI YA KUIKWEPA DHIKI KUBWA.
Katika Isaya
26:20 Biblia inasema, “Njoni, watu wangu, ingia wewe ndani ya
vyumba vyako ukafunge mlango nyuma yako ujifiche kitambo kidogo mpaka ghadhabu
hii itakapopita” Kila anayetaka kuikwepa dhiki hii kubwa inambidi
kujificha ndani ya vyumba na kufunga nyumba kama wakati wa Safina ya Nuhu kwa
kufanya yafuatayo:-
(i) Kuhakikisha umetubu dhambi na
kuziacha na kuokolewa kwa kumwamini Yesu Kristo. (Mithali 28:13; Yohana
3:36, Ufunuo 13:10, Isaya 33:1)
(ii) Kukaa ndani yake Yesu kwa kufuata Neno
lake na maagizo yake yote kwa gharama yoyote, siyo kukaa ndani ya mapokeo ya
wanadamu au ndani ya dhehebu (1Yohana 2:28; Zaburi 119:6,9)
(iii) Kukaa mahali ambapo pana waalimu wenye mafundisho
yote ya kweli ili tujue nini mapenzi ya Mungu (Isaya 30:20-21). Kuwa
mbali na viongozi wanaofundisha uongo (Isaya 9:14-15).
Mtu akiwa na sikio na asikie (Ufunuo 13:9).
TAJI NA HARUSI YA MWANAKONDOO.
Katika sura
iliyopita, tumeona jinsi watu wenye dhambi watakaoachwa katika mateso na
maumivu ya kutisha kwa miaka saba. Sasa basi, katika sura hii tunakwenda
kujifunza juu ya yale yatakayoambatana na wale watakaokuwa wamenyakuliwa kwenda
kumlaki Bwana Yesu mawinguni.
KUONDOKA KWA SHANGWE KWA WATAKATIFU.
Wakati wa
kunyakuliwa kwa watakatifu hapa duniani kwa muda mfupi sana watafundishwa
nyimbo mbili na Mungu mwenyewe, wimbo mmoja unaitwa wimbo wa Musa na mwingine
wimbo wa mwanakondoo, katika kitabu chaUfunuo15:3-4 Biblia
inasema,”Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu,na wimbo wa
mwanakondoo, wakisema, Ni makuu na ya
ajabu matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi ni za haki na za kweli, njia zako,
Ee mfalme wa mataifa. Ni nani asiyekucha, Ee Bwana, Ee Bwana na kulitukuza jina
lako? Kwa kuwa wewe peke yako umtakatifu; Kwa maana mataifa yote watakuja
kusujudu mbele zako; kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha kufunuliwa”.
Mungu alimfundisha Musa wimbo na kumwambia awafundishe Waisraeli ili waukumbuke
wakati Mungu atakapowaka hasira juu yao na kuwaacha (Kumbukumbu 31:17-19;
Kumbukumbu 32). Hiki kilikuwa ni kivuli cha mambo yajayo wakati watakatifu
watakapoimba wimbo wa Musa na wa Mwanakondoo na kuondoka huku nyuma yao
hasira ya Mungu ikidhihirika kwa wenye dhambi waliobaki wakati wa dhiki kubwa.
Vilevile, Musa na wana wa Israeli baada ya kuwaona wamisri wamekuja na
kuteganishwa nao kabisa waliimba wimbo wa Musa wakiwa wanaanza kwenda Kanaani (Kutoka
15:1-20) Watakatifu nao itakuwa hivyohivyo. Wataimba wimbo wa Musa
watakapoanza kwenda Kanaani. Siyo hilo tu, Yesu Kristo alikuwa akiimba na
wanafunzi wake hivyo alikuwa mwimbaji, katika kitabu cha Marko 14:26 Biblia
inasema, “Nao walipokwisha kuimba walitoka kwenda mlima wa mizeituni”.
Wimbo huu ndiyo wimbo wa mwanakondoo. Watakatifu watauimba wakiwa wanapaa juu
mawinguni baada ya kumshinda shetani na majaribu yake yote.
KITI CHA THAWABU.
Neno la
Mungu yaani Biblia mara zote inazungumzia juu ya kulipwa kwa kazi inayofanywa
na watumishi wa Mungu hapa duniani.Biblia inasema tutapewa taji au thawabu (Ruthu
2:12; Zaburi 58:11; Mithali 13:13; Isaya 40:10; Yeremia 31:16; Mathayo 5:12;
1Wakorintho 3:8; 1Wakorintho 9:25; 1Wakorintho 15:58; Waebrania 10:35; 2Yohana
1:8, Yohana 4:35-36). Thawabu au taji hizi atakuja nazo Yesu mwenyewe
mawinguni na kila mmoja atalipwa kulingana na utumishi aliomfanyia Mungu katika
kipindi chake chote cha wokovu hapa duniani.Taji hizi zitatolewa mawinguni mara
tu baada ya kumlaki Yesu (Ufunuo 22:12; 2Timotheo 4:8; Luka 14:12-13).
Wakati wa kutoa taji hizi, Bwana Yesu atakalia kiti maalumu kinachoitwa Kiti
cha hukumu cha Kristo (2Wakorintho 5:10), kiti hiki kwa kiyunani
kinaitwa “Bema”. Ni kiti atakachokalia Yesu na kutoa hukumu kwamba nani
apewe thawabu au taji ipi.Kwa upande mwingine tungeweza kukiita “Kiti cha
Thawabu au taji.”
KUJARIBIWA KWA KAZI YA KILA MTU.
Katika
mchakato mzima wa kujua nani apewe taji ipi, kazi ya kila mtu aliyeokoka
aliyoifanya katika kumtumikia Mungu, itajaribiwa kwa moto ili ipate kufahamika
thawabu ipi mtu atakayopata, katika kitabu cha 1Wakorintho 3:10-15 Biblia
inasema, “Kwa kadri ya neema ya Mungu, niliyopewa mimi kama mkuu wa
wajenzi mwenye hekima naliuweka msingi na mtu mwingine anajenga juu yake.
Lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake. Maana msingi mwingine
hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa yaani Yesu
Kristo, lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huo dhahabu au fedha au mawe ya
thamani au miti au majani au manyasi kazi ya kila mtu itakuwa dhahiri, maana
siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto na ule moto wenyewe
utaijaribu kazi ya kila mtu ni ya namna gani, kazi ya mtu aliyoijenga juu yake
ikikaa atapata thawabu. Kazi ya mtu ikiteketea, atapata hasara ila yeye
mwenyewe ataokolewa lakini ni kama kwa moto”. Ikiwa kazi
aliyoifanya mtu ni ya thamani sana kama dhahabu, fedha au mawe ya thamani,
itakapopitishwa katika moto itazidi kung’aa na wengine wote watashangilia
pamoja na malaika. Ikiwa kazi aliyoifanya mtu ilikuwa duni, itakapopitishwa
katika moto itateketea kama miti, majani au manyasi na itakuwa ni aibu! Ingawa
mtu ataendelea kuwepo mbinguni; atakuwa kama mhalifu msalabani bila kuwa na
taji yoyote na daraja yake itakuwa ya chini.
AINA ZA TAJI ZITAKAZOTOLEWA KWA WATAKATIFU.
Haitafurahisha kabisa kumuona mtu ambaye hakupewa taji yoyote wakati alikuwa na
muda wa kumfanyia kazi Mungu tofauti na yule mwizi pale msalabani. Ni wajibu
wetu kutamani sana kupata taji zozote zifuatazo tena kwa gharama yoyote katika
maisha yetu ya wokovu. Kwa hiyo zifuatazo ndizo taji zitakazotolewa na Yesu
Kristo kwa watakatifu katika harusi ya mwanakondoo.
1: Taji
isiyoharibika (Incorruptible Crown) (Wakorintho 9:23-25).
Taji hii watapewa
watakatifu ambao walifanya mambo yote kwa ajili ya injili, walijizuia yote
katika maombi yao kwa ajili ya injili ili kushiriki pamoja na wengine.
Walijizuia yote katika utoaji wao kwa ajili ya injili, walijizuia yote katika
maombi yao kwa ajili ya injili na pia walitumia vyote walivyo navyo; muda,
ujuzi, vipawa, cheo chao, uwezo wao wote, nguvu zao n.k kuishiriki injili
pamoja na wengine.
2: Taji ya
kujionea fahari (Crown of Rejoicing)( 1Wathesalonike 2:19, Daniel 12:3).
Taji hii inaitwa
taji ya kujionea fahari kwa sababu watakaopata taji hii watang’ara kama nyota
tofauti na wengine watakavyong’ara. Fahari yao itakuwa kubwa kuliko ya wengine.
Mng’ao wao wa utukufu utakuwa mkubwa kuliko wengine. Taji hii watapewa wale
waliowaleta watu wengi kwa Kristo, kutokana na kushuhudia kwao au kuhubiri injili.
Washuhudiaji wale waliozaa watoto wengi katika injili yao ya nyumba kwa nyumba
au vinginevyo na wakahakikisha watoto hao wanakuwa kiroho kwa kuwafundisha au
kuwaongoza kwa walimu wazuri watakaowafundisha watapewa taji hii.
3: Taji ya uzima
(Crown of life) (Ufunuo 2:10).
Taji hii ni maalum
kwa wale waliopita katika majaribu au mitihani mikubwa ya maudhi na kuchukiwa
kwa ajili ya Kristo na wakashinda au hata kufa, hawakupenda maisha yao kufa,
lakini walifanya hivyo kwa ajili ya Kristo (Yakobo 1:2; Ufunuo 12:11;
Mathayo 5:11 – 12 Waebrania 11:24-26; Zaburi 129:2).
4: Taji ya haki
(Crow of Righteousness) (2Timotheo 4:6-8).
Taji hii ni kwa
wale waliopenda kufunuliwa kwake Yesu Kristo.Wakati wote walikubali kutii kila
neno aliloagiza Bwana Yesu. Walikuwa na utakatifu wakati wote. Kila neno
walilojifunza walilitendea kazi, kwao hakukuwa na kurudirudi nyuma na kwenda
duniani kwanza, halafu wakaendelea tena na wokovu kidogo.Hivyo Yesu akawakuta
katika hali ya utakatifu. Taji hii pia ni kwa wale waliowatendea mema adui zao
(Luka 6:34-36).
