JE UMEJIANDAAJE KUKABILI MWAKA
2016?
Nakusalimu
katika Jina la Yesu Kristo. Heri ya Mwaka mpya 2016!
Ni
kawaida kwa watu wengi kila ifikapo mwanzo mwa mwaka mpya kufanya maandalizi
mbalimbali eidha binafsi, familia, ukoo, taasisi na hata nchi. Wengine huanza
maandalizi mwishoni mwa mwaka uliokwisha na wengine hufanya mwanzoni mwa mwaka
mpya. Ni jambo jema kufanya maandalizi ya kukabili mwaka kwani hukuandaa kuishi
sawasawa na ulivyokusudia.
Lakini
Je kama Mkristo umejiandaaje kukabili mwaka 2016? Biblia inasemaje kuhusu
majira, nyakati na mwaka aliotupa Bwana?
Biblia
inatuambia katika kitabu cha Mhubiri 3:1-8 ‘kwa
kila jambo kuna majira yake, na wakati wa kila kusudi chini ya mbingu; Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda,
na wakati wa kung'oa yaliyopandwa; Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; Wakati
wa kubomoa, na wakati wa kujenga; Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati
wa kuomboleza, na wakati wa kucheza; Wakati wa kutupa mawe, na wakati wa
kukusanya mawe; Wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia; Wakati wa
kutafuta, na wakati wa kupoteza; Wakati wa kuweka, na wakati wa kutupa; Wakati
wa kurarua, na wakati wa kushona; Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena;Wakati
wa kupenda, na wakati wa kuchukia; Wakati wa vita, na wakati wa amani.’
Katika
mistari hiyo tunaona Biblia ikielezea vitu vingi ambavyo Mungu ameviumba na
kuviweka chini ya mbingu LAKINI vyote vimewekwa katika WAKATI (TIME) yake ndani
ya kusudi maalumu la Mungu. Maana yake ni kwamba kila kitu ambacho Mungu
amekiweka chini ya mbingu kipo/kimefungwa ndani ya muda/wakati wake maalumu na
haiwezekani kukatokea muingiliano, kwani wakati ndio UFUNGUO au ndio unao amuru
kitu gani kiwepo au kisiwepo. Huu ndio utaratibu wa Mungu aliouweka.
Kwanini Mungu ameweka utaratibu huo? Ipo
siri ya Mungu na muda, Muda na Mungu ni
marafiki tena wana mahusiano mazuri sana. Muda anaongoza maamuzi ya Mungu na
Mungu anaongoza matumizi ya muda kwa kuiweka mipango yake ndani ya mtu au
kuachilia majira Fulani katika mwaka na kumwagiza mwanadamu atekeleze hiyo
mipango/majira ndani muda sahihi aliokusudia.
Kwahiyo
hata katika mwaka 2016, ipo mipango na yapo majira, na nyakati Mungu aliyoamuru
Kuwepo na vyote hivyo vimefungwa katika muda ili viweze kutimia sawasawa na
mpango wa Mungu, na Mwanadamu ndiyo amepewa hiyo mamlaka ya kufahamu na
kuyatimiza yote lakini ndani ya wakati wa Mungu pekee. KWAHIYO Mwanadamu kamwe
hana wakati wakwake peke yake bali kila jambo ndani ya wakati (Time) pamoja na
Mungu aliye hai. Ms. 11 ‘Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; tena ameiweka hiyo
milele ndani ya mioyo yao…’
Unaweza jiuliza KUSUDI la
Mungu hapa ni nini? Ukiendelea Ms. 14 utapata jibu ‘Najua ya kwamba kila kazi aifanyayo Mungu
itadumu milele; haiwezekani kuizidisha kitu, wala kuipunguza kitu; nayo Mungu
ameifanya ili watu wamche Yeye’. Mungu ameyafanya hayo yote ili tu
Mwanadamu amche yeye pekee na si vinginevyo.
