Monday, December 7, 2015

HUDUMA YA KUWASOMESHA WATOTO WASIOJIWEZA

Nakusalimu katika Jina la Yesu Kristo. USCF-SJUT tunayo huduma ya kuwasomesha watoto wasiojiweza ambapo mpaka hivi sasa tunao watoto 3 tunao wasomesha na kuwalea Kiroho. Kati ya hao watoto 3, watoto 2 wanasoma kidato cha kwanza, mmoja anasoma shule ya Kikuyu sekondari iliyopo Dodoma na mwengine anasoma shule ya Mtwara Tech. sekondari iliyopo mkoani Mtwara na mwengine anasoma shule darasa la 4 shule ya msingi Kikuyu mkoani Dodoma ambae pia ni mlemavu wa ngozi (Albino).
Uongozi unapenda kukukaribisha wewe upendwaye na Yesu kutoa mchango wa fedha kiasi chochote kile kadri Mungu alivyokubariki kwaajili ya kuhakikisha huduma hii njema inasonga mbele. Kama huduma tunaendelea kujitahidi kuwasomesha watoto hawa lakini kwa wewe kushiriki kwako kutafanyika Baraka sana kama Mlezi wa watoto hawa.
Unaweza kutuma kiasi chochote cha fedha na kitapokelewa. Tuma kwa Mhazini USCF-SJUT (Trezia Mbukwa) kwenye namba za simu zifuatazo:-
Tigo-0652547094
Vodacom-0766607948.
Mungu wa Mbinguni akubariki sana kwa moyo wa utayari ulio nao. Hakika tunamwamini Mungu ataikumbuka sadaka yako. YAKOBO 1:27
Share:

USCF-SJUT NEWS

Designed by Joel Elphas @ 2015. Powered by Blogger.

Recent Posts