5: Taji ya
utukufu, ile isiyokauka (Crown of Glory) (1Petro 5:2-4).
(a) Taji hii watapewa wachungaji,
waalimu au watumishi wa Mungu wanaojitaabisha kuwafundisha wengine na kuwalea
kiroho kwa njia zozote, kuwafundisha kanisani na kuwapa huduma za kichungaji,
kuandika vitabu au tracts za mafundisho ya neno la Mungu yanayowasaidia watu
wakue kiroho.
(b) Taji hii pia watapewa wale
wanaowahudumia mitume, wachungaji, manabii, wainjilisti na waalimu ili wapate
urahisi wa kuzifanya kazi zao(Mathayo 10:41-42).
(c) Taji hii watapewa wote
wanaochukua muda wao wote kuwasaidia watu kukua kiroho kama kuwaazima au
kuwanunulia vitabu, CD au kaseti za mafundisho, kuwapa nauli ili waende
kanisani, kazi za kuhudumia kanisani n.k.
HARUSI YA MWANAKONDOO.
Watakatifu walionyakuliwa wanaitwa Bikira safi wa Kristo, katika2Wakorintho
11:2 Biblia inasema, “Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu kwa
kuwa naliwaposea mume mmoja ili nimletee Kristo bikira safi”. Lakini
pia wanaitwa Bibi harusi wa Kristo, katika Yohana 3:29Biblia
inasema, “Aliye naye bibi harusi ndiye bwana harusi lakini rafiki yake
Bwana harusi yeye anayesimama na kumsikia alifurahia sana sauti yake bwana
harusi.”Hivyo baada ya kupewa taji, Yesu atawafanyia watakatifu karamu
ya kuwapongeza. Hii ndiyo karamu ya mwanakondoo (Ufunuo 19:7-9). Hii
itafanyika katika kipindi hichohicho cha miaka saba wakati huku duniani wakiwa
katika dhiki kuu.
JINSI YA KUSHIRIKI HAYA YOTE.
(i) Kuwa
miongoni mwa watakatifu (Waebrania 12:14)
(ii) Kuifanya
kazi ya Mungu kwa bidii zote na nguvu zote (Muhubiri 9:10;
Yohana 4:34-36 Warumi
12:11, 1Wakorintho 7:29-35).
Tumeokolewa ili tumtumikie Mungu
(Kutoka 8:1; Kutoka 10:24-26; Kutoka 12:31)
KUJA KWA YESU MARA YA PILI DUNIANI.
Tukiangalia
katika sura zilizopita, kwamba dhiki kubwa au dhiki kuu itachukua kipindi cha
miaka saba (07). Katika kipindi hiki pia watakatifu walionyakuliwa watakuwa
katika kipindi cha kupewa taji na kufanyiwa karamu ya harusi ya mwanakondoo.
Hivyo ni makusudi ya sura hii kujifunza tukio litakalofuata mwisho wa miaka
saba. Tukio hili ni kuja kwa Yesu Kristo mara ya pili Duniani.
KUJA KWA YESU MARA YA PILI DUNIANI.
Yesu Kristo,
mara ya kwanza alikuja hapa duniani katika hali ya udhaifu na unyonge kwa
kuzaliwa na Mariamu na kulazwa katika holi ya kulia ng’ombe. Kwa Waisraeli
ambao hawakujua maandiko vema, hawakutambua kwamba Kristo ndiye Yesu, kutokana na
mazingira yake ya umasikini na unyonge, katika kitabu cha Luka 9:58 Biblia
inasema, “Yesu akamwambia, mbweha wana pango na ndege wa angani wana
viota, lakini mwana wa Adamu hana pa kujilaza kichwa chake.” pia
katika kitabu cha 2Wakorintho 8:9 Biblia inasema, “Maana
mmejua neema ya bwana wetu Yesu Kristo jinsi alivyokuwa masikini kwa ajili yenu
ingawa alikuwa tajiri ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umasikini wake.”
Wana wa Israeli walidhani kwamba wakati ule wa kwanza angekuja kama mfalme,
kumbe kwa Kristo kuja kama mfalme ilikuwa ni wakati wa kuja mara ya pili
duniani. Wakati wa kuja kwa Yesu mara ya pili, atakuja katika mazingira tofauti
kabisa na pale mwanzoni.Atakuja katika hali zifuatazo;
(a) Atakuja kama umeme (Mathayo 24:27).
(b) Atakuja pamoja na Malaika na uwezo wake (2Wathesalonike
1:7-8).
(c) Atakuja juu ya mawingu pamoja na
nguvu na utukufu mwingi
(Mathayo 24:30; Mwanzo
25:31).
(d) Atakuja kama mfalme wa wafalme na Bwana wa
mabwana (Ufunuo 19:16).
HALI HALISI YA KUJA KWA YESU MARA YA PILI DUNIANI.
Mara tu
baada ya harusi ya mwanakondoo, mwishoni mwa ile miaka saba, Yesu Kristo
atawachukua watakatifu wote aliowanyakua na kuanza nao safari kuja
duniani.Bwana Yesu atakuwa amepanda farasi mweupe akiongoza. Watakatifu nao kila
mmoja atakuwa amepanda farasi mweupe wakifuata maelfu kwa maelfu pamoja na
malaika, katika kitabu cha Yuda 1:14 Biblia inasema,” Na
Heroko, mtu wa saba baada ya Adamu alitoa maneno ya unabii juu ya hao akisema,
Angalia Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu na maelfu”. Pia katika
kitabu cha Ufunuo 19:11-14 Biblia inasema, “Kisha
nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda,
aitwaye mwaminifu na wa kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita. Na macho
yake yalikuwa kama mwali wa moto na juu ya kichwa chake vilemba vingi naye ana
jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe. Naye amevikwa vazi
lililochonya katika damu na jina lake aitwa, Neno la Mungu. Na majeshi yaliyo
mbinguni yakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe
safi”.
Bwana Yesu
atakuwa amezungukwa na mwali wa moto na atakuja kama umeme unaonekana pande
zote. Na mara tu safari ya kuja duniani itakapoanza, jua litatiwa giza na mwezi
hautatoa mwanga na nyota zitaanguka kutoka mbinguni kwa ajili ya kupamba
sherehe ya kifalme. Nyota hizi ni zile zipitazo upesi mawinguni (Meteros) au
kwa kiswahili “Vimondo” (Mathayo 24:29-30).
Bwana Yesu
atakuja na kukanyaga mlima mizeituni, mahali palepale alipopaa kwenda mbinguni
wakati Yesu alipotoka duniani mara ya kwanza (Matendo 1:10-12). Katika
kitabu cha Zekaria 14:4 Biblia inasema, “Na siku hiyo
miguu yake itasimama juu ya mlima wa Mizeituni unaoelekea Yerusalemu upande wa
mashariki, nao mlima wa Mizeituni utapasuka katikati yake upande wa mashariki
na upande wa magharibi, litakuwapo huko bonde kubwa sana na nusu ya mlima ule
utaondoka kwenda upande wa kaskazini na nusu yake utaondoka kwenda upande wa
kusini”
Mara tu
baada ya kushuka, kazi ya kwanza atakayofanya Bwana Yesu itakuwa kuwatuma
malaika ili kuwakusanya Waisraeli wote waliotawanyika duniani kote wakikimbia
dhiki nzito juu ya Israeli katika ile miaka 3½ ya mwisho wa dhiki kubwa. Wale
wote waliokwepa kupotezwa na Kristo wa uongo (Mpinga Kristo) watakusanywa (Mathayo
24:23-27;
Mathayo 24:29-31).
Tofauti kati ya kuja kwa Yesu wakati wa unyakuo wa kanisa na
kuja kwa Yesu mara ya pili Duniani.
Watu wengi
huwa wanachanganya matukio haya mawili, lakini ni matukio yaliyo tofauti
kabisa, lifuatalo ni jedwali linaloonyesha utofauti huo;
KUJA KWA YESU WAKATI WA KUNYAKULIWA KWA KANISA.
|
KUJA
KWA YESU MARA YA PILI.
|
· Anakuja kama Bwana Arusi kumchukua Bibi Arusi wake yaani
kanisa tukufu lisilo na waa wala doa
(Waefeso
5:27; Yohana 14: 1 – 3).
|
· Bwana Harusi Yesu Kristo anakuja pamoja na bibi harusi
kutoka huko juu na kuja hapa duniani kutawala na watakatifu wake (Yuda
1:14; Ufuno 1:7).
|
· Anakuja na kukutana na watakatifu wake mawinguni
hatakanyaga dunia na waliopo duniani hawatamwona wakati huu (1Wathesalonike
4:17).
|
· Anakuja duniani na kukanyaga mlima Mizeituni na waliopo
duniani watamwona (Zekaria 14:4-5: Mathayo 24:27).
|
· Kunyakuliwa
kwa kanisa ni kabla ya Dhiki kubwa (Ufunuo3:10; Luka 21:22-23; Luka
21:34-36; 1Wathesalonike 1:10).
|
· Kuja kwa Yesu mara ya pili duniani ni mara baada ya dhiki
kubwa
(Mathayo
24:29-30;2 Wathesalonike2:1-4).
|
MAKUSUDI YA KUJA KWA YESU MARA YA PILI DUNIANI.
Yapo makusudi
makuu matatu ya kuja kwa Yesu mara pili duniani;
a) Kutawala mataifa yote
duniani miaka 1,000 pamoja na watakatifu wake, kama mfalme wa wafalme na Bwana
wa Mabwana (Ufunuo 11:15; Ufunuo 2:26; Ufunuo 5:10;
Ufunuo 20: 4-5).
b) Kuwalipiza kisasi wao
wasiomjua Mungu na wao wasioitii injili ya Bwana wetu Yesu Kristo (2Wathesalonike
1:8; Yuda 1:14-15)
c) Kuwakusanya Waisraeli na
kuwabagua Waisraeli (kondoo) mbali na mataifa waliosalia katika dhiki kubwa
(mbuzi) Waisraeli wote watakaokusanywa wataokolewa na Yesu
(Mathayo 24:31;
Isaya 11:12; Mathayo 25:31 – 34; Warumi 11:25-31).