Je tunawezaje kuyafahamu majira na nyakati Mungu alizoamuru kwa
Mwaka 2016 ili tuweze kuishi sawa sawa na Mungu anavyotaka? Kama anayosema
katika neno lake Zaburi 32:8 ‘Nitakufundisha na kukuonyesha njia
utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama’.
Ukisoma
1 Wakorinto 2:9 -10 ‘Lakini, kama ilivyoandikwa, mambo ambayo
jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (wala hayakuingia katika moyo wa
mwanadamu,) mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao. Lakini Mungu
ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchungza yote, hata mafumbo ya Mungu’.
Kwahiyo njia peke ni kumuliza Roho wa Mungu peke yake ndiye aliye na uwezo wa
kutufunulia yote ili tuweze kujua.
Maelezo
ya Mtume Paulo yanatufanya tujue kwamba katika mwaka 2016 kuna mambo mazuri
ambayo Mungu amewandalia watoto wake na kwa njia ya Roho Mtakatifu tunao uwezo wa kutambua nini kinakuja kwenye kila
eneo la maisha yetu hata kabla hatujauingia mwaka husika.
Tambua
kwamba katika mwaka 2016 kila ufalme yaani ufalme wa Mungu (Nuru) na ule wa
Shetani (Giza) kuna mambo umeyaandaa/kusudia kwa ajili yako kifamilia, ndoa,
kazi, huduma, masomo, biashara, kanisa lako, taifa lako n.k. LAKINI Ni dhahiri kwamba Mungu amekusudia
mema kwa ajili yako kama Neno lake linavyosema katika Yeremia 29:11a ‘Maana nayajua
mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya,
kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho’. Shetani kama ilivyo asili
yake amekusudia mabaya juu yako.
Je, unakumbuka
matukio ya mwaka 2015 kwako binafsi, kifamilia, kikanisa, Kitaifa na dunia kwa
ujumla? Je, unajua katika ulimwengu wa
roho matukio hayo yameacha au kuzaa kitu gani? Naam chukua muda yatafakari
kibiblia na kisha jiulize laiti ungejua
kabla hujaingia mwaka 2015, kwamba hayo yaliyotokea yatatokea ungechukua hatua
gani?
Kumbuka
lolote unaloliona katika ulimwengu wa mwili linatokea ujue, lilishatokea kwenye
ulimwengu wa roho kwanza. Naam kwenye ulimwengu wa roho, ndipo una fursa ya
kuona mambo yanayoenda kutokea duniani, kabla hayajatokea. Ni katika ulimwengu
wa roho ndipo unaweza:-
(I)
kupambana ili kuhaikisha jambo jema ambalo
Mungu amekusudia linatimia. Pia,
(II)
kuzuia lolote baya ambalo Shetani amekusudia
juu yako, famila n.k katika ulimwengu huu wa mwili lisitokee.
Kutokana
na umuhimu wa kuwa na ufahamu wa nini kinakuja siku za usoni yaani mwaka 2016,
imenilazimu kuandaa ujumbe huu ili ukusaidie kujua angalau kwa sehemu 2016 ni
mwaka wa namna gani na ndani yake kuna nini? Hii itakusaidia sana kujua ufanye
nini ili kufanya maandalizi mazuri tushirikiana na kuyakabili yale
yanayokuja.
Kila
mwaka, ndani yake kuna mambo ambayo ni LAZIMA yafanyike au yatime kulingana na
nyakati ambazo zimeamriwa juu yako na Taifa pia (Rejea Mhubiri 3:1). Kwa mwaka
2016 yafuatayo ni baadhi ya mambo muhimu ambayo ambayo Roho wa Mungu
amenifunulia tujue Mungu alivyokusudia kwa ajili yetu watoto wake:-
1.
Ni
mwaka wa kuwekeza na kukusanya (kuweka akiba) Zaidi kwa kuwa kuna mabadiliko ya
kiuchumi yanakuja.
