Leo tarehe 26 mwezi wa saba 2015 siku moja kabla ya kuanza mitihani ya mwisho wa muhula wa pili kwa mwaka wa masomo 2014/2015, imefanyika ibada ya pamoja katika ukumbi wa chuo MH.
Ibada hii ya pamoja kwa fellowship zote za kikiristo ilikuwa ni kwaajili ya kuwaombea wahitimu wanaohitimu mwaka huu kwenda kulitumikia taifa pamoja na maombi kwaajili ya mitihani inayoanza jumatatu ya kesho tarehe 27/5/2015.
Cannon MATONYA amefundisha neno la MUNGU na kuwataka wahitimu wote kuwa wakalitumikia taifa kwa uaminifu na kwa upande mwingine kwa wale wanaobaki na wanaohitimu waendelee kumsikiliza na KUMSHUKURU Mungu kwa mambo makubwa anayoyatenda katika maisha.
ZABURI 108:3-5 na WAFILIPI 4:8.