Wana wa
Israeli au Wayaudi, watabadilisha kabisa msimamo wao kuhusu masihi Yesu Kristo.
Watalia kwa uchungu na wakiomboleza huku wakijilaumu kwa nini walimkataa na
kumchoma kwa mkuki ubavuni na kisha watamkubali kuwa Masihi na mwokozi wao
(Ufunuo 1:7; Zekaria
12:10-14; Zekaria 13:6; Isaya 3:9; Zekaria 13:9).
VITA VYA HAR-MAGEDONI NA KUFUNGWA KWA SHETANI
MIAKA ELFU MOJA.
Kabla ya
utawala wa Kristo miaka 1000 pamoja na watakatifu wake kutatokea vita
ijulikanayo kama vita vya Har-magedoni (Ufunuo 16:14-16). Vita hivi
vitatokana na mpango wa shetani wa kutaka kuchukua ufalme kutoka kwa Yesu
Kristo kama alivyojaribu kufanya mbinguni (Ufunuo 12:7-8).
Kabla ya
kuja kwa Yesu mara ya pili duniani kwa jitihada za pamoja; shetani, mpinga
Kristo (Mnyama) na nabii wa uongo watatuma roho chafu ambazo zitawaandikisha
watu wa mataifa yaliyobaki katika dhiki kuu kutoka duniani kote na kuweka
tayari kwa vita ili kupigana na majeshi ya Yesu Kristo mahali paitwapo kwa
kiebrania “Har-magedoni” Hapa ni bonde la Megido ambalo limekuwa mahari
pa vita muda mrefu sana. Bonde hili lipo kusini magharibi mwa mlima karmeli,
katika kitabu 2Nyakati 35:22 Biblia inasema, “Walakini
Yosia hakukubali kumgeuzia uso mbali, akajibadilisha apate kupigana naye
asiyasikilize maneno ya Neko, yaliyotoka kinywani mwa Mungu, akaja kupigana
bondeni mwa Megido”. Pia katika kitabu chaZekaria 12:11 Biblia
inasema” Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu kama
maombolezo ya hadadrimoni katika bonde la Megido”
Kwa ujumla
katika bonde hili, Yoshua alifanya vita na kumshinda mfalme wa mji huu wa
wakanaani; katika eneo hili pia Sisera na jeshi lake walishindwa na hatimaye
kukimbia, katika eneo hili Sulemani aliuimarisha mji, kadhalika Ahazia alikufa
mahali hapa; pia Yosia aliuawa katika eneo hili katika vita na Farao Neko (Yoshua
12:21, Waamuzi 5:19-20; 1Wafalme 9:15; 2Wafalme 9:27, 2 Wafalme 9:23:29).
Katika vita
hiyo kutakuwa na mauaji makuu. Wenye dhambi watauwa kwa maangamizo makuu (Ufunuo
17:12-14, Ufunuo 14:19-20; Ufunuo 19:11-21; Isaya 13:9; Isaya 29: 5-8).
Hapo ndipo Bwana Yesu ataonekana kuwa mtu wa vita na Bwana wa vita halisi, kama
maandiko yanavyosema katika kitabu chaKutoka 15:3, “Bwana ni mtu
wa vita Bwana ndilo jina lake” Baada ya vita hivi, shetani atashikwa na
kufungwa miaka elfu moja (Ufunuo 20:1-3), na hapa ndipo utakapoanza
utawala wa miaka elfu moja wa Yesu Kristo duniani.
Je ungependa kupanda farasi mweupe pamoja na Yesu?
(Ufunuo 19:11-14).
MIAKA 1,000 YA UTAWALA WA YESU DUNIANI.
Tulijifunza
katika sura iliyopita jinsi ambavyo Yesu Kristo atakavyokuwa mtu wa vita au
Bwana wa vita halisi. Yesu atawauwa wenye dhambi wote waliojipanga kupigana
naye mahali paitwapo kwa Kiebrania Har-magedoni. Wale wote
watakaouawa hapa, ndege watashiba nyama zao; kisha yule mnyama yaani mpinga
Kristo na yule nabii wa uongo watakamatwa na kutupwa wangali hai katika ziwa la
moto. Katika kitabu cha Ufunuo 19:20-21 Biblia inasema “Yule
mnyama akakamatwa na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo
ishara mbele yake ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa
ya huyo mnyama nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hai
katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti na wale waliosalia waliuawa kwa
upanga wake yeye aliyeketi juu ya yule farasi, upanga utokao katika kinywa
chake. Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao.”
Baada ya
tukio hilo, shetani naye atakamatwa na kutupwa kwenye shimo refu sana na
kufungiwa humo kwa miaka 1,000. Biblia zote za Kiswahili limetumika neno shimo
la kuzimu hata hivyo ni muhimu kufahamu kwamba hapa
hawakumaanisha Jehanamu ya moto. Biblia za Kiingereza
linatumika nenoBottomless pit (Ufunuo 20:1-3). Baada
ya kufungwa shetani ndipo utawala wa Yesu Kristo duniani pamoja na watakatifu
wake utakapoanza (Ufunuo 20:4-6).
MAKUSUDI YA UTAWALA WA YESU KRISTO MIAKA 1,000 DUNIANI.
Ni vizuri
tukifahamu kwamba mwanzoni kabisa katika mpango wa Mungu, mwanadamu alikusudiwa
kuishi maisha ya amani, furaha na mafanikio chini ya utawala wa Mungu mwenyewe.
Adamu alipotenda dhambi aliukatisha mpango huu kwa Mwanadamu na kutolewa katika
bustani ya Edeni. Hapo ndipo maisha magumu kwa mwanadamu yalipoanza. Ardhi ililaaniwa
na tukaanza kula chakula kwa jasho, na kuishi maisha ya taabu tofauti kabisa na
mpango wa Mungu kwa mwanadamu (Mwanzo 3:13-19). Ndipo Mungu alipoanza
mpango wa kumrudisha mwanadamu katika amani na furaha aliyomkusudia na hatimaye
akaja Yesu Kristo duniani mara ya kwanza na kufa kwa ajili ya dhambi zetu. Hata
hivyo katika kukamilisha kile alichokikatisha Adamu, Mungu katika mpango wake
amekusudia kuuonyesha ulimwengu maisha yale aliyoyakusudia kwa mwanadamu kama
wasingekubali kuacha utawala wake na kuugeukia utawala wa shetani. Kwa kuwa
shetani atakuwa amefungwa miaka elfu moja, wanadamu wataweza kutawaliwa bila
kushawishiwa na ibilisi kutenda dhambi na kuwa katika serikali moja duniani
kote, iliyo chini ya mtawala Yesu Kristo. Utawala huu utawaongezea majuto
wanadamu wenye dhambi waliomkataa Mungu atawale kwa kuona wema na uzuri wake.
HALI YA MAISHA ITAKAVYOKUWA DUNIANI WAKATI WA UTAWALA WA
YESU KRISTO DUNIANI.
1 FURAHA ITAJAA
KABISA ULIMWENGUNI.
Hakutakuwa na huzuni wala masikitiko kabisa ulimwenguni
(Isaya 9:3-4; Yeremia 31:13).
2 UTAKATIFU
UTATAWALA DUNIANI.
Kama ilivyokuwa kipindi cha
waamuzi katika agano la kale, watakatifu watakaotawala na Kristo watakuwa ni
waamuzi. Watashauri watu na kuwahukumu kwa hekima kuu itakayoleta maisha ya
uaminifu na yote yanayompendeza Mungu (Isaya 1:26)
3 HAKUNA KUUGUA
DUNIANI.
Magonjwa ni ya shetani,
kwa kuwa shetani atakuwa amefungwa, kutakuwa hakuna magonjwa kabisa na
hosipitali zitakuwa hazina kazi. Isaya 33:24Biblia inasema, “Wala
hapana mwenyeji atakayesema, mimi mgonjwa; watu wakaao humo watasamehewa uovu
wao.”
4 LAANA JUU YA
ARDHI ITAONDOLEWA.
Laana ya mwanzo (Mwanzo
3:17-19) itaondolewa hakutakuwa na miiba wala magugu. Mvua itakuwa ya
manyunyu safi. Ukilima kidogo utavuna sana. Kutakuwa hakuna kula kwa jasho (Ezekieli
34:26-27).
5 Utakuwa utawala
wa haki tupu wala watu hawatasikia upendeleo, rushwa, ufisadi nk. (Isaya
9.7; Isaya 11:5; Yeremia 23; 5 ; Isaya 33:15).
6 KUTAKUWA
HAKUNA KUFA.
Watu watazaliwa tu, lakini hakuna
kufa. Watu watakuwa wengi mno duniani (Amosi 9:15; Zekaria 14:9-11)
7 Hakuna kuonewa,
njaa, kiu wala mateso (Isaya 49:10; Isaya 14:3-7). Nyakati hizo zitajaa
kuimba tu hakuna jua kali wala baridi kali.
8 Dunia
itapendeza mno na hakutakuwa na umasikini. Kila sehemu kutakuwa na maua mazuri
mno wala hakutakuwa na magonjwa kabisa (Isaya 65:21-24; Isaya 35:1-2)
9 DUNIA
ITAJAWA NA KUMJUA BWANA.
Kila mtu atamjua Mungu yaani wema
wake, uzuri wake, haki yake n.k kila mtu atamjua Yesu kuwa ni Mungu na kujawa
maarifa kamili ya mpango wake kwa mwanadamu
(Isaya 11:9; Habakuki 2:14).
10 HAKUTAKUWA NA VILEMA, VIZIWI, MABUBU
DUNIANI.
Kazi zote hizi zilitokana na
shetani kupewa nafasi kumtawala Adamu. Zitamalizwa katika utawala wa Yesu
duniani (Isaya 29:18; Isaya 35:3-6).