Biblia
katika kitabu cha Mwanzo 41:35-36 inasema ‘Na
wakusanye chakula chote cha miaka hii myema ijayo, wakaweke akiba ya nafaka
mikononi mwa Farao wakakilinde kuwa chakula katika miji. Na hicho chakula
kitakuwa akiba ya nchi kwa ajili ya miaka hiyo saba ya njaa, itakayokuwa katika
nchi ya Misri, nchi isiharibike kwa njaa’. Maelezo haya ya Yusufu ni
matokeo ya fasili ya ndoto ya Farao kiongozi wa Misri. Baada ya kupata tafsiri yake ilibidi Taifa la
Misri watumie miaka saba ya mwanzo kukusanya chakula kwa ajili ya miaka mingine
saba ya njaa iliyokuwa inakuja mbele yao.
Usiogope, binafsi, sikuelezi
kwamba pia katika Taifa letu kuna miaka saba ya njaa inakuja La hasha!. Hata
hivyo jambo ambalo nina uhakika linaenda kutokea ni mabadiliko muhimu ya
kiuchumi si tu wa nchi yetu bali Dunia nzima kuanzia mwaka 2016 ambayo yataleta
athari si tu kwa uchumi wa Taifa bali mpaka mtu mmoja mmoja. Mabadiliko hayo
kama yatakukuta haujajipanga vizuri kwa kuwekeza katika sekta na nyanja
mbalimbali za kiuchumi itakugharimu sana. Naam! mabadiliko haya yaliyoanza kwa
sehemu mwaka 2015 na kuendele kwa kasi mwaka 2016 yatakuwa mazuri kwa wale
waliojiandaa kuyakabili, na si vinginevyo (asomaye na afahamu).
Hivyo
nakushauri mpedwa katika mwaka 2016 fanya kila jitihada kuwekeza fedha, muda na
nguvu katika kuimarisha biashara zako, kazi zako, mifugo na zaidi kuongeza
vyanzo vingine vya mapato. Naam tia bidii sana katika kila utakalofanya kwa
mwaka 2016 ukimtanguliza Mungu.
Katika Kumbukumbu la Torati 8:18
imeandikwa ‘Bali utamkumbuka BWANA, Mungu
wako, mana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake
hata hivi leo’. Hivyo tarajia kupata mawazo mapya na yaliyo bora zaidi
yatakayokusaidia kupata utajiri katika mwaka 2016 kutoka kwa BWANA Yesu, naam
tegemea akili zako kutakaswa na hivyo kuwa na mawazo ya ubunifu na ufumbuzi
zaidi katika mwaka 2016 yatakayopelekea kukubalika na kuinuliwa kwako zaidi
kushinda wengine kazini kwako.
Kama
una mradi wako yaani duka au biashara yoyote usiridhike nayo ipanue zaidi au
kuongeza nyingine mpya, naam chukua hata mkopo upanue wigo wako ni muhimu sana
kwa kule tunakokwenda. Sambamba na hayo
anza sasa kuweka akiba ya fedha (endapo hufanyi hivyo) ambayo ni muhimu sana
kwa huko tunakokwenda, ni muhimu sana ukaweka akiba yako kwenye mifuko
mbalimbali ya kutunza akiba ya kijamii au ukawa na akaunti maalum kwa ajili ya
akiba.
N: B KUMBUKA
Tunza na zingatia sana Muda katika kila jambo, usipoteze muda kwenye mambo
yasiyo ya msingi kama kuangalia Tv, Sinema masaa 24. Tunza muda na tumia vizuri
muda wako, muda ni mali kwani muda ukipita hauridi tena na mafanikio yako yote
yamefungwa katika Muda kama Biblia inavyosema. Kufanikiwa au kutokufanikiwa
kwako kunategemea kwa kiasi gani umetumia muda wako vizuri.
2.
Ni
mwaka wa kucheka kwa kuwa BWANA anaenda kuwafurahisha watu wake wale
wanaomtegemea.