11 Hakutakuwa na vita kabisa kati ya
mwanadamu na mwanadamu.Silaha zitabadilishwa kuwa vyombo vya amani kama
maandiko yanavyosema katikaIsaya 2:4,” Naye atafanya hukumu kati ya
mataifa mengi, atawakemea watu wa kabila nyingi; nao watafua panga zao ziwe
majembe, mikuki yao iwe miundu, taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine,
wala hawatajifunza vita tena kamwe.”(Zekaria 9:10; Mika 4:3). Juhudi
za kuleta amani zimeshindikana kuletwa na umoja wa mataifa hivi sasa.Haya yote
yatatimia wakati wa utawala wa Yesu duniani.Katika utawala huu hakutakuwa na
mbu,funza,kunguni au wadudu wowote wabaya kama bacteria n.k.Vilevile hakutakuwa
na ndege wa kula nafaka wala wanyama waharibifu.Katika kitabu cha Hosea
2:18 Biblia inasema,” Nami siku hiyo nitafanya agano na
wanyama wa mashamba kwa ajili yao,tena na ndege wa angani,tena na wadudu wa
nchi,nami nitavivunja upinde na upanga na silaha vitoke katika nchi, nami
nitawalalisha salama salmini.” Kutakuwa na amani kati ya mnyama na
mnyama.Simba atakula majani, chui atalala pamoja na mwanambuzi, simba na
ng’ombe watakula pamoja.Nyoka hawatakuwa na madhara tena (Isaya 11:6-9).
Hakutakuwa na wizi au unyang’anyi.Wakati huo hakutakuwa na haja ya kufunga
milango na makufuli
(Ezekieli 34:25-28).
VITA VYA GOGU NA MAGOGU.
Mwishoni mwa
miaka elfu moja, shetani atafunguliwa kutoka kifungoni, na ataanza kuwadanganya
watu wote na kuwashawishi ili wafanye vita na kupigana na Yesu pamoja na
watakatifu wake. Watu wote kwa kuwa wana asili ya dhambi watashawishika na
waasi watajikusanya nchi ya Gogu na Magogu iliyo Kaskazini ya Palestina
mashariki ya kati na kuja kuishambulia maskani kuu ya watakatifu yaani
Yerusalemu. Hapo ndipo itatokea vita vya Gogu na Magogu. Hasira ya Mungu
itawaka na wanadamu wote wataangamizwa kwa kuliwa na moto utakaoshuka kutoka
mbinguni. Watasalia tu watakatifu pamoja na Yesu. Shetani naye atakamatwa na
kutupwa katika ziwa la moto (Ufunuo 20:7-10). Wale wote walioliwa na
moto, watakuwa wote Jehanamu ya moto kusubiri ufufuo wa pili au ufufuo wa
hukumu.
Je ungependa kutawala pamoja na Yesu Duniani?
(Ufunuo 20:6).
JEHANUM YA MOTO.
Watu wengi,
mamekuwa wakijiuliza kwamba, Je, watu wanaokufa katika hali ya dhambi
wanakwenda wapi? Jibu ni kwamba wanakwenda Jehanum ya moto na
ndiyo maana Bwana wetu Yesu Kristo anatufundisha waziwazi kuhusu Jehanum ya
moto akituonya kumuogopa Mungu mwenye uwezo wa kututupa Jehanum. Anaendelea
kutuonya kwamba ni heri kukubali lolote lile litupate kuliko kwenda kwenye
mateso makali ya Jehanum. Katika kitabu cha Luka 12:5 Biblia
inasema, “Lakini nitawaonya mtakayemuogopa; mwogopeni yule ambaye akiisha
kumuua mtu ana uweza wa kumtupa katika Jehanum, naam nawaambia mwogopeni huyo.”
Soma pia (Mathayo 5:2, Mathayo 5:29-30). Maandiko pia yanaendelea
kusisitiza kwa msisitizo mkubwa kwamba ni jambo la kutisha kuanguka katika
mkono wa Mungu aliyehai na kutupwa katika Jehanam ya moto (Waebrania 10:26 –
31).
Jehanum ya
moto inaitwa pia “kuzimu”. Katika kitabu cha Zaburi 9:17 Biblia
inasema, “Wadhalimu watarejea kuzimu, naam mataifa yote wanaomsahau Mungu.”
Jehanum ya moto pia inaitwa “Tofethi”; katika kitabu cha Isaya
30:33 Biblia inasema, “Maana tofethi imewekwa tayari tokea
zamani, naam imewekwa tayari kwa mfalme huyo; ameifanya kubwa, inakwenda chini
sana, tanuru yake ni moto na kuni nyingi pumzi ya Bwana, kama moto wa kiberiti
huiwasha”Kamwe hatupaswi kulipuuzia jambo hili na kulifahamu jambo hili
kijuujuu tu. Hivyo basi ningeomba uendelee kufuatana nami ili uweze kujifunza
kwa undani sana kuhusu eneo hili la hatari sana.
HUKUMU BAADA YA KUFA.
Biblia
inaeleza waziwazi kwamba mtu anapokufa sekunde ileile ya kufa kwake anakabiliwa
na hukumu, katika kitabu cha Waebrania 9:27 Biblia inasema, “Na
kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja na baada ya kufa hukumu.”
Kuna watu wanafundisha kinyume na kweli ya neno la Mungu, hufundisha kwamba mtu
anapokufa analala tu na hakuna lolote la hukumu ya mara moja. Wanatumia
maandiko yanayozungumzia kulala kwa kuyatafsiri isivyo (Mathayo 27:52;
1Wakorintho 15:20; Yohana 11:11 – 14) na pia huwadanganya watu kwa kusema
kuwa wafu hawajui lolote kwa kutumia maandiko kama Mhubiri 9:5.
Ukweli ni
kwamba, kinachobaki kaburini ni mwili tu, Nafsi na roho ya mtu huondoka na
kuvalishwa mwili mwingine kabisa kama Biblia inavyosema katika1Wakorintho
15:40, “Tena kuna miili ya mbinguni na miili ya duniani, lakini
fahari yake ile ya mbinguni ni mbali na fahari yake ile ya duniani ni mbali.”Mwili
unaobaki kaburini ndiyo ambao umelala haujui lolote na hauna kumbukumbu, lakini
pasipo mwili huo, mtu atamwona Mungu ikiwa ameishi katika mapenzi yake (Ayubu
19:26). Mwili hubaki kaburini lakini roho ya mtu huondoka (Muhubiri 12:7).
Ikiwa mtu ameishi katika mapenzi ya Mungu, mara tu baada ya kufa huchukuliwa
mbinguni na malaika kwa kutumia magari maalumu ya mbinguni,katika kitabu cha
Zaburi 68:17 Biblia inasema, “Magari ya Mungu ni
ishirini elfu, maelfu maelfu; Bwana yumo kati yao kama katika Sinai katika
patakatifu”.Soma pia (Luka 16:22; 2Wafalme 2:11-12). Lakini
ikiwa mtu huyu ameishi katika dhambi hukumu yake huwa kutupwa katika Jehanam ya
moto mara baada ya kufa (Mithali 9:13-18; Isaya 5:11-15; Mithali 7:24-27).
JEHANUM YA MOTO IKO WAPI?
Mara mtu
anapokufa tu huwa kwenye njia panda. Kila mmoja hupenda kwenda mbinguni hata
hivyo ikiwa jina lake halimo katika kitabu cha uzima cha mbinguni, hulazimika
kwenda Jehanum ya moto. Mtu anayetakiwa kwenda Jehanam ya moto huchachamaa na
kukataa kwenda kwenye njia mbaya inayotisha ya motoni na hulazimika kukamatwa
na kutupwa Jehanam kwa nguvu (Ufunuo 19:20; Ufunuo 20:10).Kuzimu au
Jehanam ya moto ipo chini yaani pande za chini za nchi, katika kitabu cha Mithali
15:24, Biblia inasema, “Kwa mtu mwenye akili njia ya uhai huenda juu,
ili atoke katika kuzimu chini.”(Zaburi 63:9; Ezekieli 31:14)
HALI HALISI YA JEHANUM YA MOTO NA WALE WALIOKO HUKO.
Jehanum ya
moto ni shimo kubwa na refu sana lililojaa moto. Moto huu huwashwa mfululizo
kwa pumzi ya Bwana (Isaya 14:15; Isaya 30:33). Moto huu ni mkali
sana kuliko moto wowote tunaoufahamu hapa duniani, uwe wa gesi, umeme, makaa ya
mawe au lolote jingine, kitabu cha Waebrania 10:27 Biblia
inasema, “Bali kuna kuitazama hukumu yenye kutisha na ukali wa moto ulio
tayari kuwala wao wapingao.” Moto huu ni mweusi sana unaosababisha giza
na kufanya mtu awaone wenzake wachache tu wa karibu naye (Mathayo 8:11-12;
Yuda 1:6). Moto huu una uwezo wa kula na kutafuna, hivyo huwala na
kuwatafuna wale walioko motoni na kufanywa milio mikubwa kama milipuko ya
mabomu. Wakati wote watu walio katika moto huu ndimi zao huwa ziko nje kama
mbwa wakitamani wadondoshewe angalau tone la maji, kitabu chaLuka 16:23-24 Biblia
inasema, “Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake alipokuwa katika mateso
akamwona Ibrahimu kwa mbali na Lazaro kifuani mwake Akalia, akasema Ee baba
Ibrahimu nihurumie umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini
auburudishe ulimi wangu kwa sababu ninateswa katika moto huu.”Hata
hivyo, kama jinsi ambavyo chumvi inavyozuia nyama kuharibika, vivyo hivyo na
moto huu humtafuna mtu lakini hamaliziki (Marko 9:43-49) Huu ni moto wa
milele (Mathayo 25:41).
MAFUNDISHO POTOFU JUU YA MOTO WA MILELE.