Ayubu 42:10 ‘Kisha BWANA akageuza uteka wa Ayubu, hapo
alipowaombea rafiki zake; BWANA naye akampa Ayubu mara mbili kuliko hayo
aliyokuwa nayo kwanza’. Ukisoma
kitabu cha Ayubu sura 1-2 utaona
habari za Ayubu na jinsi Shetani alivyoharibu maisha yake kwa ujumla. Kilikuwa
ni kipindi kigumu sana kwa Ayubu, hata hivyo hizo ndio nyakati zilizokuwa
zimeruhusiwa juu yake. Maandiko yanaonyesha kuwa baada ya Ayubu kusimama vizuri
na Mungu wake katika kipindi hicho kigumu, BWANA alimrejeshea Ayubu maradufu
kila kilichokuwa kimeharibiwa na Shetani yaani furaha, afya, watoto na mali
zake zote.
Vivyo
hivyo katika mwaka 2016 BWANA amekusudia kutimiza ahadi nyingi kwa watu wake
wanaomtegema, kile kilichoharibiwa kitarejeshwa, haki zilizopotea zinaenda
kurejeshwa, BWANA anaenda kurejesha uzima katika mwili wako nk. Kama ni familia
yako, ndoa yako, huduma yako, kazi yako nk Shetani aliharibu na kuteka, uwe na
uhakika BWANA Yesu anaenda kuponya na kurejesha uhai tena.
3.
Ni
mwaka wa amani utakaokupa fursa ya kujijenga na kutimiza mapenzi ya Mungu kwa
mwaka husika
1 Waflme 5: 3-5, ‘Umemjua Daudi
baba yangu jinsi asivyoweza kujenga nyumba kwa jina la Bwana, Mungu wake, kwa
sababu ya vita vilivyomzunguka pande zote, hata Bwana alipowatia watu chini ya
nyayo zake. Ila leo Bwana, Mungu wangu, amenipa amani kila upande; hakuna adui,
wala tukio baya. Nami, tazama, nakusudia kujenga nyumba kwa jina la Bwana,
Mungu wangu, kama Bwana alivyomwambia Daudi baba yangu, akisema, Mwana wako,
nitakayemweka katika kiti chake cha enzi mahali pako, ndiye atakayeijenga
nyumba kwa jina langu’.
Maneno
haya yalisemwa na Sulemani baada ya kutawazwa kuwa mfalme kufuatia kifo cha
baba yake Daudi. Ukisoma Biblia yako vema utagundua kwamba utawala wa Daudi
ulikuwa na vita sana, na kwa sababu ya vita na damu nyingi iliyomwagika katika
kipindi chake BWANA alimzuia Daudi asimjengee Hakalu. Hekalu lilijengwa kipindi
cha mwanawe Sulemani. Naam ili Sulemani
aweze kujenga hekalu vema, BWANA akampa
amani pande zote na kazuia baya lolote lisitokee.
Vivyo
hivyo Mungu anaenda kuleta amani juu yako kila upande katika mwaka 2016 ili
utumie fursa si kujijenga wewe binafsi bali kuujenga ufalme wake kwa mwaka
husika kwa kutimiza yale anayotaka kufanya juu ya Taifa, Kanisa, familia, ndoa
kupitia wewe. Hii haina maana kwamba Shetani hajapanga mabaya, tunafahamu
kwamba yeye ni baba wa uongo, lengo lake kubwa ni kuiba, kuchinja na kuharibu.
Amini
kwamba kabla Shetani hajatekeleza mipango yake BWANA ataizuia na kupigana kwa
ajili yako ili kutoathiri kusudi lake kupitia wewe kama alivyofanya siku za Mfalme Yehoshafati, aliposema “Hamtahitaji kupigana vita, jipangeni,
simameni, mkauone wokovu wa BWANA ulio pamoja nanyi, enyi Yuda na Yerusalemu; msiogope
wala msifadhaike; kesho tokeni juu yao, kwakua BWANA yu pamoja nanyi” (2Nyakati 20:125), naam hivi ndivyo
BWANA anavyoenda kuwashindia watoto wake katika mwaka huu.