Kuna
mafundisho potofu yanayowafariji watu na kusema eti mtu ataunguzwa na moto na
kutoweshwa au kupotea na kuangamia kabisa na hivyo kufikia mwisho. Haya ni
mafundisho potofu yanayoletwa na shetani kupitia watu fulani ili kuwadanganya
watu. Wanatumia maandiko kama Mathayo 10:28(kuangamizwa) na Yohana
3:18 (Kupotea). Kuangamizwa hakumaanishi kutoweka kabisa kama
alivyolitumia neno hili Esta wakati anataka kwenda kuonana na mfalme (Esta
4:16). Mfano Kondoo akipotea haimaanishi hayupo kabisa bali ametengwa na
mchungaji (Isaya 57: 1-3). Kadhalika neno “Kuharibu” linapotumika
kuhusiana na adhabu ya milele halina maana ya kufanya kitu kisiwepo bali ni
kuadhibu vikali (1Wakorintho 3:16-17).
Walimu hawa
wa uongo hufundisha pia kwamba ati watu watatoweshwa kama moshi baada ya
kuungua na wanatumia andiko la Zaburi 37:20; Kutoweshwa hapa ni
kutenganishwa mbali na Mungu. Pia wapo wanaojifariji kwa kusema kuwa Mungu
hawezi kumchoma moto mwanadamu kwani yeye ni Mungu wa huruma, hivyo wenye
dhambi watahurumiwa. Ni kweli Mungu ana huruma sana, lakini ni wakati huu ambao
unahubiriwa injili ili upate kutubu wakati ukiwa duniani, lakini baada ya hapo,
ghadhabu ya Mungu itamkalia kila aliyetenda dhambi. Angalia gharika ya Nuhu
katika kitabu cha Mwanzo 7:1-24 jinsi Mungu alivyowaharibu
wanadamu wote wakubwa kwa wadogo na akabaki Nuhu na familia yake. Pia angalia
miji ya Sodoma na Gomora (Mwanzo19:1-26).Mungu alivyoiharibu kwa moto na
akapona Ruthu na watoto wake tu na katika miji hiyo walikuwepo wakubwa kwa
watoto.
MAKALI YA JEHANUM YA MOTO.
Moto huu wa
milele huambatana na madini yanayoitwa kiberiti au kwa lugha ya kitaalamu
yanaitwa “Sulphur”. Madini haya yakiwaka huwa kama mpira na hutoa harufu
mbaya kama mayai viza (mayai yaliyooza). Harufu ya namna hii inaifunika kuzimu
yote. Lakini pia katika moto huu wamo funza maalum ambao huwatafuna watu na
kuifanya miili yao iwe na matundu mengi na funza hawa huingia katika miili yao
na kutoka. Hii hufanya miili ya watu na sura zao kuwa mbaya mno kama madude ya
kutisha! (Isaya 14:11; Marko 9:43-49; Isaya 66:24). Kutokana na moto huu
kuwa mweusi hufanya miili yao kuwa myeusi kama mkaa. Watu walioko motoni hujawa
na wakati wote na vilio na tena husaga meno yao kama mtu anayehisi baridi kali
sana (Mathayo 8:12), hivyo kuwafanya waonekane wamechakaa sana. Hakika
kuzimu ni pigo lifurikalo ambalo huwachukua wenye dhambi asubuhi, mchana na
usiku (Isaya 28:15, Isaya 28:18-19). Walioko motoni hujifahamu sana
zaidi hata walipokuwa duniani na kuwakumbuka ndugu, marafiki na majirani zao (Luka
16:19-24).
Juu ya yote
hayo, katika vilio vyao humwomba Mungu awahurumie na kuwasamehe lakini Mungu
mwenyewe amekwisha sema, “Nami jicho langu halitaachilia, wala sitaona
huruma”. (Ezekieli 9:10; Ezekieli 8:18)
USEMI NA FIKRA ZA WALE WALIOKO MOTONI.
11 Watu walioko motoni hutamani sana mtu
mmoja kati yao aje awashuhudie ndugu zao duniani ili waache dhambi na kukwepa
mateso yao (Luka 16:27-31).
12 Wale walioko motoni ambao walilijua
kweli neno la Mungu na wakateleza, husema maneno yafuatayo, “Jinsi
nilivyochukia maonyo na moyo wangu ukadharau kukemewa, wala sikuisikia sauti ya
waalimu wangu, wala sikuwategea sikio langu walionifundisha.”(Mithali
5:11-13).
13 Watu walioko motoni wakimwona mtu
yeyote ametumbukia huko waliko humwambia huku wanalia, “Je, wewe nawe
umekuwa dhaifu kama sisi! Wewe nawe umekuwa kama sisi!” (Isaya
14:9-10).
Lakini pia wale
watakaokuwepo mbinguni watapewa nafasi kidogo ya kuwaangalia waliopo motoni (Isaya
66:24), lakini hawatakuwa na huzuni wala machozi yoyote juu yao.
TOFAUTI KATI YA JEHANUM YA MOTO NA ZIWA LA MOTO.
Jehanum ya
moto ni tofauti kabisa na ziwa la moto linalotajwa katika Ufunuo
20:14-15; Ufunuo 21:8; kwa jinsi ileile mbingu ya sasa
ilivyo tofauti na mbingu mpya inayotajwa katika Ufunuo 21:1. Ziwa
la moto kwa sasa halina mkazi ndani yake. Watakaokuwa wa kwanza kuingia humo
watakuwa Mnyama (Mpinga Kristo) na nabii wa uongo (Ufunuo 19:20). Kisha
atafuata Ibilisi ambaye atatupwa humo baada ya vita vya Gogu na Magogu (Ufunuo
20: 7-10). Baada ya hapo kutafuata hukumu ya kiti cha enzi cheupe kikubwa.
Hukumu hii itatolewa baada ya ufufuo wa pili au ufufuo wa hukumu ambao
utawafufua walioko Jehanam ya moto. Baada ya hawa kuelezwa kwa nini
wamehukumiwa adhabu ya mateso ya milele ndipo watakapotupwa katika ziwa la
moto. Mateso yaliyoko katika ziwa la moto ni zaidi sana kuliko mateso ya
Jehanam ya moto. Ni kama Jehanam walikuwa mahabusu na sasa wanapelekwa
gerezani. Kama mbingu mpya itakavyokuwa nzuri zaidi kuliko mbingu ya sasa, vivyohivyo
ziwa la moto litakuwa na mateso yaliyokithiri kuliko Jehanum ya moto, maana
mauti na kuzimu vyote vitatupwa humo (Ufunuo 20:14).
JINSI YA KUIKWEPA JEHANUM YA MOTO.
1. Kuungama
dhambi na kuziacha (Mithali 28:13).
2. Kulishika neno la Mungu
kwa kufanya maagizo yote ya Mungu na kuwakataa wafariji wenye kutaabisha
wanaosema kufanya hili na lile siyo lazima (Yohana 8:5; Zaburi 119:6;
Ayubu 16: 1-2)
3. Kutoihesabu sheria kuwa
kitu kigeni. Kukubali kuongozwa na sheria ya Kristo. Hakuna mwanafunzi
asiyeishi kwa sheria. (Hosea 8:12; Wagalatia 6:2; Isaya 8:16)
4. Kuwa mtakatifu na
kutoifuatisha namna ya dunia hii katika mavazi, usemi, matendo n.k (Waebrania
12:14; Warumi 12:2; Yakobo 4:4; 1Yohana 2:15-17).
Je nawe utakuwa dhaifu kama walio Jehanam ya moto
(Isaya 14:9-10).
UFUFUO WA WAFU.
Mtu
anapokufa moja kwa moja anakwenda kukutana na hukumu yake (Waebrania 9:27).
Kama mtu amekufa akiwa ameokoka na kuishi katika utakatifu mpaka dakika yake ya
mwisho, sekunde ileile anakwenda peponi (Luka 23:39-43; Matendo 7:54-59;
Wafilipi 1:21-23). Ikiwa mtu amekufa akiwa hajaokoka sekunde ileile
anakwenda katika mateso ya moto wa Jehanum (Luka 16:19-28). Ingawa mwili
wa mtu anayekufa unabaki kaburini, roho yake pamoja na nafsi yake vinaambatana
na mwili mpya kwa kuwa kuna miili ya duniani tena kuna miili ya mbinguni (1Wakorintho
15:40-44; Ayubu 19:25-27; Mhubiri 12:7). Katika mwili mpya, mtu anakwenda
motoni au mbinguni. Akiwa huko atajijua kabisa. Atakuwa anaona, kuhisi, kusikia
na kuwa na kumbukumbu hata ya ndugu zake waliobaki duniani (Luka 16:27-31)
UHAKIKA WA UFUFUO WA WAFU.
Ufufuo wa
wafu ni moja ya masomo ya msingi sana katika ukristo na pia ni mafundisho ya
kwanza ambayo kila mkristo inampasa kuyafahamu (Waebrania 6:1-2). Kiyama
cha wafu au ufufuo wa wafu, umetabiriwa mapema katika neno la Mungu kwenye
vitabu vya Luka 14:13-14; Yohana 5:28-29; Wafilipi 3:10-11; 1Wathesalonike
4:16. lakini hata hivyo, Yesu Kristo ndiye kielelezo cha ufufuo wa wafu na
uhakika wa ufufuo wa wafu kwa watu wote. Katika kitabu cha1Wakorintho 15:20,
Biblia inasema, “Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu limbuko lao
waliolala.” Yesu Kristo alitabiri mapema juu ya kufufuka kwake kabla
hata hajafa (Mathayo 16:21; Mathayo 17:22-23, Mathayo 20:17-19; Marko
8:31-32, Marko 10:32-34; Luka 9:20-22, Luka 18:31-34), lakini kutokuamini
kwa wayahudi hakukuzuia kufufuka kwa Yesu, vivyo hivyo hata leo pamoja na
kuwepo kwa watu wasioamini kwamba kutakuwa na ufufuo wa wafu, kutokuamini kwao
hakutaweza kuzuia jambo hilo kutokea (Warumi 3:3-4). Uongo wa askari
walinzi wa kaburi la Yesu walioutawanya baada ya kupokea rushwa na kufundishwa
kusema uongo kwa kuambiwa, “Semeni ya kwamba wanafunzi wake walikuja
usiku, wakamwiba, sisi tulipokuwa tumelala”, ni uongo ulio dhahiri (Mathayo
28:11-15). Ikiwa walinzi walikuwa wamelala usingizi waliwaona namna gani
watu waliokuja kuuiba mwili wa Yesu na kufahamu kwa hakika ni wanafunzi wake?
Na kama waliwaona kwa nini waliwaacha wakauiba mwili huo na wasiwazuie kufanya
hivyo?. Ni uongo ulio wazi. Ni jambo lililo dhahiri kwamba Yesu alifufuka! Kwa
jinsi hiyohiyo, ufufuo wa wafu wote ni jambo lililo dhahiri kabisa kutokea.
UFUFUO WA WAFU UNAVYOFANYIKA.
Ufufuo wa
wafu ni kama kuvua nguo mpya na kuvaa nguo ya zamani. Kwa jinsi ambavyo mtu
alivyokufa na kuacha mwili wake duniani, ndivyo itakavyokuwa tena. Katika
ufufuo wa wafu mtu atatoka katika Jehanam ya moto na kuurudia mwili wake wa
duniani au atatoka peponi au mbinguni na kuurudia mwili wake wa duniani. Hata
kama mwili ule umekuwa udongo baada ya miaka mingi ni muhimu kukumbuka kwamba
Mungu aliyemuumba mwanadamu kutoka katika mavumbi, hashindwi kufanya mwili
uliokuwa udongo urudie hali ya mwili tena (1Wakorintho 15:42-44).
AINA ZA UFUFUO WA WAFU.
Katika mpango wa Mungu wa
ufufuo wa wafu, kuna aina mbili za ufufuo wa wafu;
1: Ufufuo wa kwanza au
ufufuo wa uzima.
Ufufuo huu
umepewa majina mengine pia katika Biblia kama ufufuo ulio bora au ufufuo wa
wenye haki (Yohana 5:28-29; Ufunuo 20:4-6; Luka 14:13-14; 1Wathesalonike
4:16; Waebrania 11:35). Ufufuo wa kwanza unajumuisha wale wote waliokufa na
kwenda mbinguni yaani wenye haki au watakatifu. Hawa ndiyo wenye sehemu katika ufufuo
wa kwanza. Huu ni ufufuo wa uzima kwa sababu wale wote watakaokuwa katika
ufufuo huu watakuwa katika uzima wa milele katika mbingu mpya na nchi mpya. Huu
ndiyo ufufuo ulio bora. Ufufuo huu umegawanyika katika sehemu mbili.
(a) Ufufuo wa
watakatifu wote walio mbinguni wakati wa kunyakuliwa kwa kanisa.
Hawa watafufuliwa kwanza
kisha kufumba na kufumbua miili yao itabadilishwa na kuwa ya utukufu kisha wote
kwa pamoja watakwenda kumlaki Bwana Yesu mawinguni (1Wathesalonike 4:16).
(b) Ufufuo wa
watakatifu wa wakati wa dhiki kuu.
Hawa ni watakatifu ambao
hawakumsujudia yule mnyama yaani mpinga Kristo wala sanamu yake na kukataa
kabisa kupokea chapa ya 666 katika vipaji vya nyuso zao na hivyo kuteswa na
kuuawa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu na neno la Mungu wakati wa dhiki kuu. Hawa
watafufuliwa wakati wa kuja kwa Yesu Kristo mara ya pili pamoja na watakatifu
wake walionyakuliwa. Watakatifu hawa baada ya kufufuliwa huku moja kwa moja
watatawala pamoja na Kristo miaka elfu moja duniani (Ufunuo 20:4-6).
2: Ufufuo wa pili
au ufufuo wa hukumu.
Ufufuo huu
pia unaitwa ufufuo wa aibu na kudharauliwa (Yohana 5:29; Danieli 12:2).
Huu ni ufufuo wa watenda mabaya au wenye dhambi wote ambao watakuwa Jehanam
hivi sasa hadi wale watakaokwenda huko baada ya vita vya Gogu na Magogu
itakayofanyika mwishoni mwa miaka elfu ya utawala wa Yesu Kristo duniani,
ambayo itawamaliza wenye dhambi wote na kisha waende wote motoni. Wote hawa
watafufuliwa katika ufufo huu wa pili utakaofanyika muda mfupi baada ya miaka
elfu ya utawala wa Kristo miaka elfu duniani. Walipokwenda motoni walikuwa
hawajaelezwa waziwazi makosa yaliyowapeleka motoni sasa hapa ndipo Yesu Kristo
mhukumu wa haki atakapo waonyesha waziwazi mbele ya watu wote. Hapa ndipo watu
watajitetea, “Bwana Bwana hatukufanya unabii kwa jina lako na kwa jina
lako kutoa pepo …………” naye Yesu mhukumu wa haki atawaambia
dhahiri, sikuwajua ninyi kamwe! ondokeni kwangu ninyi mtendao maovu wote
watatupwa kwenye ziwa la moto.
Je baada ya maisha ya duniani utakuwa katika ufufuo upi?
HUKUMU YA MWISHO
Baada tu ya
vita vya Gogu na Magogu vitakavyofanyika mwishoni mwa miaka elfu moja ya
utawala wa Yesu Kristo duniani, kutafuata ufufuo wa pili unaoitwa pia ufufuo wa
Hukumu (Yohana 5:28-29). Huu ni ufufuo wa wale waliotenda mabaya, yaani
wote wenye dhambi waliokufa pasipo utakatifu, tangu nyakati za mwanzo kabisa za
vizazi vya Adamu hadi wale wote watakaoliwa kwa moto kwenye vita vya Gogu na
Magogu (Ufunuo 20:7-9). Hawa wote baada ya kufa kwao wamekuwa katika
kipindi chote hicho kwenye mateso makali katika Jehanam ya moto. Hawa
watafufuliwa na kurudia miili yao ya asili na kusimama mbele ya kiti cha enzi
kikubwa cheupe cha hukumu.
HAKIMU ATAKAYEHUKUMU.
Hakimu huyu
ni Yesu Kristo. Maandiko yanaelezea jambo hili waziwazi, Biblia inasema katika
kitabu cha Yohana 5:22, “Tena Baba hamhukumu mtu yeyote, bali
amempa Mwana hukumu yote.” Neno la Mungu pia linasema katika 2Timotheo
4:1, “Nakuagiza mbele za Mungu,na mbele za Kristo Yesu,
atakayewahukumu walio hai na waliokufa ;kwa kufunuliwa kwake
na kwa ufalme wake.” Soma pia (Matendo 10:36; Warumi 2:16).
Wakati wa
hukumu, Bwana Yesu atakikalia kiti cha enzi kikubwa cheupe cha hukumu. Hivyo
yeyote anayemkana Yesu leo kuwa siyo Mungu atafahamu hapa kwamba hukumu yote
iko chini yake (Yohana 5:22; Matendo 10:38-41, Warumi 2:16; 2Timotheo
4:1). Ni heri kufahamu mapema hivi leo kwamba Yesu ndiye hakimu na kuomba
msamaha kwake, yeye yuko tayari na kurehemu na kusamehe kabisa (Isaya 55:6-7).
Yesu atakapokikalia kiti cha enzi kikubwa cheupe atakuwa mwenye hasira, huruma
itakuwa mbali naye kabisa (Ezekieli 7:4, Ezekieli 8:18; Warumi 2:4-5).
LENGO LA HUKUMU HII.
Hukumu hii
haitakuwa na lengo la kuwaweka huru wenye dhambi fulani. Hivyo ni kwamba yeyote
yule asiyemwamini Yesu hadi kufa kwake ghadhabu ya Mungu inamkalia kama Biblia
inavyosema katika Yohana 3:36, “Amwaminiye mwana yuna uzima
wa milele, asiye mwamini Mwana hatauona uzima bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.”
Kawaida mtu yeyote mwenye dhambi anapokufa huenda motoni moja kwa moja. Mtu
huyu huenda huko bila kuelezwa ni kwa nini anapelekwa kwenye mateso hayo.
Makusudi ya hukumu hii itakuwa kumfahamisha kila mmoja aliye katika mateso ya
Jehanam uhalali wa yeye kupewa hiyo adhabu ya milele. Itadhihirishwa kwa kila
mmoja kwamba adhabu ya moto wa milele ni malipo halisi aliyoyapata kadri ya
matendo yake (Warumi 2:6). Yesu hapa anasimama kama mhukumu wa
haki kama Biblia inavyotueleza katika Matendo 17:31, “Kwa
maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki …………….”
IDADI KUBWA YA WATU WATAKAOHUKUMIWA.
Watu
wanaokwenda Jehanam ni wengi sana kuliko wengi wanavyofikiria (Mathayo
7:13-14). Mbinguni kuna vitabu vya aina mbili; Kitabu cha uzima ambamo
huandikwa majina ya wale waliookoka ambao hudumu kutenda mapenzi ya
Mungu,katika kitabu cha Luka 10:20 Biblia inasema, “Lakini
msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii, bali furahini kwa sababu majina yenu
yameandikwa mbinguni.” Soma pia (Wafilipi 4:3). Wale waliookoka
wasiodumu kutenda mapenzi ya Mungu, hufutwa majina yao na kuondolewa katika
Kitabu cha uzima, kitabu cha Kutoka 32:33 Biblia inasema, “BWANA
akamwambia Musa, mtu yeyote aliyenitenda dhambi ndiye nitakayemfuta katika
kitabu changu”.Soma pia (Ufunuo 3:5).
Wale wote
watendao dhambi na kuwa mbali na wokovu majina yao yamo katika vitabu vya
kumbukumbu vya hukumu. Kwa kuwa watu hawa ni wengi sana, majina yao yapo katika
vitabu vingi, lakini wale wa mbinguni wapo katika “Kitabu kimoja cha
uzima” (Ufunuo 20:12). Kamwe hatupaswi kudanganyika kutokana na
watu wengi wanaosema wameokoka huku maisha yao hayako nuruni na kufikiria
kwamba wote hawa wataingia mbinguni. Gharika iliwaangamiza wote duniani na
kubakiza wanane tu Safinani. Viwango vya Mungu vya utakatifu havibadiliki (Mathayo
5:48; Waebrania 12:14; 1Petro 1:15-17).