Hakika
huu ni mwaka wako wa kujijenga kiuchumi, kibiashara, kifamilia, kikazi, kwa
kilimo nk. Ndio BWANA anaenda kuruhusu majira mazuri juu ya nchi yetu na kuzuia
kila uharibifu uliokusudiwa juu yetu.
Kwa
uchache na kadri Mungu alivyonifunulia siri hizi kwa habari ya mambo yanayokuja
siku za usoni katika mwaka huu. Hayo ni mawazo ya Mungu kuhusu watu wake na
kanisa kwa ujumla kwa mwaka 2016, na daima mawazo ya Mungu ni mawazo ya amani
(Yeremia 29:11), haya ambayo amesema nawe kuhusu 2016 unapaswa kuhakikisha
unayafuatilia mpaka yatimie juu yako na Taifa letu pia. Namna mojawapo ya kuhakikisha
haya yanatimia ni kujiwekea malengo ambayo yatatoa fursa kwa imani yako kuwa na
mahali pa rejea kadri unavyozidi kuukabili mwaka 2016.
TAMBAUA; Biblia katika kitabu
cha Waebrania 12:1 inasema ‘Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo
yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana’. Ni muhimu sana ukajiwekea utaratibu wa kuwa na malengo
ili yakusaidie kujua hatua zilizoko mbele yako ambazo unapaswa kuzifikia. Naam
si suala tu la kuweka malengo bali kuyaweka kwa kuzingatia kile kinachokuja
katika mwaka 2016. Natambua liko kundi kubwa la watu ambao wanaweza kuwa
walishaweka malengo yao hata hivyo bado una fursa ya kuyaboresha (adjust) kwa
kuzingatia hiki ambacho umejifunza katika ujumbe huu.
Malengo
yako yatakusaidia kujua hatua unazopiga endapo zinakufikisha kule ambako Mungu
anataka ufike katika mwaka 2016.
Maandiko
yanasema katika Isaya 60: 1 ‘Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, Na
utukufu wa BWANA umekuzukia’. Ukisoma msatri huu katika toleo la kiingereza la
ESV unasema ‘Arise, shine, for your light has come, and the glory of the LORD
has risen upon you’ (Isaiah 60:1). Neno ondoka ambalo kwa kiingereza ni ‘arise’
kwa fasiri ya kamusi ya kiebrania na kigiriki lina maana ya timiliza
(accomplish), maliza (complete), fikia lengo (achieve) au fanikiwa
(succeed).
Kwa
tafsiri hii ina maana kwamba, Mungu anayo mambo (mipango) ambayo katika mwaka
2016 anataka ufanikiwe katika kuyatimiliza na kukamilisha.
Naam
na ili uweze kuyafikia yeye anaenda kukulinda kwa kufanyika ukuta wa moto
utakaokuzunguka pande zote sawasawa na Zekaria
2:5 ‘Kwa maana mimi, asema BWANA,
nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka pande zote, nami nitakuwa huo utukufu ndani
yake’.
Zaidi
katika Mitahli 8:17 imeandikwa ‘Nawapenda wale wanipendao, Na wale
wanitafutao kwa bidii wataniona’. Ni imani yangu kama:-
(i)
Ukidumu katika kumpenda Mungu kwa kuzishika
amri zake
(ii)
Ukadumu katika kumtafuta
(iii)
Ukasimama vema kwenye nafasi yako kama mlinzi
basi uwe na uhakika haya ambayo leo Mungu ameyafunua kwako kuhusu mwaka 2016
yatakuwa dhahiri na mwaka huu utakuwa wa baraka za pekee kuliko yote
iliyotangulia.
Mungu
akubariki kwa kusoma na kuelewa maneno yake katika msisitizo huu, Biblia
inasema ‘wakati wasemapo kuna amani ndipo uharibifu uwajiapo’. Hivyo ni muhimu sana ukazingatia kumpenda Mungu
na kuwa makini na maisha yako kwa kila hatua kwa mwaka huu mpya 2016. Amen!!
*************************************************************************************