WATOTO WADOGO PIA KUHUKUMIWA.
Wakubwa kwa wadogo
watakuwepo kwenye hukumu hii, kama Biblia inavyosema katika kitabu cha Ufunuo
20:12, “Nikaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho
kiti cha enzi na vitabu vikafunguliwa na kitabu kingine kikafunguliwa ambacho
ni cha uzima na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika
vile vitabu, sawasawa na matendo yao.” Ni muhimu kuwashuhudia injili
watoto wetu wadogo walio na akili ya kujua mema na mabaya na kuwapa nafasi ya
kutubu na kuokolewa au sivyo tutahuzunika kuwaona wakiwa kwenye hukumu hii,
wakiwa wametoka kwenye mateso ya moto. Kwa mtoto mdogo anayeweza kufahamuhesabu
ya 59 + 68, ana upeo mkubwa wa kufahamu mema na mabaya. Katika injili yetu
kwa watoto wa jinsi hii tunatakiwa kutaja dhambi wanazoweza kuzielewa kama vile
wizi wa penseli, uongo, kutokuwatii wazazi, kiburi, ukaidi n.k. Ni muhimu
kukumbuka kwamba ni watoto wadogo kabisa wasiofahamu sheria ambao ufalme wa Mungu
ni wao umri wa kukumbatiwa (Marko 10:13-16; Warumi 4:15; 5:13).
KIPIMO KITAKACHOTUMIWA KATIKA HUKUMU.
Watu wengi
wanafanya makosa makubwa sana pale wanapojifariji na kufikiria kwamba
watakwenda mbinguni kutokana na kufanya mambo yaliyo sawa na mafundisho ya
madhehebu yao au wachungaji wao. Hiki siyo kipimo kitakachotumiwa na Yesu
katika kuhukumu. Wengi wanaojifariji kwa kutenda yaliyo halali kwa wachungaji,
manabii, mitume, walimu au wainjilisti au madhehebu yao, ingawa yapo tofauti na
maagizo ya neno la Mungu, watakwenda katika mateso ya moto wa milele.
Kipimo atachotumia
Yesu katika hukumu ni neno la Mungu kama Biblia inavyosema katika Warumi
2:16,”Katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu sawasawa
na injili yangu kwa Kristo Yesu.”Ni jambo la msingi sana kulinganisha
yale tunayofanya au kuyafundisha na neno la Mungu na siyo na mafundisho ya
madhehebu yetu au wachungaji na maaskofu wanaotuambia kufanya hili na lile siyo
lazima (Utafikiri wanambingu ya kukupeleka), wakati neno la Mungu linatuambia,
“Ndipo mimi sitoaibika nikiyatafuta maagizo yako yote” (Zaburi
119:6). Siyo hilo tu, kwa vile kipimo cha Yesu katika hukumu kitakuwa ni
neno la Mungu hivyo wale ambao waliokaa katika makanisa ambayo hayakuwa na
mafundisho pamoja na wale ambao walikatazwa na wazazi wao kuwa wakristo, wote
hawa watapotea pasipo sheria. Kukosa kuifahamu yaliyo halali, siyo udhuru
utakaokubalika, kwani kama uliweza kuwa na juhudi katika kutafuta chakula cha
mwili ulishindwa nini kutafuta chakula cha kiroho, pia kama uliweza kuwa na
juhudi ya kutafuta elimu ya duniani, ulishindwa nini kuwa na juhudi ya kutafuta
kuyajua mapenzi ya Mungu. Wale wanaofahamu mafundisho ya kweli lakini
hawayatendi na kuyafundisha, watapigwa sana yaani kuteswa zaidi kuliko wale
ambao hawakuyajua, kama maandiko yanavyosema katika kitabu cha Luka
12:48, “Na yule asiyejua naye amefanya yastahiliyo mapigo atapigwa
kidogo. Na kila aliyepewa vingi; kwake huyo vitatakwa vingi; kwake huyo
watataka na zaidi.” Soma pia (Warumi 2:11-14; Walawi 5:17). Mungu
anamtarajia kila mwanadamu kuyatafuta mafundisho ya kweli hata iwe mbali kiasi
gani kama alivyotayari kuifuata elimu Ulaya au biashara nchi za nje. Katika
kitabu cha Mathayo 12:42 Biblia inasema, “Malkia wa
kusini atasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki naye atawahukumu
kuwa wamekosa kwa sababu yeye alikuja kutoka pande za mwisho za dunia ili
asikie hekima ya Sulemani na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani.”
Hivyo, hata kama eneo ambalo wanafundisha kweli lipo mbali nawe anza kutia bidii
kuanzia leo, ili usije ukahukumiwa kwa ushuhuda wa Malkia wa kusini.
KUFUNULIWA KWA SIRI ZOTE MBELE YA MASHAHIDI WA MUNGU.
Mwenye
dhambi mmoja baada ya mwingine, watasimama mbele ya kiti cha enzi kikubwa
cheupe. Mahali hapo itakuwa mahali pa aibu na kudharauliwa (Danieli 12:2).
Kila mmoja ataonyeshwa matendo yake, maneno yake, mawazo yake na nia yake kwa
mfano wa video iliyotunza kumbukumbu zake. Siri zote za wanadamu zitakuwa wazi
mahali hapo. (Mithali 26:26; Mhubiri 12:14; Luka 12:2; 1Wakorintho 4:5;
Ayubu 20:27). Mahali hapo tutawaona wachungaji na maaskofu wazinzi na
wataonyeshwa wazi wazi wakifanya tendo la uzinzi na wenzao, ingawa tuliwajua
kuwa watakatifu. Hatua zote za mtu za kumshawishi mwanamke wa mtu hadi kufanya
naye uzinzi, vyote vitaonyeshwa. Jinsi unavyotamani wake au waume za watu vyote
vitaonyeshwa kwa mfumo wa video na watu wote wataona uchafu huo. Lolote lile
lililo ovu ambalo lilifanywa pasipo watu kujua, siku hiyo litajulikana. Hakika
itakuwa ni aibu kubwa sana. Maneno yote mtu anayotamka yatawekwa wazi hapo na
kwa mtu anayotamka yatawekwa wazi hapo na kwa kila neno mtu atahukumiwa (Mathayo
12:36-37). Mtu aliyekuwa anahudhuria mikutano ya injili bila kukata shauri
kuokolewa atajiona picha yake akiwa katika mikutano hiyo na atajiona anasema “Siwezi
kuokoka”. Wale walioshindwa kufanya hili na lile kwa visingizio kuwa ni
wanajeshi, ni vijana wadogo n.k. wataona mashaidi wa Mungu waliofanya
waliyokataa kuyafanya wakiwa na hali kama zao. Watakatifu watakuwepo kuona kila
kitu na kuwa mashahidi wa Mungu (Waebrania 12:1; Mathayo 12:42; Malaki 3:18;
Malaki 4: 1-2).
HUKUMU YA MWISHO.
Watu watalia
na kujitetea, wanaojiita manabii, wachungaji, mitume, wainjilisti watalia na
kusema "Mimi nilifanya miujuza kwa jina lako" wengine
watajitetea mimi nilitoa pepo kwa jina lako kadhalika wengine watajitetea
"Mimi nilishuudia na kufuatilia" n.k, lakini Yesu
atasema "Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu"
(Mathayo 7:22-23). Kila mtu atatolewa hapo na kukamatwa kwa nguvu kisha
atatupwa kwenye ziwa la moto (Ufunuo 20:15). Ziwa la moto ni tofauti na
Jehanum ya moto (Kuzimu). Ziwa la moto kwa sasa halina mtu yeyote ndani yake,
wa kwanza kutupwa humo watakuwa mnyama (Mpinga Kristo) na nabii wa uongo (Ufunuo
19:20). Kisha atafuata shetani (Ufunuo 20:10). Mateso ya ziwa la
moto ni mazito zaidi kuliko Jehanamu, kama jinsi mtu anavyotolewa mahabusu na
kutupwa gerezani. Mauti na Jehanamu (Kuzimu) ya sasa vyote pia vitatupwa katika
ziwa la moto pamoja na wenye dhambi wote (Ufunuo 20:14-15, Ufunuo 21:8).
Hapo itakuwa ni kwa heri ya kutoonana tena kwa wenye dhambi na watakatifu.
Watumishi waliokuwa wanafundisha watu uongo kwa kusudi la kuwafariji watu
watakumbuka na kujuta sana.
Wakati wa kwaheri ya kutoonana utakuwa katika kundi lipi?
MBINGU MPYA NA NCHI MPYA.
Baada ya
kujifunza masomo mengi kwa mfululizo kuhusu matukio ya mwisho wa dunia katika
sura zilizopita, sasa katika sura hii tunakwenda kujifunza somo la mwisho
kabisa katika mfululizo huu. Baada tu ya hukumu ya kiti cha enzi kikubwa
cheupe, ndipo utakapofuata "MWISHO WA MIISHO YOTE" yaani kuharibiwa
kwa dunia ya sasa na mbingu ya sasa ili tupate mbingu mpya na nchi mpya.
KUUNGUZWA NA KUFUMULIWA KWA MBINGU NA NCHI YA SASA.
Mara tu
baada ya hukumu ya kiti cha enzi kikubwa cheupe, ndipo utakapofuata mwisho wa
miisho yote. Bwana wetu Yesu Kristo katika mafundisho yake alirudia tena na
tena akieleza kwamba, mbingu na nchi za sasa zitapita. Katika kitabu chaMathayo
24:35 Biblia inasema, "Mbingu na nchi zitapita lakini
maneno yangu hayatapita kamwe."Soma pia (Marko 13:31; Luka
21:33), hivyo basi wakati wa tukio hilo ndiyo huu. Pia tangu mapema kabisa
Mungu wetu anatufundisha kwamba, mbingu na nchi za sasa zitachakaa na kuaribiwa
na kama mavazi Mungu atazibadilisha kama tunavyoweza kusoma katika Zaburi
102: 25-26, "Hapo Mwanzo uliutia msingi wa nchi na mbingu ni
kazi ya mikono yako. Hizi zitaharibika bali wewe utadumu Naam, hizi zitachakaa
kama nguo, Na kama mavazi utazibadilisha, Nazo zitabadilika.” Pia
tukiangalia katika kitabu cha Isaya 66:22 Biblia inasema,
"Kama vile mbingu mpya na nchi mpya nitakazofanya zitakavyokaa mbele
zangu asema BWANA, ndiyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa" (Isaya
65:17; 2Petro 3:13; Ufunuo 21:1-7). Mbingu mpya na nchi npya zitakuwa ni
nzuri mno, hakuna mfano wake uliowahi kuwako au utakao kuwako. Ufundi wote wa
uumbaji wa Mungu utaishia hapa.
Miji yote ya
dunia hii imebuniwa na kujengwa na wanadamu wenye upungufu wa ubunifu wa
michoro, fedha, vifaa n.k; Mbingu mpya ni mji uliobuniwa na mbunifu mkuu, Mungu
mwenyewe mwenye uwezo wote. Barabara zake sio lami bali dhahabu tupu.
SABABU ZA KUUNGUZWA NA KUFUMULIWA
KWA NCHI NA MBINGU ZA SASA.
Nchi ya sasa yaani
dunia hii au ulimwengu huu umechosha na kuchakaa mno baada ya kukaliwa na
mamilioni ya wenye dhambi wanaofanya machukizo mbele za Mungu. Dunia hii
imechakazwa kwa gharika wakati wa Nuhu na vita vya kila namna mpaka vita ile ya
mwisho ya “Gogu na Magogu”. Miti yake mizuri imetumika kutengeneza sanamu za
kuabudu, pia hata kumsulubisha mwana wa Mungu katika mti, kila namna ya matambiko
na machukizo yanafanywa ulimwenguni. Damu za watu zimemwagika kwa wingi wake,
tangu damu ile ya Habili. Dunia imejaa harufu ya damu na haifai kukaliwa tena.
Pia mbingu hizi zilizo juu yetu yaani anga na sayari vyote vimejaa rekodi ya
maneno ya wanadamu ya matusi na Lugha chafu za kumkufuru Mungu, vimejaa harufu
ya uzinzi na usherati na za matendo ya sodoma. Mbingu hii ya kwanza na ya pili
vyote havifai. Hata mbingu ya tatu yaani mbinguni aliko Mungu kwa sasa hakufai
pia. Hapa ndipo mahali palipotunzwa kumbukumbu zote za dhambi za wanadamu
katika vitabu vya hukumu kwa maelfu ya miaka. Rekodi au kumbukumbu hizi
zimeifanya mbingu hii pia kuchukiza haifai nayo!. Kwa hiyo Mungu atazikamata
nchi na mbingu hizi za sasa na kuziunguza na kila kitu ndani yake kitafumuliwa
na kutoweka kama moshi kwa mshindo mkuu (2Petro 3:7; 2 Petro 3:10-12; Isaya
51:6). Mamilioni ya tani za gesi za oksijeni, haidrojeni, Acetylene n.k,
zilizoko ulimwenguni na angani zitashika moto na madini ya kila namna
yatayeyuka. Kila kitu, majengo miti yote na vinginevyo kama bahari n.k, vyote
vitateketea na kuyeyushwa kabisa. Kisha vitatoweka kama moshi na kutoonekana
kabisa.
MAISHA KATIKA MBINGU MPYA (YERUSALEMU MPYA).
“Nami
nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa
Mungu, umewekwa tayari kama bibi harusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.” (Ufunuo
21:2). Yerusalemu inatokana na maneno ya kiebrania Y’ru-shalaim maana
yake “Misingi ya amani”. Hivyo Y’r-shalaim maana yake “Kuwekwa misingi
ya amani”. Pia Yerusalemu inatokana na maneno “Jireh-shalom”. Neno “Jire” maana
yake “atawapa” na neno “Shalom” maana yake “Amani”. Hivyo “Jire-shalom” maana
yake “Atawapa Amani”. Yerusalemu ya sasa, iliitwa hivyo kwa sababu ndipo ambapo
Yesu Kristo alipokuja kutuwekea misingi ya Amani kwa kutupatanisha na Mungu kwa
damu yake kisha akasema, “Amani nawaachieni, amani yangu nawapa”
(Yohana 14:27). Baada ya mtu kuwa na amani ya Mungu ipitayo fahamu zote,
hatimaye ataingia Yerusalemu mpya, mji uliojengwa juu ya misingi ya Amani.
Katika
kitabu cha Yohana 14:2, Yesu anasema katika mji huu kuna
“makao” mengi. Neno la Kiyunani linalotafsiriwa hapa “Makao” ni “Mone” lenye
tafsiri ya kiingereza “Mansion” katika Biblia ya tafsiri ya King James Version,
“Mansion” ni jumba kubwa la kifahari (mansion house). Vivyohivyo mbinguni kuna
majumba mengi ya kifahari. Kila mtu atakayeingia mbinguni atapewa “Kao” au
jumba mojawapo la kifahari la kuishi.
MUUNDO WA MJI WA YERUSALEMU MPYA.
(Ufunuo 21:11-27).
Mji huu una ukuta
mkubwa, mrefu wenye milango kumi na mbili (12) na majina yameandikwa ambayo ni
majina ya kabila kumi na mbili za Waisraeli. Upande wa mashariki milango
mitatu, upande wa magharibi milango mitatu, upande wa kasikazini milango mitatu
na upande wa kusini milango mitatu. Na ile milango kumi na miwili ni Lulu kumi
na mbili, kila mlango ni lulu moja. Madini ya Lulu yanapatikana duniani yana
umbo dogo sana kama mawe madogo tu na wala siyo ukubwa wa milango mikubwa kama
hii. Lulu ni aina fulani ya madini ya thamani kubwa sana ambayo hupatikana
katika wanyama fulani wa baharini wenye gamba au kobe aina ya chaza (Oyster).
Thamani ya Lulu moja ni karibu dola za kimarekani laki nne ($ 400,000) ambazo
ni sawa na Tsh. 270,000,000/=
Ukuta wa mji huu
una misingi kumi na mbili (12) juu ya misingi hiyo yameandikwa majina ya wale
mitume kumi na mbili wa Yesu. Mji huu marefu yake, mapana na kwenda juu ni
sawasawa yaani maili 1,500. Ukuta wake ni dhiraa 144 sawa na futi 300. kuta
zake zimejengwa na madini ya ajabu!. Dhahabu safi mfano wa kioo safi. Msingi wa
kwanza umejengwa kwa Yaspi, ambayo ni madini yanayonga’ara sana
yenye rangi ya kijani iliyochanganyika na bluu. Msingi wa pili umejengwa kwa yakuti
samawi, haya ni mawe ya bluu, mazuri sana yenye ugumu unaofanana na madini
ya almasi. Msingi wa tatu umejengwa kwa madini ya kalkedoni, haya
ni aina ya madini mazuri sana yenye rangi aina nne mbalimbali, yaani nyekundu
iliyochanganyika na njano,hudhurugi (Brown) iliyochanganyika na nyeusi, bluu
iliyochanganyika na nyeupe, na rangi ya maziwa. Msingi wa nne ni zumaridi,
haya ni madini yenye rangi ya kijani. Msingi wa tano umejengwa kwa madini ya Sardoniki,
madini yenye rangi ya bluu, nyeupe na nyekundu. Msingi wa sita umejengwa kwa akiki madini
yenye rangi ya damu. Na msingi wa saba umejengwa kwa madini ya Krisolitho, haya
ni madini yaliyo kama dhahabu ila yana rangi ya kijani iliyochanyika na njano,
msingi wa nane umejengwa kwa zabarajadi, haya ni madini maangavu
(transparent) yenye rangi ya bluu iliyochanganyika na kijani. Msingi wa tisa
umejengwa kwa Yakuti ya manjano, ni madini ya njano iliyochanganyika
na kijani, msingi wa kumi umejengwa kwa madini ya Krisopraso, haya
ni madini yenye rangi tatu pamoja yaani njano, kijani na bluu. Msingi wa kumi
na moja umejengwa na madini yaHiakintho.Na msingi wa kumi na mbili
umejengwa kwa madini ya amethisto,haya ni madini yenye rangi ya
zambarau, yenye bluu na wekundu ndani yake. Barabara za mji huu siyo lami bali
nidhahabu safi kama kioo.
Mji
hauhitaji jua wala mwezi kuangaza kwani utukufu wa Yesu unatosha! Hakuna usiku
humo! Maisha yatakuwa ya kupumzika (Ufunuo 14:13), furaha tele wala
hakuna maombolezo wala kilio (Ufunuo 21:4), katika mji huo kutakuwa na
kumwabudu na kumsifu Mungu tu (Ufunuo 19:1; Ufunuo 7:9-12; Ufunuo 5:11-14),
Leo tunafahamu kwa sehemu yale tu tuliyofunuliwa lakini tukifika mbinguni
tutajua yote (Kumbukumbu 29:29; 1 Wakorintho 13:12).
Pia mavazi meupe ya wale waliopo mbinguni hubadilikadilika rangi mara kwa mara
kutokana na rangi ya mwanga inayoakisi kutoka katika majengo,hivyo kufanya watu
kupendeza sana.Chemichemi za maji na mito ya maji ya uzima, inauzunguka mji.Pia
mbinguni kuna kula na kunywa, hakuna mauti wala maumivu au taabu(Luka
22:14-16,Luka 22:29-30; Ufunuo 2:17;Ufunuo 21:4-5;Ufunuo 14:13), Kuna
kuimba nyimbo za sifa na vinanda (Ufunuo 14:2-3;Ufunuo
15:2-4), Pia ufahamu wetu utaongezeka(1 Wakorintho 13:12).Kwa ujumla
mbinguni kuna mengi yasiyoweza kutamkika kwa lugha za duniani (2
Wakorintho 12:4).Majibu mengine ya maswali yako utayapata ukifika huko
mbinguni.
Yeye ashindaye atayarithi haya (Ufunuo 21:7).
NA: DR. GODWIN GUNEWE